Makosa Makubwa 3 ya Diamond ni haya

Makosa Makubwa 3 ya Diamond ni haya

profkobayashi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
224
Reaction score
71
DIAMOND ANA MAKOSA 3 MAKUBWA ALIYOTUTENDEA WATANZANIA:

1.Kosa la kwanza ni KUWA NA BIDII KWENYE MUZIKI WAKE...Hili ni kosa kubwa sana kwa Watanzania..Hakupaswa kuwa na bidii hivi..Angekuwa tu wa KAWAIDA kama wenzake waliopita ili AFULIE awaachie na wengine waje kwenye chati arudi Tandale kuuza Wali..

2.Kosa la 2 ni KUJITAMBUA YEYE NI NANI..Kwanini ajitambue wakati wenzie wenye majina walishindwa??Kwani yeye nani awe tofauti??Hii ni DHARAU KUBWA sana kwa Watanzania na Wanamuziki wenzie na inaonyesha ana KIBURI..Diamond kujua yeye ni Mwanamuziki mahiri na kutumia VALUE yake aliyoipata kwa mbinde kuiletea sifa Tanzania nje ya Mipaka ni KOSA KUBWA!

3.Kosa lake la 3 ni KUUHESHIMU MNO MUZIKI UNAOMPA HELA...Kwanini asiwe kama wakina Mr nanihii tu,kwani wao hawakuhit kama yeye?Mbona waliishi kawaida tu na kuuchukulia muziki poa hadi walipofulia na leo hata wakiingia Masai Club nobody cares..Kwani kufulia kitu gani?Diamond hakupaswa kuuheshimu Muziki kama kazi..Angefanya bora liende tu aimbe imbe yaishe..Sasa kujifanya Anatoa Collabo mara Davido mara Mafikizolo mara Trey Songs na K'Cee na Yemi Alade AMETUMWA NA NANI??Huku ni kutafuta sifa tu alipaswa awe mdogo milele awaachie na wenzie.. Kwa makosa haya ma3 WATANZANIA wameamua kumuadhibu..Diamond Anaringa...Ana dharau sana..Anaupenda sana Muziki uliompa JINA..HESHIMA..PESA..na ametafutiwa REPLACEMENT kwa sababu tu ANAHESHIMU MUZIKI KAMA KAZI na sio JUST SINGING FOR FAME...

Watanzania tumeamua kuadhibu MTU ANAYEHESHIMU KAZI YAKE iliyomtoa from Zero to Hero na tutamshusha kwa lazima taji apewe mwingine..Watanzania tunataka Diamond awe another Mr Nice ili tupate kitu cha KUCOMPARE...Shida yetu kuu wala sio dharau ila ni KWANINI DAI HASHUKI???? Hardwork Pays! Respect Pays! Knowing Your Value Pays! Kama alimpandisha MUNGU...Hakuna wa kumtoa pale... Nasibu..wakomeshe..Toa ule wimbo na MAFIKIZOLO wiki ijayo tuone kama watazomea Spika za redio zao... Nalala zangu MDOGO MDOGO...


Source ni:bikira wa kisukuma na repost by jestina geroge

http://instagram.com/officialjestinageorgeblog?modal=true

 
Kiukweli ulichokiandika ndicho ninachokiona.........mimi si mpenzi sana wa bongo fleva lakini muziki anaofanya diamond naukubali na kuuheshimu sana mimi binafsi sioni makosa ya diamond mpaka achukiwe kiasi hiko na hata huyo wanaempambanisha nae sijaonna muziki wake kiiivo wa kumtisha domo angalau hata angekuwa belle 9 au ben paul kidogo'''''''just my view tu.
 
sipendi kuchangia hizi mada ila wakati mwingine inaudhi...unasema mtu anaheshimu mziki huku haeshimu mashabiki na wanamziki wenzake...kama unawapambe ambao wanatukana mashabiki unataka watu wakushabikie tu...unawapambe wanadharau watu wenye kipato kidogo eti wanatumia techno, mara dharau hii mara ile alafu watu wamshangilie tu...achene kumdanganya kama ninyi ndo mnamzunguka mumshauri vizuri
 
umesema ukwli mtupu na hii nuanzia hata ngazi ya familia/kaya/ukoo
 
sipendi kuchangia hzi mada ila wakati mwingine inaudhi...unasema mtu anaheshimu mziki huku haeshimu mashabiki na wanamziki wenzake...kama unawapambe ambao wanatukana mwashabiki unataka watu wakushabikie tu...unawata watu maskini ndo maana wanatumia techno, mara dharau hii mara ile alafu watu wamshangilie tu...achene kumdanganya kama ninyi ndo mnamzunguka..
. Alizomewa maisha club wakasema oooh watu walipangwa,fiesta napo ooohh watu walipangwa diamond na management yake hawauthamini wala kuheshimu mziki wangekuwa wanajielewa yasingetokea ya kule UK!mwambieni huyo domo kubwa anapolifungua aliunganishe na kichwa chake ila ndo hivyo tena kichwani penyewe hakuna kitu
 
Hii wiki mpaka iishe, magazeti yataandikwa mengi humu jf.Mleta mada umesahau sababu ya 4 kuwa akiharibu anatafuta visababu na visingio visivyokuwa na tija.
 
Hii wiki mpaka iishe, magazeti yataandikwa mengi humu jf.Mleta mada umesahau sababu ya 4 kuwa akiharibu anatafuta visababu na visingio visivyokuwa na tija.

Na anaeongelewa ni domo tu watu na nyota zaooo aiseeeee
Na hapo mseme anapenda skendo ney wa mitego alivaa sare za jeshi lakin haongelewii anaongelewa Domo wacha banaaa
 
Jamani kwan diamond kakfanywa nini.??
Si kazomewa tu mara1 kwan ndo kashuka kimuziki.??
 
kosa la nne kufundisha watu kuwa ili uwe mwanamuziki lazima uwe mzinzi,yule mi namuona mziznzi zaidi ya mwanamuziki mara wema ,mara penny,mara jokate
 
kosa la nne kufundisha watu kuwa ili uwe mwanamuziki lazima uwe mzinzi,yule mi namuona mziznzi zaidi ya mwanamuziki mara wema ,mara penny,mara jokate

Ni kweli nimemshuhudia mara kadhaa kwenye TV akitamba bila kujutia kutembea kingono na mabinti kadhaa. Hivi hafahamu kuwa hawa mabinti anaowatangaza ni mabinti wa watu?hajui kuwa ni dada za watu? Wengine ni wapenzi wa watu? Anashangaa anapata wapi maadui? Unatangaza kutembea na binti yangu au dada yangu kwenye TV then utegemee nikupigie makofi?..jingine ni ile tabia ya kujivuna kuwa ana hela nyingi na kwenye akaunti yake haijawahi kupungua mil 100! ..tabia ya majivuno kwenye jamii ya watu masikini kama hii yeye anaiona iko sawa?..kwa nini ujivune kiasi hiki?..maadui amewatengeneza mwenyewe.mimi mwenyewe nilikua napenda sana juhudi zake kwenye mziki lkn nilipoona majivuno yake kwenye TV nimemshusha sana. Ila kuna jambo moja hata maadui zake wanatakiwa kukubali. Kijana anajuhudi sana kwenye kazi yake
 
Back
Top Bottom