Makosa 10 tunayofanya wakati wa kulea watoto

Makosa 10 tunayofanya wakati wa kulea watoto

Joined
Aug 11, 2017
Posts
61
Reaction score
78
Makosa kumi wafanyayo wazazi wakati wa kuwalea watoto wao. Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu hivyo basi,tunapaswa kuwapokea kama walivyo na kuwapa malezi bora yanayostahili. Mwalimu wa kwanza katika malezi ya watoto ni mzazi.

Yafuatayo ni makosa kumi wanayofanya wazazi au walezi katika malezi ya watoto

1.Upendeleo kwa watoto.
Upendeleo huwa unawagawa watoto katika familia. Kwa mfano,mzazi anasema kwa kuwa wewe unafanya vizuri darasani wewe ndio mwanangu na wengine ni watoto wa nani?

Au kusema kwa kuwa wewe ni mtoto wa kiume basi wewe ni wa kwangu na watoto wa kike ni wa mama. Upendeleo unaanza kuwaathiri watoto kisaikolojia wanakufa taratibu na kujihisi hawana thamani.

2.Kuwatukana hovyo watoto.
yaani kuna watoto wanapitia wakati mgumu katika maisha sana wazazi wao kabisa wanawatukana matusi ya kila aina ambayo hata mtoto hastahili kuyasikia.

Watoto wanatukanwa matusi ya ajabu hatimaye anakua na kuona matusi ni sehemu ya maisha yake hivyo anakwenda naye kujenga jamii iliyo mbovu.Tokea mtoto yuko tumboni anasikia tu matusi jinsi mama yake anavyotukana bila hata ya kuona son

3.Kuwapiga watoto kwa hasira.
Kama tunavyojua kuwa falsafa ya hasira ni hasara. Mzazi anakuta amekwazika katikashughuli zake basi anaona hasira zake azimalizie katika kumpa mtoto mapigo yasiyostahili na hatimaye kumuumiza vibaya. Epuka kumpiga mtoto unapokua na hasira zako bali pumua kwanza hata kwa dakika tano kwani hutojutia maamuzi yako

4.Kutowajali na kuwathamini.
Imekuwa ni desturi watoto wa familia zingine wazazi hawawajali watoto kabisa yeye anajijali yeye kwanza
Kwa mfano,mtoto anaweza kudaiwa ada shuleni lakini mzazi anaona ni bora atoe hata ada nusu ili apate hela ya kunywa pombe.

Au wengine wanakula ada za watoto na hatimaye wanafukuzwa shule.Ni bora kutokuzaa kuliko kuzaa na kuja kuwapa watoto shida. Mzazi ni haki yako kumpatia mtoto mahitaji yake yote ya msingi. Mthamini mtoto kwa kumjali hata kuvaa mavazi nadhifu na ya heshima ili naye apendeze.

5.Kumwachia jukumu la malezi msaidizi wakazi.
Hili ni tatizo katika zama hizi mzazi anajua kuzaa na kumwacha mtoto akilelewa na dada wa kazi. Kwa namna hii mtoto atawezaje kupata upendo wa mama ? Kwanini unamlea mtoto kama watoto wa chupa au mdori ?

Hata kama una kazi hakikisha unapangilia muda wa kukaa na mtoto au watoto na kuwapa malezi bora. Acha tabia ya kumwaachia dada wa kazi kila kitu. Mtoto akiharibika unaanza kulalamika bila kujua wewe ndio kiini cha kosa.

6.Malezi ya kidini.
Mfundishe mtoto dini ya kiislamu aijuwe ili asijiingize kwenye makundi mapotofu. Mtoto akikosa dini huyo umeshampoteza. Dini ndio Dira ya binadamu wote. Ingia hapa kwa ajiri ya kuangalia malezi ya watoto wa kiislam.

7.Kutowasimamia katika masomo yao.
Watoto wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wazazi wao ili kuweza kufika pale wanapotaka. Wazazi mnatakiwa kuacha tabia ya kuwaachia walimu kila kila katika mambo ya darasani.

Kuwa mwalimu wa kwanza kwa mtoto wako hakikisha unamkagua na kujua nini amejifunza kila siku na
kumsaidia kazi za nyumbani. Wasimamie siyo kuwaua watoto kwa kuwaachia uhuru wa kuangalia tv na kusahau masomo yake muhimu.

8.Kutowapa watoto muda.
Hakuna zawadi kama muda ambayo unaweza kumpatia mtoto na akahisi unampenda. Kisaikolojia mtoto anafurahi mzazi anapokua naye anahisi unampenda na unamjali. Changamoto ya watoto siku hizi ni wazazi kutowapatia watoto muda wa kukaa nao. Mzazi anawahi kuondoka na kuchelewa kurudi.

Hata kama kuna kitu anataka kukuambia na kugundua kipaji kwa mtoto unashindwa kabisa. Acha kuua kipaji cha mtoto na kutompatia muda wa kukaa naye.

9.Kuwakosoa na kutowasikiliza.
Kukosolewa kwa mtoto ni kumdoofisha kiakili kabisa. Mtoto anatakiwa kusikilizwa na kutiwa moyo na kumpa faraja katika kitu alichofanya. Kukosea siyo kushindwi bali kufanya makosa ndio mwanzo wa kujifunza.

Usimkosoe mtoto vibaya bali mtie moyo na kumuonesha njia sahihi ya kupita ni ipi ili aweze kufika. Huwezi kuwa mtaalamu wa kitu Fulani bila kufanya makosa. Makosa ni sehemu ya kujifunza.

10.Kuwalaani watoto.
Wazazi wamegeuka kwa kuwa laana kwa watoto wao na siyo Baraka. Mzazi anamlaani mtoto wewe huwezi kufanikiwa. Wewe huwezi kufanya chochote yaani anamjengea mtoto vizuizi vya kutotimiza ndoto yake.

Kwa mfano,wewe utaweza wapi wewe ni wa kufeli tu,kama Fulani alifeli wewe ndio utaweza ? Maneno ni mabaya sana yanamuuza mtoto moyo kabisa na kumkatisha tamaa na kumjengea hofu ya maisha.

Zingatia kauli hii. [emoji116][emoji116][emoji116]
mtoto huathirika kwa kile anachokiona na kukisikia.
 
sijiungi tena yani ni ubaguzi kwanza kwa mleta uzi huu dini kwani ni moja peke yake ndo inafundisha maadili ya watoto.
 
Umeharibu kwenye dini wewe ni gaidi bila shaka
fd545e3a9bc88fd6a0792a8e728f05d9.jpg



Mimi sio gaidi ila kuna mkristo alichokifanya sio kizur nafikiri huyu sasa ndio gaid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kajifujnze maana ya uchochezi na jiulize mchochezi ni nani? kama usipo jikuta kwenye hilo kundi
 
Umefundisha vzr japo ingekuwa vema kama ungesema mtoto afundishwe Dini (pasipo kutaja dini gani) ili kuonesha dini ina nafasi kubwa kwenye malezi. Kwa kutaja dini moja umeonesha Dini zingine hazitoi mafundisho kwa watoto.

Philips X2560
 
Back
Top Bottom