Albashiri
New Member
- Aug 28, 2022
- 2
- 1
UTANGULIZI ;
Kwa jina naitwa Albashiri (0652472119 ) mjasiriamali ambaye napambana na maisha ya kuitafuta pesa, katika kuitafuta hiyo pesa tangu nikiwa chuo nilijaribu njia nyingi ikiwemo kuhifadhi hela kutoka hela ya malazi ninayopata nikiwa chuoni ,kutoa huduma za fedha kwa njia ya mitandao ya simu kama M-pesa ,kujaribu biashara za mitandaoni na pia kilimo ,yote hayo ni katika kuipata pesa ,sijafanikiwa kiasi hicho ila nimepata kujifunza vingi katika kutafuta kuimiliki pesa, kwa uzoefu wangu binafsi kama mpambanaji , kupitia kusoma vitabu mbali mbali na kuhudhuria semina mbali mbali juu ya kuelimisha vijana hasa kujitegemea na hatuwezi kujitegemea kama vijana bila kuwa na pesa za kufanya ivo ,mana pesa ndo kitu cha muhimu unapotaka kujitegemea ,bila pesa huwezi kujilisha ,kujivisha , kustarehe ,kulipa kodi na kufanya mengine mengi katika maisha .Na ndiyo mana nikasema niweke mawazo yangu hapa ambayo yatatusaidia katika kuhakisha tunatambua ni wapi tunakwama katika kuimiliki pesa hasa sisi vijana
MAKOSA KATIKA KUIMILIKI PESA
Yafuatayo ni baadhi ya makosa ambayo huwa tunayafanya hasa katika kutaka kuimiliki pesa
(1) Kutumia zaidi ya kile unachokipata ,kuwa na matumizi yanayozidi au kuwa sawa na unachoingiza,matumizi kuwa sawa na unachokipata itakufanya kila hela unayoipata unatumia na hamna unachoweza kuweka kama akiba kwa matumizi ya dharura au kuanzisha biashara yani maisha ya kuwa unachokipata ni kukitumia kama kilivo ,kwa tabia ya hivi itakuwa ngumu kuondokana na changamoto ya pesa utakuwa unapambana kuitafuta lakini hauipati ni kwa sababu ukiipata unaitumia kama ilivo ambapo inakuwa sio rahisi kuimiliki hiyo pesa kwa kuwa nayo ya kutosha. Ukitaka kuondokana na changamoto ya pesa jitahidi matumizi yawe chini sana hata ikibidi iwe haizidi 60% ya pesa unazoingiza
(2) Kukopa pesa ya riba kubwa ili kuanzisha biashara ,kuna taasisi nyingi hasa kwa Karne hii ambazo hushawishi hata raia wa kawaida kukopa lakini riba zao sio rafiki hasa kwa mtu ambaye ndo kwanza anaenda kuanza biashara ,kukopa fedha ambayo ulipaji wake ni mgumu tena wa gharama kubwa ni kama kujiandalia kufilisika au kuwa chini ya hapo ulipokuwa mwanzoni ,tunatakiwa kuangalia aina ya mikopo ya kuchukua na hali za biashara ya unayomiliki na utawezaje kurudisha hilo deni ,na wakati mwingine tupendelee kuanza chini hata kwa mtaji wa kawaida kama laki 1 mpaka laki 7 hii unaweza hata ukapambana kwa njia nyingine kuipata ili uanze biashara ako .Unaweza hata kuazima pesa kwa mzazi ndugu ambao naamini kama watakusaidia itakuwa nafuu tofauti na pesa za kukopa kwenye taasisi ambapo wako na mwisho wa muda wa kulipa ,kwa ndugu kama wanakupenda na wanataka ufanikiwe kitu kama riba lazima kitakuwa ni nafuu na wataweza kukuelewa hasa pale unapokuwa unaendesha biashara ako kwa hasara ,kwa hiyo kijana kabla hujakopa pesa uanzishe biashara angalia unakopa wapi ? Kwa ajili ya kuanzisha nini ? Na unaenda kufanyia wapi ? Na ikitokea umepata hasara utawezaje kuendelea kusimama kiuchumi ? Na uliyemkopa atakuelewaje utakapoanza kusua sua kulipa deni lake ? Ukishajiuliza hayo ni rahisi kutambua ni upi mkopo wa kuchukua na ni wapi ambapo utaona afadhali kwa ndugu au mzazi kama anazo huwa litakuwa Kimbilio.
