Makosa ya baadhi ya Askari wa Usalama Barabarani (trafiki) wasio na weledi yaliyowahi kusababisha maafa

Makosa ya baadhi ya Askari wa Usalama Barabarani (trafiki) wasio na weledi yaliyowahi kusababisha maafa

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
12,283
Reaction score
23,443
Ukosefu wa weledi katika kutekeleza majukumu ya kusimamia usalama barabarani yaliyowahi kuleta majanga:

Mamlaka za usalama barabarani zipo chini ya kikosi cha usalama barabarani (Trafiki)

Pamoja na kupewa mamlaka hayo makubwa kusimamia vyombo vyote, yapo makosa ya wazi kabisa ambayo hufanywa na baadhi ya Trafiki wasio na weledi na HAKUNA JITIHADA ZA WAZI ZINAZOCHUKULIWA Kuondoa ukanjanja katika sekta hii nyeti.

Haya ni matukio machache yaliyowahi kutokea miaka mitatu iliyopita
1. Siku moja Trafiki walimpiga na fimbo kijana wa boda boda aliyekuwa kabeba abiria akiwa kwenye mwendo kiasi kilichopelekea abiria w kudondoka na kufariki na trafiki waliokuwa maeneo hayo walipotea walikimbia hawakuonekana baada ya kuona abiria kafariki.

2. Tukio jingine ni hapo mbezi luis njia ya mageti kwenda goba, Kuna trafiki walikuwa wanajificha na kujitokeza ghafla barabarani kwa kushitukiza kusimamisha magari; miaka minne iliyopita, Walisimamisha ghafla gari ikasababisha magari zaidi ya 6 yaliyokuwa nyuma kugongana baada ya gari lililosimamishwa ghafla kusimama! Na wale askari waliokuwa eneo hilo walikimbia baada kuona ajali imetokea! Hadi leo hawajawahi kurudi kusimama eneo hilo kwenye mtelemko.

3. Tukio jingine bagamoyo kuna trafiki alivunja taa ya gari akimshurutisha kusimama ghafla, Mashuhuda wanadai kumbe yule mtu alipofika mbali alipogundua gari lake lilipasuliwa taa, alikodi boda wakatoa namba , wakarudi na rungu wakampiga rungu la mgongo trafiki aliyekuwa akiendelea na majukumu! Wakisema amewapasulia taa na kutokomea.

Yapo matukio mengi sana ambayo chanzo cha hatari huchangiwa na ukosefu wa weledi kwa baadhi ya trafiki tunaoamini wanasimamia sheria.

Tunaomba hayo mamlaka yao yaangaliwe namna ya kuzibiti ubabe, matusi, katika utekelezaji wa majukumu yao
 
Nchi hii huwezi kutofautisha kati ya msomi na ambaye hajasoma
Waliosoma na kuaminiwa wakapewa mamlaka ya kusimamia sheria ndiyo namba moja wa kuvunja sheria na kwenda kinyume na maadili na miiko yao ya kazi, kuna muda unatamani tuwe kama Somalia🇸🇴 muuza mirungi ana AK47 mnunuzi naye ana AK47 sasa hapa ni kuheshimiana
 
Wanaonewa sana watu wa dala dala.na mwenyewe matrafiki wana maisha mazuri,kila mmja ana nyumba na magari ya kutembelea
 
Wanaonewa sana watu wa dala dala.na mwenyewe matrafiki wana maisha mazuri,kila mmja ana nyumba na magari ya kutembelea
Wanavumilia tu ili biashara iende
 
Nchi hii huwezi kutofautisha kati ya msomi na ambaye hajasoma
Waliosoma na kuaminiwa wakapewa mamlaka ya kusimamia sheria ndiyo namba moja wa kuvunja sheria na kwenda kinyume na maadili na miiko yao ya kazi, kuna muda unatamani tuwe kama Somalia🇸🇴 muuza mirungi ana AK47 mnunuzi naye ana AK47 sasa hapa ni kuheshimiana
Na wajinga ndiyo wanasimamia sehem mhimu
 
Back
Top Bottom