Ila Makongoro sometimes anaiaibisha sana familia ya Baba wa Taifa. Kila akipewa nafasi kuongea yeye anakomaa yale yale "nimepata nafasi si kwasababu nina uwezo, hakuna jambo la maana nililofanya la kunifanya nistahili kuwa Mkuu wa Mkoa", mara "wamenipa tu kwasababu ni mtoto wa Nyerere", halafu tena "nimepata upendeleo tu kupata hii nafasi".
Brother Makongoro, acha ujinga wa kujinyenyekeza kiasi hicho. Hiyo nafasi UNASTAHILI kabisa na wala siyo kwa ajili ya upendeleo. Unataka kusema akina Mchengerwa, Ridhiwani Kikwete, Hussein Mwinyi, Joseph Sokoine, Balozi Ali Karume wao wamepatwa nafasi hizo kwasababu wana uwezo mkubwa sana? Nakukubali bro, ila kadri siku zinavyosonga unazidi kunikera. Wao mbona hawaongei hayo unayoyaongea?
Nakuuliza, hao niliowataja hapo juu wamelifanyia nini Taifa hadi wastahili hivyo vyeo, halafu wewe usistahili?