Innocent Ngaoh
Member
- Jul 13, 2021
- 19
- 35
Emmanuel Olumide mwandishi wa vitabu kutoka Nigeria aliandika kitabu cha “50 common money mistakes” kitabu ambacho ameelezea makosa hamsini (50) ambayo watu wengi hufanya kwa kujua au kutojua na kupelekea kupoteza fedha zao, inawezekena kabisa unapata fedha lakini hujui wapi fedha zako zimekwenda kwa sababu kuna makosa unafanya na kuwa sababu ya wewe kupoteza fedha zako…
….kupitia makala hii utapata kujua makosa kadhaa ambayo wajasiriamali, wafanyabishara, wawekezaji na watu wa kawaida wanafanya na kupelekea kupoteza fedha zao.
Yafuatayo ni makosa saba (07) ambayo hupekea kupoteza fedha;
1. Kupuuzia kuongeza elimu ya fedha,
watu wengi hawapo tayari kutumia muda wao kuongeza elimu ya fedha badala yake wanatumia muda mwingi kutafuta fedha lakini kwa bahati mbaya wanapoteza fedha zao kwa sababu hawana msingi mzuri wa kutunza na kuzalisha fedha na kuwa na elimu ya fedha ambayo mashuleni na vyuo vikuu haifundishwi elimu hii muhimu ya kufanikiwa kifedha kwa maana hiyo kuipata ni juhudi yako kwa kusoma vitabu, kuhudhuria semina , kufuatilia mafunzo ya fedha, kusoma makala n.k mfano kwanini kupata tsh 1,000,000 ni kazi sana lakini kuipoteza tsh 1,000,000 ni rahisi sana kwa sababu ya kukataa na kupuuzia kuongeza elimu ya fedha. Tafuta kitabu cha “Richest man from babylon” cha George Carson, “Rich dad poor dad” cha Robert Kiyosaki, msingi wa elimu ya fedha cha Amani Makirita, Kanuni 20 za fedha cha Victor Mwambene, “Money Formula” cha Joel Nanauka n.k. utajishukuru kwa kusoma vitabu hivi na kupiga hatua kwenye eneo la uchumi.
2. Kupuuzia utamaduni wa kuweka akiba,
Kila fedha ambayo unaipata usitumie yote asilimia 10% au zaidi weka akiba, watu wengi wanajua faida ya kuweka akiba lakini wanapuuzia na matokeo yake wanabaki kuwa maskini na hili ni kosa kubwa ambalo unafanya kwa kutokuweka akiba na kupelekea kutumia fedha yote kwenye matumizi yako kama vile kununua chakula, nguo, kulipa gharama ya usafiri n.k kwa kigezo cha kusema fedha wanayopata ni ndogo kwahiyo hawawezi kukuweka akiba lakini fahamu kwamba kuweka akiba ni tabia na fedha haijawahi kutosha ndiyo maana hata matajiri bado wanatafuta fedha ingali wana fedha nyingi kwa maana hiyo anza kuweka akiba asilimia 10% au zaidi itakusaidia kujenga kesho yako iliyo bora zaidi weka akiba kidogo kidogo “Akiba ni mtaji wa uwekezaji”.
3. Kuwekeza fedha zako sehemu ambayo huifahamu vema,
Watu wengi wanaweza fedha zao kwa sababu ya hisia au kusikia ukiwekeza kwenye kitu fulani tu utapata faida lakini matokeo yake unapoteza fedha kwa sababu ya kuwekeza eneo ambalo hulijui wala hujafanya utafiti wa kutosha juu ya uwekezaji wako pia mwandishi anasema ni hekima kubwa kufanya utafiti kabla ya kuwekeza fedha zako kwa maana hiyo njia pekee ya kuepuka kosa hili ni kuwa na muongozo sahihi juu ya uwekezaji ambayo itakusaidia usingie kwenye mtego wa kupoteza fedha zako mfano ”Kuna kipindi watu walipoteza fedha zao kwenye kilimo cha matikiti kwa kusikia matikiti yanalipa bila ya kufanya utafiti wa juu ya kilimo cha matikiti, wakalima na matokeo wakapata hasara kubwa.”
