Makosa ambayo hayana dhamana kisheria Nchini Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kifungu cha 148(5)(a) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 kinasema;

Afisa polisi ambapo mtuhumiwa anashikiliwa au mahakama ambapo mtuhumiwa amepelekwa kusikiliza shauri lake, haitoruhusiwa kutoa dhamana kwa mtu ambaye ameshtakiwa kwa makosa YAFUATAYO;

1. Mauaji
2. Uhaini
3. Unyang'anyi wa kutumia silaha
4. Unajisi
5. Ugaidi
6. Utakatishaji fedha
7. Biashara ya dawa za kulevya. n.k




Source: Jungu la Sheria Tanzania
 
Uhaini ni pale mtu anapotenda jambo dhidi ya nchi yake. Kwa mfano, mtu anaweza kuisaidia nchi nyingine ipigane vita dhidi ya nchi yake kwa kutoa habari za siri.
Kifupi ni kua msaliti kwa Taifa lako
Vipi serikali ikisaliti wananchi? Huo Ni uhaini?
Wote tunajua hakuna nchi bila wananchi.
 
Vipi serikali ikisaliti wananchi? Huo Ni uhaini?
Wote tunajua hakuna nchi bila wananchi.
Ndio maana tanakata katiba mpya ili hawa wala asali wote waonje joto ya jiwe na wafilisiwe.
 
Uhaini ni pale mtu anapotenda jambo dhidi ya nchi yake. Kwa mfano, mtu anaweza kuisaidia nchi nyingine ipigane vita dhidi ya nchi yake kwa kutoa habari za siri.
Kifupi ni kua msaliti kwa Taifa lako
Umekosea,treason ndio uhaini lazima kuwe na njama za kupindua au kuua kiongozi wa nchi usika hata kama haujahusisha nchi nyingine
 
Nimetoka kusoma uzi unaomuhusu daktari wa amana moja ya mashtaka yake ni ulawiti lakini amepewa dhamana,hii imekaaje?
 
Sasa yule Daktari wa Amana aliebaka na kulawiti mtoto wa miaka 17 mbon kapewa dhamana? Au hawa majaji na mahakimu wanabaka na kulawiti hizi sheria? 😬
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…