(3) Kutumia pesa ambayo bado haijawa mikononi ,yani kutumia pesa ambazo bado hazijawa katika umiliki wako kama vile kuwa mfukoni kwako au kwenye akaunti zako za benki , kwamba unapangia bajeti pesa bado hujaimiliki ,kwenda dukani kufanya matumizi ambayo unasubiri upate pesa fulani ndo uje ulipe ,kuahidi mtu pesa ambayo na wewe umeahidiwa .Ikitokea hiyo pesa haijakufikia mikononi kwa sababu mbalimbali itakufanya ushindwe kulipa deni la watu na hii ndo itakuingiza kwenye migogoro na watu hasa wale uliowaahidi kuwalipa ukijua akilini ukishaipata,na hiyo migogoro inaweza sababisha kukosa imani ya kusaidiwa siku nyingine ukihitaji msaada na kama mtu anayetaka kumiliki biashara unahitaji kujenga imani na imani kwenye pesa huwa unachoongea inatakiwa iwe kweli ,umeahidi mtu nitakupa pesa kama haki yake mpe kweli ,umekopa hela na kuahidi unarudisha baada ya wiki mbili basi fanya hivo ili uje usaidiwe siku nyingine ,na pia kufanya matumizi ya pesa kabla haijakufikia mkononi itakufanya kila unapoipata unaitoa kwa haraka na haitakaa kwako na hivyo kukufanya kuendelea kuwa na uhaba wa pesa ,kwa hiyo jitahidi kutofanya matumizi ya pesa ambayo hata haipo kwenye miliki zako hata kama ni zako unazisubiria ,fanya tu pale inapokulazimu kama kupata chakula au matibabu mana hivo vitu huwa haviepukiki
(4) Kufanya matumizi ya pesa kabla ya kutunza ,yani hapa unafanya matumizi ya pesa itakayobaki ndo utunze ,unachopata unakitumia kwanza ndo kitakachobaki utakitunza na mara zote huwa hakibaki ,mfano mdogo kwa watu wanaofanya michezo ya kubahatisha kamari wapo wanaoshinda tena mpaka mamilioni ya pesa na sio mara moja au mara mbili ni mara nyingi tu lakini ukiangalia uchumi wao ni wa kawaida tu kwa walio wengi ,na pia kuna mtu unasimuliwa kuwa alianza biashara ya kuuza viatu barabarani lakini saa ivi ana maduka makubwa mjini ya kuuza vitu mbali mbali vya mitindo, mfano mwingine mwepesi juu ya utajiri wa bakhresa kuwa inaaminika alianzia kwa kuuza viatu japo hatujui alianzaje ila uhakika ni kwamba alianzia chini zaidi ya hapa alipo, ndo tunapokuja suala la bajeti yako na pesa, wengi huwa tunasubiri tupate pesa ndo tupange manake tusipopata hatutapanga chochote, na ukiwa hivi hauwezi kuimiliki pesa kirahisi mana hata ukiipata wakati unaipangilia na yenyewe itaanza kukushawishi kupanga ambavyo hata sio vya lazima katika maisha, mfano mimi nimesoma vitabu mbali mbali ikiwemo cha P.T.Barnum cha art of money getting na baadae nikasoma kitabu cha Mbinu za kuongeza kipato; Maarifa juu ya kuongeza fedha,biashara na uwekezaji katika sura ya siri ya kupanga bajeti yenye kukusaidia kuishi ndani ya kipato chako ukurasa wa 32 kilichoandikwa na kijana mtanzania Joel Nanauka katika sehemu ya namna ya kupanga bajeti binafsi ,baada ya kukisoma nikachukua mawazo ya hawa watu wawili nikaja na mawazo yangu kwamba lazima niwe na bajeti ya ivi ili nipunguze changamoto ya pesa na bajeti yenyewe imekaa ivi katika hela angu ninayoingiza kwa mwenzi ;50% ni matumizi ya lazima kama kodi chakula na mavazi ,25% kuwekeza katika biashara yangu ,5%sadaka ,15% starehe kama kutumia na mpenzi wangu na kwenda sehemu za matembezi binafsi ,5% akiba kwa ajili ya dharura kama nikipata msiba au ikitokea kusafiri kwa dharura manake hela itatoka hapa ,ipangilie pesa kabla hujaipata ,jiwekee vipaumbele ,kipi cha kuanza unapopata pesa ako na wala hela isikupangie ufanye kipi
