Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Historia ya uhuru wa Tanganyika itachukua miaka mingi hadi itulie na watu waseme hakika hii sasa ndiyo historia yetu.
Leo katika pita pita yangu nimekuta kitabu hicho hapo chini, ''The Media History of Tanzania,'' (1998) kikieleza historia ya magazeti toka enzi ya Wajerumani.
Kitabu hiki kimeandikwa na Martin Stummer na kimechapwa na Ndanda Mission Press.
Kilichonigusa ni pale niliposoma pale palipoandikwa kuwa gazeti la Zuhra lililokuwa likimilikiwa na Ramadhani Mashado Plantan na ndiye alikuwa mhariri wake na kuchapwa Mtaa wa Ndanda Mission Quarter liliacha kuchapwa mwaka wa 1950.
Hii si kweli.
Laiti ingejaaliwa kuwa hivyo Julius Nyerere na chama cha TANU kingepata shida kubwa kufahamika kwa wananchi.
Zuhra ndilo lilikuwa gazeti la kwanza kumtangaza Nyerere na TANU na hii ilikuwa mwaka wa 1954 na nakala za gazeti hili zipo Maktaba ya Chuo Kikuu, East Africana kwa mtafiti yeyote kusoma.
Mimi binafsi nimeziona baadhi ya nakala za Zuhra nyumbani kwa mjane wa Mashado Plantan Bi. Asha nyumbani kwake Mtaa wa Lindi na Nyamwezi katika miaka ya 1980.
Huyu mama alikuwa amehifadhi baadhi ya vitu vya marehemu mumewe na moja ni nakala chache za Zuhra.
Kilele cha gazeti la Zuhra katika historia ya gazeti hili ni kuandika mkutano wa Nyerere alipotoka UNO safari ya kwanza na kufanya mkutano mkubwa sana Mnazi Mmoja.
Gazeti hili la Machi 1955 nimelishika kwa mikono yangu na nimelisoma wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.
Historia ya Mashado Plantan na mchango wake katika uhuru wa Tanganyika na jinsi gazeti lake Zuhra lilivyousanifu mkutano wa Nyerere baada ya kurudi UNO nimeuandika kwa kirefu katika kitabu cha Sykes.
Mashado Plantan kweli hayuko katika historia ya uhuru lakini ikiwa sasa hata watafiti wanafanya makosa kama haya historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika inazidi kudidimizwa.

5Salma Said, Nasoro Omary and 3 others
1 Comment
2 Shares