Makosa katika uandishi wa maneno

Makosa katika uandishi wa maneno

Mama

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2008
Posts
2,848
Reaction score
64
Si sahihi kuandika maharifa, maalifa: Sahihi ni maarifa
Si sahihi kuandika hushahuri, ushahuri, ushauli: Sahihi ni ushauri
Si sahihi kuandika agharabu, Hagalabu: Sahihi ni aghalabu*(aghlabu)
Si sahihi kuandika hunaweza: Sahihi ni unaweza
Si sahihi kuandika hutakayo: Sahihi ni utakayo
Si sahihi kuandika Mahabara, maabala: Sahihi ni maabara
Si sahihi kuandika munaweza: Sahihi ni mnaweza

n.k
 
haya maneno mara nyingi hukosewa sana kila siku,sasa sijui tuseme ni common mistakes au ni uzembe. Mimi nadhani kuna kauzembe fulani hivi kanako sababisha waandishi wengi kutohoa maneno wasiyo yajua.
 
Its good to learn through mistakes than from no mistakes.

Because if one has not made a mistake in his/her entire life rest asured that he/she has never tried up a new thing in his/her entire life. Now this is bogus and boring!!!

If you fail 1000 times while doing something then correct translation or inference is that there is 1000 WAYS of failure in accomplishing a particular task. That is the importance of failures and mistakes.
 
Last edited:

How do you know that you are making mistakes?
 
How do you know that you are making mistakes?

If you do not find any problems/challenges doing something or rather say in accomplishing issues rest asured again you not doing it right! That is when you will realise you are making mistakes!

Anyway tks mama!
 
kwa mfano mimi kama mimi mwenyewe binafsi uwaga nafikili akuna hanayejua kua hanakosea adi aambiwe kua hanakosea au hajifunze kujuwa makosa.
 
kwa mfano mimi kama mimi mwenyewe binafsi uwaga nafikili akuna hanayejua kua hanakosea adi aambiwe kua hanakosea au hajifunze kujuwa makosa.

si kweli mara zote tunapo kosea huwahatujui, mpaka adi uambiwe. kuna mifano mingi, kama wakati wa mitihani shuleni unafanya swali ukiwa na uhakika na njia unavyojibu baada ya kutoka tu kwenye mthiani hata haujaambiwa na mtu,unagundua kabisa pale kwa njia ile nimkosea. au mfano mwingine mfalme daudi alifanya kosa hatahajaambiwa na mtu alianza mipano ya kuficha makosa yake, kwa kifupi unapokosea haiitaji mara zote kuambiwa na mtu umekosea majibu kwa uliyo tenda ni jambo tosha kukujulisha. labda uwe unamaanisha kukosea katika lugha hapo sina neno
 
Si sahihi kuandika maharifa, maalifa: Sahihi ni maarifa
Si sahihi kuandika hushahuri, ushahuri, ushauli: Sahihi ni ushauri
Si sahihi kuandika agharabu, Hagalabu: Sahihi ni aghalabu*(aghlabu)
Si sahihi kuandika hunaweza: Sahihi ni unaweza
Si sahihi kuandika hutakayo: Sahihi ni utakayo
Si sahihi kuandika Mahabara, maabala: Sahihi ni maabara
Si sahihi kuandika munaweza: Sahihi ni mnaweza

n.k

Haya si makosa ya maneno, bali ya uundaji sentensi
Nilikwenda nikamkuta hayupo...
Kwa niaba yangu binafsi
 
Haya si makosa ya maneno, bali ya uundaji sentensi
Nilikwenda nikamkuta hayupo...
Kwa niaba yangu binafsi
kama ni makosa ya uundaji wa sentensi, je makosa haya yaendelee kuwepo na kutumika? kama sivyo nini kifanyike.

Hofu ni kuwa makosa katika utumiaji wa maneno au hata katika uundaji wa sentensi yatapelekea kwenye kuharibu (deformation) ya lugha hii.
 
kama ni makosa ya uundaji wa sentensi, je makosa haya yaendelee kuwepo na kutumika? kama sivyo nini kifanyike.

Hofu ni kuwa makosa ya utumiaje wa maneno au hata iwe uundaji wa sentensi yatapelekea kwenye kuharibu (deformation) ya lugha hii.