(5) Kupendelea kuomba pesa kuliko kuomba maarifa ya kuipata hiyo pesa ,mfano unapata nafasi ya kukutana na mtu tajiri wengi cha kwanza hufikiria sana kuomba pesa kuliko kuomba maarifa ya na yeye atawezaje kuipata pesa na ndo mana tunafurahi sana kupewa pesa kuliko kupewa maarifa juu ya juipata pesa ,vijana wengi wako hapa yani tunaangalia sana wapi tunapata pesa kuliko wapi tunaweza kujifunza namna ya kuipata pesa ,mtu anaweza kuishi na bosi wake kwa miaka zaidi ya 10 lakini bado uchumi wake ukawa wa kawaida au ule ule ni kwa sababu anafurahia kupewa anachotaka katika kutimiza matumizi ya maisha kama kula vizuri ,kulipa kodi na kutembelea sehem za starehe ambapo wakati mwingine mlipaji huwa ni bosi mwenyewe ,yani kupenda kitonga cha kupewa tu lakini hujifunzi nawezaje na mimi kukipata ? Na ndo mana tunawapenda watu wanaotupa pesa kuliko wale wanaotuelekeza namna ya kuipata pesa ,tunawapenda wanaotupa njia kuliko wanaotuelekeza namna ya kuitengeneza njia wenyewe ,kusaidiwa pesa ni jambo nzuri ila ni vyema ukasaidiwa pesa na wewe hiyo ikakusaidia kujitengenezea nyingine ,mfano unaweza ukawa na wazo nzuri la biashara ukampa mtu mwenye pesa akakusaidia pesa ili uanzishe hilo wazo manake hapo umeomba pesa lakini kwa ajili ya kutengeneza pesa nyingine
(6) Kufurahia kupata pesa unayolipwa /kupokea na kuiweka benki bila kufanya uwekezaji wowote yani kijana una ajira unalipwa mwisho wa mwezi na furaha yako kubwa ni kuona hela unazotunza zinaendelea kuongezeka benki kila mwisho wa mwezi mwingine na mwingine ,hii huwa itakufanya uendelee kuwa na changamoto ya pesa ,njia nzuri ni kuwa na bajeti ya hela unayoipata kwa kila pesa unayoingiza jitahidi asilimia kadhaa unawekeza ili pesa unayopata iweze kuleta pesa nyingine tena na tena hii itasaidia kupunguza changamoto ya pesa.
Mfano wa kupanga bajeti nimeuelezea katika kosa namba 4 ,usiogope kuingia hasara mana hata waliofanikiwa wote walipoteza kwanza ndo wakapata ,walipoteza muda ,afya na pesa ndo wakawa hivi tunavoona kama ndo wamefanikiwa mfano ni rahisi bilionea mpya wa migodi ya madini ya tanzanite mererani wilayani simanjiro mkoani manyara katika mahojiano yake ,bilionea Anselim Kawishe alisema kuwa huu ni mwaka wa 15 ndo anapata faida miaka yote alikuwa anaendesha kwa hasara na ilifika wakati aliwashauri wezake wauze mgodi wagawane ili kila mtu angalau akaanzishe biashara nyingine yenye faida ila wezake walimkatalia walimwambia tupambane ivo ivo ipo siku tutafanikiwa ambapo ndo mwezi huu wa nane akatangazwa kama bilionea mpya kwa kifupi usiitunze mbegu ipande ili ikuletee mbegu zingine nyingi
(7) Kutembea na pesa ambayo huna matumizi nayo ,hii inaweza kukushawishi kufanya matumizi yasiyo ya lazima mana pesa uko nazo kwa wakati huo ,pendelea kutembea na pesa ambazo unaenda kuzitumia tu labda na ziada kindogo ila isiwe pesa nyingi ambayo siyo ya kwenda kutumia mara zote zitakupangia kufanya kitu ambacho hukupanga na wala hata hakukuwa ulazima wa kufanya hivo
HITIMISHO; Hizo ni baadhi tu ya makosa ambayo tunayafanya tunaona ya kawaida kumbe ndo chanzo cha sisi kushindwa kufanikiwa katika suala nzima la kuimiliki pesa angalau za kutosha

Upvote
0