4. Kutokuweka bajeti ya fedha zako,
Kosa kubwa ambao watu wengi hufanya ni kutokuwa na utaratibu wa kuweka bajeti ya fedha zako kabla ya kuanza kufanya matumizi na matokeo yake wanatumia fedha zako sehemu ambazo sio muhimu na lazima na wengine wanakula kabisa mitaji ya biashara zao kwa maana hiyo ili usipoteze fedha zako ni kuweka bajeti ambayo itakupa rekodi ya matumizi ya fedha zako pia bajeti itakusaidia wewe kujua matumizi yako ya fedha zako; anza kuweka bajeti na iwe sehemu ya maisha yako ya kila siku.
5. Kuingia kwenye mtego wa madeni,
Kukopa sio vibaya lakini kukopa ni mwanzo wa kuingia kwenye mtego wa kuwa mtu wa madeni na kupelekea kila fedha ambayo unapata ulipe madeni na ndiyo mwanzo wa kuwa mtumwa wa madeni na njia pekee ya wewe kutokuwa mtumwa madeni ni kutochukua mkopo kwa ajili ya matumizi binafsi, badala yake chukua mkopo ajili ya kuwekeza kwenye eneo ambalo huna uhakika wa kurudisha fedha uliyowekeza ili ulipe deni na kubaki na faida kwa maana hiyo kuwa makini sana mikopo ambayo unachuka kumbuka unaweza kuishi vizuri bila madeni.
6. Kutoheshimu kanuni ya dhahabu (Disobey Golden rule),
Kanuni ya dhahabu inasema “wafanyie watu vizuri kama ambavyo unapenda na wewe ufanyiwe” kama unataka kufanya vizuri kwenye biashara yako, kampuni yako, ujasirimali wako, huduma yako hakikisha unakuwa mtu mzuri kwa watu wengine pasipo kuwachukulia poa, kuwadharau, kuwasema vibaya, na majivuno kwa sababu watu wengi kupoteza fedha baada ya kuanza kuwabeza watu wengine na ndiyo unakuwa mwanzo wa kupoteza fedha na sio kupata fedha kwahiyo heshimu watu; kisha kuwa mtu mzuri kwenye kazi yako na kwa watu wengine na fedha zako zipo kwa watu ndio maana msemo maarufu wa Kiswahili unasema “Pata fedha tupate kujua tabia yako.”
7. Kuwa na chanzo kimoja cha kipato,
Mwanzo wa kuelekea kwenye mafanikio ya kifedha ni kuwa na vyanzo vingi vya mapato kwa sababu hata matatizo yanapotokea hayawezi kuathiri vyanzo vyote vya mapato kwa wakati mmoja kwa maana hiyo ukiwa na chanzo kimoja cha mapato basi jitahidi sana kupambana upate chanzo cha pili cha kipato na kendelea lakini kosa kubwa ambalo watu wengi hufanya ni kuridhika na chanzo kimoja cha mapato hata kama wanaweza kuongeza chanzo chengine ndiyo maana mambo yanapoenda tofauti kupoteza fedha na kubaki maskini; jitahidi kuwa na vyanzo walau vitatu vya mapato na kuendelea.
Kumbuka kufanikiwa kifedha haitazamwi unaingiza kiasi gani bali ni uwezo wa kutunza na kuzalisha fedha baada ya kuingiza fedha kwenye kitu unachofanya.
HATUA YA KUCHUKUA; oredhesha makosa ambayo yanapelekea wewe upoteze fedha zako kisha hatua gani uchukue ili uwe imara kifedha kwa maana ya kiuchumi.
~ Imeandikwa na Innocent Ngaoh. I

Upvote
8