Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Imeelezwa kuwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mdude Nyagali Mdude anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Songwe anatuhumiwa kutenda makosa matatu (3) ikiwemo kujeruhi, kutoa lugha ya matusi na kuvuruga ratiba ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2024
Hayo yameelezwa na Wakili wake Boniface Mwabukusi kupitia chapisho aliloweka kwenye mtandao wake binafsi wa kijamii wa X Novemba 24.2024 ambapo ameeleza kuwa yeye binafsi akiwa ameambatana na Mbunge wa zamani wa Mbozi (CHADEMA) Paschal Haonga na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Abdulkareem kwa pamoja wamefika kwenye kwenye kituo cha Polisi Itumba, Ileje anachoshikiliwa Mdude na kusimamia mahojiano yake
Kupata nyuzi za kimkoa Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Amesema licha ya kwamba Jeshi la Polisi limeanza kumuhoji lakini Mdude yeye amegoma kutoa maelezo ya ziada kituoni hapo badala yake ametaka afikishwe Mahakamani ili akatolee huko maelezo hayo, jambo ambalo Wakili Mwabukusi amesema ni haki yake ya kisheria.
Kupitia chapisho hilo, Wakili Mwabukusi ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) ameendelea kufafanua kuwa makosa anayoshtakiwanayo mteja wake yanadhaminika hivyo waliomba apatiwe dhamana hiyo lakini hata hivyo jambo hilo liligonga mwamba kutokana na kile walichoelezwa kuwa maafisa wengine wa Polisi wanataka kumuhoji kutokana na makosa mengine anayodaiwa kuyatenda mkoani Mbeya
Kutokana na hilo, Wakili Mwabukusi ameahidi kurudi kituoni hapo leo, Jumatatu Novemba 25.2024 ili kuendelea kumsimamia mteja wake na kwamba dhamira ni kuona haki za kisheria na Kikatiba za Mdude Nyagali zinapatikana.