Ni makusudi kabisa mama mtu anaharibu kiswahili kwani katika hata kuongea huwezi sema ::hunayo:: ukiimaanisha ::unayo:: Mdomo unakataa unless you are lazy learning guy!
 
Ni makusudi kabisa mama mtu anaharibu kiswahili kwani katika hata kuongea huwezi sema ::hunayo:: ukiimaanisha ::unayo:: Mdomo unakataa unless you are lazy learning guy!

Nini kifanyike kuhakikisha haya makosa ya makusudi yanapungua kama sio kutotokea?
 
Nini kifanyike kuhakikisha haya makosa ya makusudi yanapungua kama sio kutotokea?

Katika pita pita yangu wakati nikitafakari hili la kiswahili na nini kifanyike nilipata kutembelea China Radio Station ambayo huwa na program tele za kiswahili na hata website yao ni ya kiswahili fasaha. Sasa sisi watanzania ndio maan tunatawaliwa na kuamini sana na kusujudia weupe kuwa eti wao wana-akili sana. Hakika sii akili sana bali ni commitment tu. Kichina kilivyo kigumu na hata kijapani ambacho niko kwenye mafunzo nacho ni kigumnu has kuandika; lakini watu hawa wajua kiswahli kulikoni waswahili wenyewe. Siku moja mchina atakuja ataongea halafu tutamwuliza unamaanisha nini? It will be a shame!! Waweza pia tembelea website yao http://swahili.cri.cn/

Nini kifanyike mama tuache uvivu kuwa anyway things will just get moving despite the less effort we put on. Believe me things will soon not work out if you do not commit yourself into it very soon na hapo ndio kinachotakiwa kufanyika kitafanyika and with great losses and pain.
 
Katika pita pita yangu wakati nikitafakari hili la kiswahili na nini kifanyike nilipata kutembelea China Radio Station ambayo huwa na program tele za kiswahili na hata website yao ni ya kiswahili fasaha. Sasa sisi watanzania ndio maan tunatawaliwa na kuamini sana na kusujudia weupe kuwa eti wao wana-akili sana. Hakika sii akili sana bali ni commitment tu. Kichina kilivyo kigumu na hata kijapani ambacho niko kwenye mafunzo nacho ni kigumnu has kuandika; lakini watu hawa wajua kiswahli kulikoni waswahili wenyewe. Siku moja mchina atakuja ataongea halafu tutamwuliza unamaanisha nini? It will be a shame!! Waweza pia tembelea website yao china radio international

Nini kifanyike mama tuache uvivu kuwa anyway things will just get moving despite the less effort we put on. Believe me things will soon not work out if you do not commit yourself into it very soon na hapo ndio kinachotakiwa kufanyika kitafanyika and with great losses and pain.

Asante,

je unaweza kuelezea kwa undani hayo maandishi yaliyokolezwa.
 
...lakini watu hawa wajua kiswahli kulikoni waswahili wenyewe. Siku moja mchina atakuja ataongea halafu tutamwuliza unamaanisha nini? It will be a shame!!

Nini kifanyike mama tuache uvivu kuwa anyway things will just get moving despite the less effort we put on. Believe me things will soon not work out if you do not commit yourself into it very soon na hapo ndio kinachotakiwa kufanyika kitafanyika and with great losses and pain.

Cha kufanya, Mshiiri, labda ungeongoza juhudi hizo, kwa, kwanza kabisa, kutumia Kiswahili katika mjadala kuhusu matumizi ya Kiswahili, kwenye tundiko linalokemea wavivu wa matumizi fasaha ya Kiswahili.
 
Mama na Kuhani sasa itabidi hapa pia tupitie kwa pamoja kila thread na post na kurekebisha kiswahili. Labda kwa kuanzia hapa. Kwani kuna msemo wa kiingereza usemao "charity begins at home" Unajua mtu akiandika kiswahili kikawa kimekosewa na ikawa inarudia rudia hata kiingereza atakuwa hajui vyema na hata lugha ya mama yake itakuwa inampa shida kwani ni mtumwa wa lugha. Ni vicious cycle kind of thing. Mtu hajui lugha ya mama vizuri, na hivyo kiswahili kinampa shida kwa kuwa language skills inakosekana kutoka kuzaliwa na malezi, na finally kiswahili pia kinakuwa taabu na kiingereza pia. Sijui kama mmeshawahi kutafiti hilo.
 
