Makopo ya taka ngumu yapandishiwe thamani

Makopo ya taka ngumu yapandishiwe thamani

robbyr

Senior Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
129
Reaction score
221
Kama mtanzania Kila Kona ninayopita baada ya mvua kunyesha nakuta mlundikano Wa MAKOPO ya vinywaji mbalimbali kutoka Kwenye makampuni makubwa hapa nchini.

Tukitambua kuwa hizo ni Moja ya taka ngumu ambazo haziharibiki kabisa.

Nina mapendekezo mengi namna ya kufanya MAKOPO haya yaweze kuisha kama mifuko ya plastiki ilivyoisha na hapa tutaendelea kuheshimu na kukumbuka uongozi Wa JPM.

PENDEKEZO LANGU: Kila kiwanda kinachozalisha iwe MO, AZAM, Kilimanjaro, au Uhai nk . Serikali ihakikishe Kila kopo litakuwa na thamani ya shilingi mia litakapouzwa baada ya kutumika lengo ni kutengeneza fursa na kuchochea watu kukusanya na kuuza wakijua faida ni kubwa licha ya Sasa Bado hayana thamani sokoni baada ya kutumika.

Tuache kutazama faida katika Kodi na kwa wenye viwanda na hivyo tutazame baadae ya kizazi kijacho nani atawafuta machozi kwa uchafu huo.

Pia, inaoneka MAKOPO ya rangi hayana thamani baada ya kutoka kiwandani mfano ya Energy Azam na Mo energy hivyo imechangia hayaokotwi na kuongeza taka ngumu mtaani naomba viwanda viweke mikakati ya kurudisha kwa kwa matumizi tena.

Pia MAKOPO kama rai tunaweza kukusanya na kutengeneza urembo mbalimbali kwani hii itachangia kupunguza ongezeko lake mtaani

Na mwisho, wasomi tuwe kielelezo Cha usafi kwani si ajabu kumwona msomi na mtu mwelewa anakunywa maji na kurusha Kopo bila kujali mazingira.

Asante sana.
 
Ni afadhali kopo la MO EXTRA mfano, maana ndilo linaongoza kwa kuchafua mazingira liwe na bei maalum,hiyo MO hata iuzwe elfu 1000 halafu kilo ya kopo used iwe buku sio mbaya tofauti na sasa hayauzwi popote,tutakuwa tumepungiza tatizo kwa 75%.
 
TENA MUWASHUKURU MATEJA NA WATU WENGINE WALIYOJIINGIZA KWENYE UOKOTAJI WA MACHUPA

ova
 
Kweli kabisa. Ni maamuzi ya viongozi kwani uchafu unatisha sasa hivi
 
Ni afadhali kopo la MO EXTRA mfano, maana ndilo linaongoza kwa kuchafua mazingira liwe na bei maalum,hiyo MO hata iuzwe elfu 1000 halafu kilo ya kopo used iwe buku sio mbaya tofauti na sasa hayauzwi popote,tutakuwa tumepungiza tatizo kwa 75%.
Kweli kabisa. Ni maamuzi ya viongozi kwani uchafu unatisha sasa hivi na u
TENA MUWASHUKURU MATEJA NA WATU WENGINE WALIYOJIINGIZA KWENYE UOKOTAJI WA MACHUPA

Dah!!! Kauli yako ngumu ila hatuna budi kuwashukuru
 
Back
Top Bottom