Makosa ambayo yanafanywa na waajiriwa juu ya fedha

Makosa ambayo yanafanywa na waajiriwa juu ya fedha

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
384
Reaction score
758
Mara nyingi kabla ya kuajiriwa au wakati wa kuajiriwa kunakuwa na mafunzo ambayo mara nyingi tunapewa na miongoni mwa somo ambalo tunafundishwa ni namna y kujiandaa kustaafu wakati unaajiriwa.

Ni soma ambalo wengi wetu hatuelewe, unapoambiwa kwamba ujiandae kustaafu wakati ndio unaaza kazi na ukipiga hesabu unamiaka 30s ya kufanya kazi ?

Nilichokuja kujifunza juu ya hiyo semina ni kwamba kufikiri juu ya matumizi ya fedha yako.

Kwanini nasema hivyo kwa sababu mshahara unapoonza unakuwa ni mkubwa kwa sababu hauna majukumu

Maamuzi juu ya mshahara wako yanakuwa ni ya kwako hauna mtu wa kukushauri juu ya matumizi ya fedha yako

Matumizi ya fedha yako yanazungukwa na wale ambao wanakuzunguka

Kosa kubwa ambalo tunafanya
Kosa kubwa ambalo tunafanya waajiriwa ni kuamini kwamba wote tunalingana kwa sababu wote tuko ofisi moja?

Unapomwaona mwenzako kanunua gari na wewe unataka kuwanalo kwa sababu wote mnamshahara sawa laki haujui mwenzio kwao yukoje?

Vijana wengine wamejikuta wakichukua mikopo mikubwa na kununua gari kwa ajili ya matumizi binafsi

Kununua gari sio kitu kibaya , ila inategemea na majukumu ambayo huko nayo

Makosa ambayo tunafanya waajiriwa wapya

Kununua gari kwa njia ya mkopo asilimia kubwa ya waajiriwa tunanunua magari kwa njia ya mikopo

Kununua gari kwa mkopo sio mbaya , mbaya nikutumia asilimia 30% kununua gari wakati bado haujafanya tathimini juu ya kugharamia gari

Wakati tuko ofsini kuna watu tulikuta wanamiaka 10 na kuendelea hawana magari au wanamagari ya kawaida tu

Tuliona kwamba labda hawa wazee hawajui umuhimu wa kuwa na gari

Lakini tulichobaini gari unayonunua 20 milioni baada ya kununua thamani yake inashuka kila mwaka na gharama za kuendesha zinakuwa kila siku

Unapotumia asilimia 30% ya mshahara kwa gari na kuongeza matumizi ya gari wakati huko pekee yako inawezekuonekana sio kitu sa a ila unapoanzisha familia ndio unajua umuhimu wa ile asilimia 30

Kwa sababu kadri majukumu yanaongezeka, mshahara ndivyo unavyoonekana hautoshi na unapelekea watu wengi kuingia kwenye mikopo ambayo sio ya lazima

Ni muhimu kabla ya kufanya maamuzi yako ya kwanza ya kukopa fedha kujiuliza maswali kwamba kuna umuhimu ganu kuwa na gari na kuna faida gani utapata kwa kuwa na gari zaidi ya statues yako

Kununua gari sio kitu kibaya ila kama ni uko mwanzo wa utumishi wako nakushauri usinunue gari kwanza jaribu kuwekeza au kufanya tathimini ya kuwa na gari baada ya miaka 5 ya utumishi wako utaona umuhimu na unaweza kufanya maamuzk yaliyo sahihi.

Changamoto nyingine ni aina ya gari unayonunua

Pale unapofikia uwezo na utayari wa kununua gari, angalia ni aina gani ya gari unayotaka, mfano wewe uko mikoani na unajua tu mafundi walioko ni wazuri kwenye vitu vya mechanical unakwenda kununua magari ya umeme ?

Tukiwa tunaanza kazi tulishangaa unakuta bosi anamiliki IST lakini tukllikuja kujua kwanini walikuwa wanamiliki magari maduku IST au Carina nk

Kama ni gari yako ya kwanza hakikisha unanunua toyota kama ndio unanua gari ya kwanza utakuja kinishukuru
 
Back
Top Bottom