Nakubaliana na wewe, ila isiwe ni shughuli ya wewe, Kuhani au mimi, nadhani iwe shughuli ya kila mmoja wetu. Kuna makosa ya bahati mbaya yanaeleweka.
 
...asa itabidi hapa pia tupitie kwa pamoja kila thread na post na kurekebisha kiswahili.

"Kiswahili."

Unajua mtu akiandika kiswahili kikawa kimekosewa na ikawa inarudia rudia hata kiingereza...

Tumia "na akawa anarudia rudia," ( yani yeye mwandishi anarudia). Au, tumia "na kikawa kinarudiwa rudiwa," (yani Kiswahili kibovu kinarudiwa). Au, tumia "na yakawa yanarudiwa rudiwa (yani maandishi mabovu yanarudiwa).

Unaposema "ikawa," nini ikawa ?
vyema na hata lugha ya mama yake itakuwa inampa shida kwani ni mtumwa wa lugha.

"lugha Mama yake"

Mtu hajui lugha ya mama vizuri,

"lugha Mama"

na hivyo kiswahili kinampa shida

"Kiswahili"

kwa kuwa language skills inakosekana kutoka kuzaliwa na malezi,

"toka kuzaliwa"

na finally kiswahili pia kinakuwa taabu na kiingereza pia.

Tumia kiunganishi "pia" mara moja kwenye sentensi.

"Kiswahili na Kiingereza, pia, zinakuwa taabu. Au, sema "Kiswahili, pia, kinakuwa taabu. Na hata Kiingereza."

Sijui kama mmeshawahi kutafiti hilo.

Hiyo peke yake ndio sentensi fasaha katika tundiko lako lote. Kuna kijana mmoja, msanii kutoka Kenya, huwa akimaliza kufoka beti zake anauliza "niendelee ama nisiendelee ?"
 
kwa mfano mimi kama mimi mwenyewe binafsi uwaga nafikili akuna hanayejua kua hanakosea adi aambiwe kua hanakosea au hajifunze kujuwa makosa.
Sio uwaga ni huwaga
hapo hakuna haja ya kuweka "ha"
adi ni hadi
hajifunze ni ajifunze
....
......
Watanzania tunajisifu kuwa kuongea "kiswahili" fasaha na kinachoeleweka lakini kumbe sio.Mfano wakenya wako juu sana katika lugha ya kiswahili,kwa mwaka Kenya inatoa wahitimu wa kiswahili wengi kuliko Tanzania.
Wakenya wengi wamejazana kwenye vyuo vya elimu ya juu Marekani wakifundisha kiswahili.

Nini kifanyike?
 
Yo Yo,

Mama hakukosea kwa kutojua, bali amejiborongesha makusudi ili kusisitiza anachotaka kukionyesha. Katika tundiko lake la awali alishaanisha baadhi ya makosa hayo hayo.
 
Sio uwaga ni huwaga
hapo hakuna haja ya kuweka "ha"
adi ni hadi
hajifunze ni ajifunze
....
......
Watanzania tunajisifu kuwa kuongea "kiswahili" fasaha na kinachoeleweka lakini kumbe sio.Mfano wakenya wako juu sana katika lugha ya kiswahili,kwa mwaka Kenya inatoa wahitimu wa kiswahili wengi kuliko Tanzania.
Wakenya wengi wamejazana kwenye vyuo vya elimu ya juu Marekani wakifundisha kiswahili.

Nini kifanyike?

Hayo uliyoyaainisha sio makosa pekee kwenye hiyo sentensi. Kama hujaona makosa mengine basi inaelekea kuwa sio waandishi pekee ndio wanaokosea, hata wasomaji pia. Hatari kubwa!

Kuhusu nini kifanyike Mshiiri ametoa suggestion moja inayotekelezeka hapa JF.

Kwa ujumla, BAKITA haina kazi! Ivunjwe. Vipi kuhusu TUKI?
 
Back
Top Bottom