Makosa ya miaka mitano ya Hayati Magufuli yanasahihishwa sasa. Hongera CHADEMA kwa kuongoza hili kwa ufundi mkubwa

Kisa JPM hakuhudhuria kikao cha CDM?. Hata JPM angeenda ila hakuwa mtu wa asali.

Mbona Mbowe alihudhuria mikutano ya JPM ikiwemo ya wafanyakazi na alipewa nafasi ya kusema?

Mambo ya kulambishana Asali na kusahau shida za wananchi ndio unayasifu?

Sasa Kilo ya Unga na Mchele havishikiki. Siku hizi kula maharage ni anasa. Tembele kwenda mbele.
 
Na ndio tatizo lilipo yani bado tunaangali makosa yaliyopita tukija kushtuka haya makosa ya sasa yashakomaa. Samia hawezi kuwa Rais kwa kuondoa makosa tu yaliyopita.
"Sijaona makubwa zaidi", haya yaliyopo yanafanyiwa kazi kwa sababu nia ipo kati ya pande mbili, tofauti na wakati ule, kutekana na kuuana na ukitaka make chini mzungumze muuaji hana huo muda.
 
Wanasiasa wakimalizana tofauti zao wananchi wanafaidika nini, kwamba kila mmoja atapatiwa mbolea ya ruzuku? Au unadhani kila mwananchi anahangaikia nafasi za kisiasa?
Wanasiasa wakipatana hapo patakuwepo na nia ya kufanya kazi kwa pamoja na kusikilizana, hivyo itakuwa rahisi kwa upande mmoja kusikiliza hoja za upande wa pili na kuzifanyia kazi kwa maslahi ya taifa, nchi na wananchi wataneemeka kwa hilo.
 
Huu wimbo wa asali mnapenda kuuimba sana, lakini mkiambiwa mtoe ushahidi wa hilo hakuna yeyote kati yenu anayeweza kufanya hivyo.

Kwenu mtu kupewa haki zake mnakereka, mnaumia, hamkumbuki maumivu waliyopitia wakati wa huyo JPM mnaemsifu, leo wanapewa kile walichonyan'ganywa mnawaita wanalamba asali.

Mlitaka waendelee kuonewa miaka yao yote, kuteswa miaka yao yote, ndio mridhike muwaone wapambanaji, hiyo ilikuwa ni mentallity ya kikatili iliyopandikizwa vichwani mwa watanzania na kiongozi mshamba.

Wakati wenu ndio huu, utoeni huo ujinga vichwani mwenu, kwasababu naamini hamkuwa nao kabla ya Magufuli, msiendelee kuishi kwenye fikra za kikoloni, hii nchi ni yetu sote, na wote tuna haki sawa.
 
Tunawazoom tu mkilambishana asali.
 
Endelea kuimba tu ...

Hilo pambio mnalipenda sana!.
Kwani hatuoni watu wanalipiwa hadi nauri za safari?

Eti wewe unakaa nchi gani?

Mama atakuja kupata kashifa kubwa.
 
Haya ni malidhiano ya wanasiasa wala hayana matokeo yoyote chanya kwa wananchi!!, Wanasiasa wa Tz ni wabinafsi na wenye roho mbaya Sana!.
 
Kwa hiyo mmemuarika Samia ili kumnanga mtemi wetu wa SUKUMA GANG Mzee JPM?
 
Hii move ni nzuri lakini upande wa Chadema wafanye kwa tahadhari sana. Alichofanyiwa Maalim Seif Zanzibar na alichofanya JK kwenye katiba mpya ni funzo
Hapo katiba mpya na tume huru zinatafutwa.

Zikipatikana utaona habari tofauti na sasa.

Na istoshe wapo kwenye maridhiano. Huwezi attack adui yako wakati mnapatanishwa.
 
Hapo katiba mpya na tume huru zinatafutwa.

Zikipatikana utaona habari tofauti na sasa.

Na istoshe wapo kwenye maridhiano. Huwezi attack adui yako wakati mnapatanishwa.
Ili Katiba nzuri ipatikane lazima Chadema wawe na wawakilishi Bungeni, hivyo Uchaguzi wa 2025 Chadema hawana budi kushiriki....

Kuna ile hali ya Toa hiki Upate hiki
 
Kwenu mtu kupewa haki zake mnakereka, mnaumia, hamkumbuki maumivu waliyopitia wakati wa huyo JPM mnaemsifu, leo wanapewa kile walichonyan'ganywa mnawaita wanalamba asali.
2024 na 2025 mtapata haki zenu zengine kutoka kwa CCM na vyombo vya dola.
 
Ili Katiba nzuri ipatikane lazima Chadema wawe na wawakilishi Bungeni, hivyo Uchaguzi wa 2025 Chadema hawana budi kushiriki....

Kuna ile hali ya Toa hiki Upate hiki
Kwa hiyo tume huru tayari imepatikana ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…