Makosa ya kiserikali ya 2019 yanayoendelezwa 2021. Nini kifanyike?

Makosa ya kiserikali ya 2019 yanayoendelezwa 2021. Nini kifanyike?

Mbona sioni ulichoandika?! Utumbo mtupu, ushawishi wa Rwanda kusini umekopi na ku- paste kauli na mawazo ya Bernard Membe aliyotoa hivi karibuni basi!
Kweli wewe ni kanjanja wa kutupwa!
 
Unaliona hilo bango? Linanikumbusha Tarehe 5 December 2019 niliandika makala nikionya matendo ya serikali ambayo yalikuwa yanakinzana na dunia ya ushindani inavyokwenda, Nilionya baada ya kujiridhisha kwamba Tanzania inaenda kushoto huku Watani zetu wa Jadi Kenya na dunia kwa ujumla wanakwenda kulia kwa mwendo wa kasi.

Nilisema wazi kwamba, Wakati dola nzima iko Ufipa usiku na mchana kuhakikisha Chadema inapata mwenyekiti mdhaifu ambae kwao itakuwa rahisi kuiua Chadema, Majasusi wa Nairobi Kenya na Asmara Eritrea wako duniani wakipambana kutafuta uungwaji mkono katika kuhakikisha nchi zao moja wapo inaingia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Nakumbuka ilikuwa ni kupindi cha Uchaguzi ndani ya Chadema na tulikuwa tunapambana kuhakikisha mamluki wa ccm hawapenyi na kushika uongozi wa chama, Mamluki hao walikuwa wakiongozwa na Cecil Mwambe, Dr Mashinji na vibaraka wengine wadogowadogo. Tuliwadhibiti kwa kura wakakimbia kwa aibu.

Katika ishu ya Kenya na Eritrea kuliwa cheni ya kijasusi ikipigwa na Idara ya Ujasusi ya Djibouti hadi Mkenya akashangaa na roho yake, Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa UNSC liliipata endorsement Kenya kwa upande Afrika kuwa candidate wa Afrika. Ila Djibout ikakataa kujitoa na kumwachia Kenya kiti hicho, Eritrea ikalazimisha nayo kupeleka jina UN kugombea.

Hivyo uchaguzi ikalazimika kuwa wa Kura badala ya Acclamation ambayo ingeipa Kenya moja kwa moja kuwa mwakilishi wa Afrika katika Baraza hilo la Usalama. So kampeni zikaanza kila mmoja akitumia uwezo wake kijasusi kutafuta kura, Ilikuwa vita kali sana na ikitumia skills za kidiplomatic efforts and resources. Kenya iliunda kikosi kazi chini ya mwanadiplomasia jasusi mbobevu Bi Amina Mohamed kuendesha lobbing ambayo hadi leo kwenye korido za kijasusi wanaiita ni ya karne.

The key point angalia ajenda zao hapo kwenye moja ya bango hilo lililotumika katika kampeni, Katika kampeni hii waliyoiita "What Kenya will do on their term", ukiangalia utaona point namba moja ilikuwa ni Bridging Bridging ambapo Bango hilo liliwekwa makao makuu ya UN.

Kipindi hicho niliueleza utawala ule dharimu kwamba vita vya kijasusi vile sio simple kama vile kuua upinzani nchini Tanzania, wamejipanga hao jamaa juu ya Kenya katika uso wa dunia. Slowly wana-take role ya Tanzania Kimataifa. Katika Matokeo ya battle hii Kenya walishinda kwa kishindo.

Huku Tanzania vurugu za Serikali kuua upinzani hazikufanikiwa na nchi ilizidi kuangamia kwa mauaji ya wapinzani na wanaharakati, utekaji na kubambikia kesi na zaidi kwakutengwa na dunia. Nchi ikajikuta imejitenga yenyewe automatic, huku tukiimbishwa nyimbo za kijinga kwamba Tanzania ni dona kantiri, na ujingaujinga mwingine mwingi.

Ilipofika 2021, Si kwamba Tanzania iliendelea kuwa mtani tena wa Kenya, bali ilipoteza ushawishi wote katika eneo la maziwa makuu, Kufumba na kufumbua hata kinchi kidogo kama Rwanda ambacho sisi ndio tulimweka rais wao na kwa miaka mingi tangu Uhuru tulikuwa tukikiongoza kinchi hiki kutokea Kijitonyama na Upanga, sasa kimeipoka Tanzania ile nafasi ya ushawishi kijeshi na kiujasusi kusini mwa jangwa la Sahara. Leo Rwanda iko Msumbiji ikirejesha utulivu. Msumbiji ambako ni eneo muhimu la kimbinu kwa Tanzania liko mikononi mwa Kagame huku Sisi Serikali leo iko busy kuendeleza uzandiki uleule wa tangu 2019 kwa kumbambikia Mbowe kesi ya Ugaidi kwa lengo lilelile la kijinga la kuua upinzani na ccm itawale daima.

Kupanga ni kuchagua lakini uchaguzi wa serikali ya Tanzania ni angamizo kwa nchi. Ili taifa lipone linahitaji katiba mpya tu.

Kwa undani zaidi soma kitabu cha Ujasusi. 0715865544

Na Yericko Nyerere
View attachment 2034603
Hata IGP Siro alisikika akienda kujifunza Taarifa za ujasusi wa Usalama huko Rwanda.

Vikosi vyote viko bize kutengeneza mashahidi wa uongo dhidi ya mbowe
 
Yericko Nyerere, sina hakika kama unasoma comments. CCM haishuhuliki na maendeleo kabisa kabisa kabisa. Inatumia rasilimali za nchi kuhakikisha watu hawaendelei mbele, just emagine drama ya korosho, kuharibu soko letu Kenya, gharama wanazolipwa polisi kumtesa Mbowe, Mdude etc, suala la gasi ya Mtwara. Tozo etc
Huo ndio ukweli woote. Wanajitahidi sana kukusanya kodi ili ccm iweze kusurvive na so vinginevyo.
 
Ukiwa Tanzania unaweza kuhisi Kenya au Rwanda kuna maisha mazuri(kwa mwananchi mmoja mmoja) ukilinganisha na Tanzania.
ILA ukienda kwenye hizo nchi utagundua hisia zako hazikuwa sahihi bora hata Tanzania.
Hii inatokana na baadhi yetu kutaka tujione sisi hatufanyi vema au tunakosea kuliko wengine.

NAKUPINGA mtoa mada kwenye suala la MBOWE.
Kwenye siasa duniani kote haya mambo hayakosekani na hayazuiliki,Huwezi hitimisha hapa eti MBOWE kabambikiwa wakati bado kesi ipo mahakamani. AU mimi siwezi kumnanga eti Gaidi kisa imesemwa na fulani

NAMALIZIA kwa kusema siyo lazima kila kifanywacho na wenzetu kina tija kwetu,
Mbowe sio Gaidi Na msingi wa mashtaka yake kila mtu anajua. Ni Katiba Mpya
 
Back
Top Bottom