PreGE2025 Makosa ya kiufundi waliyofanya wanaojaribu kuhujumu "No Reforms No Election"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hata mimi naiona pia katika mitandao ya kijamii. Watu wamechefukwa vibaya mno!

Hongera kwa uchambuzi mzuri

Raia wanahitaji mabadiliko, wamechoka maigizo, maovu yanayofanywa na viongozi batili

Ni kweli, mafuriko hayazuiwi kwa mikono
na kila jambo na nyakati au wakati wake
 
Hata Barack Obama alikuwa mvuta bangi na bado akawa USA President. Msijipe umaarufu msiokuwa nao. NCCR ya Agustino Lyatonga Mrema ilikuwa maarufu kuliko CHADEMA ya sasa
Usiwafananishe Chadema ys Lissu na dalali mchumia tumbo Mrema
 
CCM inayo nafasi ya kuplay smart tena kama ilivyofanya mwaka 1992 ilipokubali vyama vingi kwa kuwa pragmatic na kukubali mabadiliko huku ikiwa na nafasi ya kuminitor, kuwa incontrol ya mabadiliko hayo. La sivyo wasiojulikana watapoteza wengi kabla hawajagundua kuwa kupoteza watu hakusaidii kuzima azma ya wananchi kutaka mabadiliko ya msingi ya namna gani nchi yao iendeshwe.
Kwa haraka haraka nilivyo kusoma, ninakubaliana na uliyoandika kwa ufundi mkubwa (kama kawaida yako), huko juu.

Hili la mwisho nina mashaka makubwa nalo. No, CCM hawana mbinu nyingine mbali ya kutumia mabavu kubaki madarakani, kama inavyoonekana wakijiandaa kwa hilo; kwa kung'ang'ana na kukataa aina yoyote ya "Marekebisho", ili uchaguzi mkuu uonekane kuwa HURU na HAKI.
Hili wanaliogopa sana, na watafanya kila njia lisitokee.

Kama wangekuwa na wigo wa kutengeneza mbinu nyingine, njia nzuri si kukataa moja kwa moja "Marekebisho".
Wangekubali kuingia kwenye "MAZUNGUMZO", huko ndiko pekee kuliko baki na mbinu; ingawaje haya huko sioni CHADEMA wakiwapa nafasi tena ya kufanya ulaghai na hadaa.

CCM hawana mbinu nyingine, mbali ya kutegemea mabavu kuwabakizamadarakani.
 
Mkuu, watu wanaongozwa na viongozi. Kusema chama si cha viongozi ni sawa na kusema timu si ya wachezaji ni ya mashabiki hata wakiondoka viongozi wote ni sawa, ni katikati ya msimu, wakitoka wachezaji nani atacheza? Muda wa kusajili wenye uzoefu upo? Hii toka toka lazima idhibitiwe, chama ni watu.
Ninakubaliana na dhana nzima; isipokuwa huko ',kudhibiti.

Mchezaji (mwanachama) ana hiari ya kuchezea timu yoyote. Ni utashi wake unaoendeshwa na mambo mbalimbali.
Utamdhibiti mchezaji ambaye kaamua kuachana na timu yako vipi, iwapo kisha ahidiwa maslahi mazuri zaidi na timu nyingine?
Kama timu hasimu wameamua kuwavuruga wachezaji wako kwa njia mbalimbali, siyo swala la viongozi wa timu inayohujumiwa kuwalazimisha wachezaji walio amua kwa sababu zao wenyewe, ambazo huna uwezo wa kuzizuia
Utamzuia mchezaji asiondoke wakati unajuwa kubaki kwake ndani ya timu ni kuiangamiza timu nzima?

Watu wasitishike na hawa watu kuondoka ndani ya CHADEMA; hili ni kundi lililodhamiria kukiua chama, siyo kukijenga.

Ukiniambia kuwa hiyo timu sasa haina uwezo wa kuingiza wachezaji wengine, tena walio bora ya hao wanaoondoka, hapo nitatishika sana na uhai wa CHADEMA.'
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kwa haraka haraka nilivyo kusoma, ninakubaliana na uliyoandika kwa ufundi mkubwa (kama kawaida yako), huko juu.

Hili la mwisho nina mashaka makubwa nalo. No, CCM hawana mbinu nyingine mbali ya kutumia mabavu kubaki madarakani, kama inavyoonekana wakijiandaa kwa hilo; kwa kung'ang'ana na kukataa aina yoyote ya "Marekebisho", ili uchaguzi mkuu uonekane kuwa HURU na HAKI.
Hili wanaliogopa sana, na watafanya kila njia lisitokee.

Kama wangekuwa na wigo wa kutengeneza mbinu nyingine, njia nzuri si kukataa moja kwa moja "Marekebisho".
Wangekubali kuingia kwenye "MAZUNGUMZO", huko ndiko pekee kuliko baki na mbinu; ingawaje haya huko sioni CHADEMA wakiwapa nafasi tena ya kufanya ulaghai na hadaa.

CCM hawana mbinu nyingine, mbali ya kutegemea mabavu kuwabakizamadarakani.

Njia ya mabavu itagota kwa sababu, wakishamwaga damu sana inaweza kuzaa visasi vinavyoweza kuanza kuwagharimu, na pia watachafuka mno kama tawala za iddi Amini, hii inaweza kuanza kufanya international community iwamulike na wajikute wako katika hali ngumu za kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria. Eventually watajikuta wao wenyewe wanaomba mazungumzo kuomba way out!
 
Lazima hadhi ya box la kura irudi kama si hivyo basi huo sio uchaguzi ni maigizo ya ccm na matawi yake.
 
Njia ya mabavu itagota kwa sababu, wakishamwaga damu sana inaweza kuzaa visasi vinavyoweza kuanza kuwagharimu, na pia watachafuka mno kama tawala za iddi Amini, hii inaweza kuanza kufanya international community iwamulike na wajikute wako katika hali ngumu za kuweza kuchukuliwa hatua za kisheria. Eventually watajikuta wao wenyewe wanaomba mazungumzo kuomba way out!
Hayo yote unayosema hapo wanayajuwa vizuri; ila sasa ni kama hayawahusu tena. Wamepofuka.

Sasa mgoja nikudokeze tu; wao wanasema hawatakuwa wa kwanza kufanya hayo katika ukanda wetu huu. Kenya kila uchaguzi una machafuko, na watu wengi wanakufa; lakini Kenya inadunda tu!

Umemtaja Idi Amin; lakini ukamsahau Museveni anavyo wadhibiti wapinzani wake kila uchaguzi. Wewe unadhani hawa CCM hawaoni 'model' kama hizo?
Ni wapi uchaguzi umefanyika ukwa ni wa haki hapa Afrika,... Afrika Kusini; Botswana. YES. Wapi kwingine.
Ukimtazama Mnangangwa pale; juzi tu hapo Msumbiji. Kote huko CCM na serikali yake imekwenda kutazama mifano ya kuiga.

Matarajio yao (CCM) makubwa ni kuwa, baada ya vurugu hizo za muda mfupi, mambo yatarudi na kuwa kama kawaida. Huku ni kucheza kamali. Hapa hatujawahi kuwa na hali ya namna hiyo, kama Kenya na kwingineko. Itakuwa ni kukosa weledi kudhani kwamba hali ilivyokuwa huko kwingine, na hapa itakuwa hivyo hivyo.

Na hasa ukichukulia odhoofu wa viongozi waliopo, wanaotafuta kubaki madarakani kwa nguvu.
 
Ninakubaliana na dhana nzima; isipokuwa huko ',kudhibiti.

Mchezaji (mwanachama) ana hiari ya kuchezea timu yoyote. Ni utashi wake unaoendeshwa na mambo mbalimbali.
Utamdhibiti mchezaji ambaye kaamua kuachana na timu yako vipi, iwapo kisha ahidiwa maslahi mazuri zaidi na timu nyingine?
Kama timu hasimu wameamua kuwavuruga wachezaji wako kwa njia mbalimbali, siyo swala la viongozi wa timu inayohujumiwa kuwalazimisha wachezaji walio amua kwa sababu zao wenyewe, ambazo huna uwezo wa kuzizuia
Utamzuia mchezaji asiondoke wakati unajuwa kubaki kwake ndani ya timu ni kuiangamiza timu nzima?

Watu wasitishike na hawa watu kuondoka ndani ya CHADEMA; hili ni kundi lililodhamiria kukiua chama, siyo kukijenga.

Ukiniambia kuwa hiyo timu sasa haina uwezo wa kuingiza wachezaji wengine, tena walio bora ya hao wanaoondoka, hapo nitatishika sana na uhai wa CHADEMA.'
Sahihi boss.
 
Hayo yote unayosema hapo wanayajuwa vizuri; ila sasa ni kama hayawahusu tena. Wamepofuka.

Sasa mgoja nikudokeze tu; wao wanasema hawatakuwa wa kwanza kufanya hayo katika ukanda wetu huu. Kenya kila uchaguzi una machafuko, na watu wengi wanakufa; lakini Kenya inadunda tu!

Umemtaja Idi Amin; lakini ukamsahau Museveni anavyo wadhibiti wapinzani wake kila uchaguzi. Wewe unadhani hawa CCM hawaoni 'model' kama hizo?
Ni wapi uchaguzi umefanyika ukwa ni wa haki hapa Afrika,... Afrika Kusini; Botswana. YES. Wapi kwingine.
Ukimtazama Mnangangwa pale; juzi tu hapo Msumbiji. Kote huko CCM na serikali yake imekwenda kutazama mifano ya kuiga.

Matarajio yao (CCM) makubwa ni kuwa, baada ya vurugu hizo za muda mfupi, mambo yatarudi na kuwa kama kawaida. Huku ni kucheza kamali. Hapa hatujawahi kuwa na hali ya namna hiyo, kama Kenya na kwingineko. Itakuwa ni kukosa weledi kudhani kwamba hali ilivyokuwa huko kwingine, na hapa itakuwa hivyo hivyo.

Na hasa ukichukulia odhoofu wa viongozi waliopo, wanaotafuta kubaki madarakani kwa nguvu.

`1. Hapa nchini tuna taasisi yenye nguvu ya Kanisa, hii ni taasisi inayoweza kuwaongoza waTZ kuigomea serikali na serikali ikaufyata. Kanisa linaweza kwenda kufanya misa Ikulu na mamilioni ya watu ya kuombea "Haki" na serikali ikaonja joto la Jiwe.
2. Strategically serikali inaweza kuzima "battle" chache za kutaka mabadiliko, ila haiwezi kuzima "war" nzima na endelevu ya kutaka mabadiliko. Hapa sizungumzii mapambano ya silaha, bali nazungumzia struggle za kijamii na kisiasa.
3. Kuna ishu za misaada kutoka nje hasa EU, wakikatiwa hii line watajitafuta sana.
4. Huko Kenya angalau kura ya mtu inaheshimika, Zimbabwe waliwekwa kikaangoni mpaka Mugabe akapinduliwa, Msumbiji raia walikuwa kama bongo kutokujali ishu za nchi yao, ila baadae walikinukisha kwelikweli. Wabongo siyo specie tofauti
 
Hiyo namba moja (1), iondoe kwenye mategemeo. Haiwezi na haiwezekani

Namba tatu, hiyo CCM watafumba macho, wakitegemea kukishatulia na wamebaki madarakani ulaghai na hadaa nyingi zitatumika; kwanza ndani kwa ndani, kama viini macho vya "maridhiano" na watakaokuwa tayari kucheza sarakasi ili kuonyesha mshikamano uliopo nchini. Wakimaliza hiyo, wanapeleka bakuli likajazwe.

Hata siku moja sijapata kuamini mabadiliko yanayotokea nje ya nchi. Wanachoweza kufanya hao, kama EU, ni kutoa tu msaada kwetu sisi wenyewe tulete mabadiliko yetu wenyewe.
Waweke vikwazo wakati tukiwakamua hao watesi wetu, na wasaidie nyenzo muhimu tutakazohitaji wenyewe kujikwamua

Hiyo namba nne (4), mfano wa Kenya bado ni mbovu; kwa sababu vurugu zile kila uchaguzi zimeegemea kwenye ukabila na mtu maalum Raila Odinga; ambaye kwa kiasi kikubwa wanaouliwa ni wajaluo. Inaposikitisha zaidi ni wakati Raila anapoingizwa tena kwenye serikali aliyoipinga kuwa imeingia visivyo kihalali (Nusu Mkate). Fuatilia matukio yote toka Moi hadi Mwai Kibaki, Uhuru Kenyatta na sasa Ruto. Kenya ni mfano mbaya sana kuuweka hapa. Nadiriki kusema, njia hiyo ilikuwa imeandaliwa safari hii kwa Samia kumnasa Mbowe; lakini sote sasa tunajuwa jinsi ilivyo sambaratishwa.
 
Hizi ni propaganda tu. Huwezi Kuta Mtu mwenye akili timamu na reputation kwenye jamii akiongea huu upupu.

Unadhani una uchungu mkubwa kwa Fr Kitime kuliko Kanisa la Katoliki? Unadhani wako kimya? na kama hawazungumzi zungumzi ni kwanini?

Unadhani unaielewa CHADEMA kuliko hao G55?

Hukimsikia Lissu aki SEAL a PROCLAMATION kuwa uchaguzi CHADEMA mwaka huu waushau?

Au hukuona hata kwenda kusaini hati ya kanuni za uchaguzi mwaka huu Chama kilikataa?
Utakuwa na kilema cha ubongo
 
Mabadiliko yoyote ya kikatiba na sheria za uchaguzi yakifanyika,ccm bye bye
 
Back
Top Bottom