Japhari Shabani (RIP)
R I P
- Jan 16, 2007
- 721
- 178
Kama kuna kosa amabalo imelitenda CCM kwa mwaka huu wa uchaguzi,ni kumchagua JK kugombeea nafasi ya Uraisi kupitia CCM.Inaeleweka hii ni kutokana na mazoea kwamba mtu anaepitishwa na CCM inabidi agombee vipindi viwili.Sasa nashindwa kuielewa kama ndio hivyo walivyoamua kwanini wawe wanapoteza pesa katika mchakato wa kumpata mgombea urais katika chama chao?Kama ccm wangelikua makini wangetumia kipindi cha miaka mitano kumpima mgombea wao ni kwa kiasi gani ametimiza sera ya chama.Kama alivurunda nibora wakamuweka mgombea mwingine.Naimani katika CCM kunawatu wengi makini amabao wanaweza kufanya vizuri zaidi ya huyu msanii Kikwete.Lakini kutokana na mazoea mchakato wa kumpata mgombea kutoka ccm inabaki kama formality,vurunda usivurunde miaka kumi ni yako.Hii inaondoa changamoto kwa mgombea na kutokua na dhamana kwa aliyoyatenda katika kipindi chake.TENDA UTAKAVYO FANYA UTAKAVYO MIAKA KUMI NI YAKO.Kwa bahati mbaya CCM wameshindwa kusoma mishale ya wakati.Watatumia pesa nyingi,watatumia mbinu chafu,wataiba kura,watawanunua wapiga kura n.k ukweli unabaki palepale KIKWETE NI MZIGO USIOBEBEKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA.