Makosa ya Musiba, hayalingani na tamaa ya Membe!

inawezekana wewe hujui mahakama inafanye kazi,aliyeathirika na kashfa hudai fidia kwa kiwango anachokuona kimamfaa na anaposhinda kesi,mahakama humuita ili kujadiliana nae hicho kiwango na inakuwa ni ka kesi hivi,sasa baada ya hapo mahakama ndio inyopanga kiasi cha fidia,hivyo membe hahusiki na huo uamuzi wa mahakama kuhusu fidia
 
Kwa nini uliamua kumtukana Membe? Unakuja hapa ili tumuonee huruma?
Pambana na hali yako, Musiba wewe!
 
Hivi wewe ni kisamv cha kopo au ni cha kutwangwa kwenye kinu?Stupengo!
 
Sasa kwa maoni yako ulifikiri ili isiwe tamaa, je:-

1. Membe angedai fidia ya shs ngapi labda?

2. Au je Musiba angemtukana na kumdhalilisha Membe kiasi gani (idadi au siku ngapi) ili kiendane na hiyo shs 8.8 billion (bila gharama za execution)?

3. Ili upewe tuzo na Mahakama (kama mdai/Membe) ni lazima uthibitishe uhalali na ukweli wa madai yako. Na mdaiwa/Musiba) ajitetee na kanushe kuonyesha mapungufu ya madai ya Membe....nk nk
Mimi na wewe hatujaona ushahidi wao au mwenendo wa shauri zima - na pengine hatuna ujuzi wa kuamua kwa usahihi uzito wa kesi yao, hata tukipewa huo ushahidi.

Vyovyote iwavyo, ni vema kutambua kuna AINA mbali mbali za adhabu.
Kuna adhabu hutolewa ili iwe SOMO au FUNDISHO KWA WENGINE.
Ndugu, usiombe uwe fundisho/somo kwenye maisha!
 
Declare to interest kuwa unamtetea bwana Musiba. Membe hana shida na hiyo hela bali kumdiscipline Musiba. Ulitakiwa umshauri hapo kabla wakati akibwabwaja matusi yasiyo na breki.
 
 
Mkuu elimu haipo shuleni tu, hata huku duniani kuna elimu pia. Hili ni somo zuri sana na hasa ukizingatia ni elimu kwa vitendo. Watu wengi watajifunza kupitia darasa hili, la "elimu nje ya darasani"
 
kwa hiyo unataka kusema majaji waliotoa uamuzi hawana akili kuliko huyo unayesema hana akili? Hivi we uko mirembe tayari au bado uko uraiani. Ule ni uamuzi wa mahakama kuu, majaji walikuwa wana uwezo wa kupunguza kiwango alichodai Membe ila walioona ni sahihi kulingana na udhalilishaji alomfanyia na kulinga na ya hadhi ya Membe.

Na ujue Membe siyo Kalagabaho km wewe.
 
Wasiompenda JPM wanashangilia sana kwa sababu .Musiba anakomolewa kupitia sheria na Mahakama inaonekana imetemda haki. Lakini mahakama hiyo hiyo ikiamua dhidi ya wapinzani inaonekana imepokea maagizo na haiko huru.

Waziri mmoja wa zamani wakati anakata rufaa kupinga ushindi wa kesi ya mgombea binafsi katika uchaguzi alisema: Mahakama ni mtu kama mimi na wewe"
Lipumba baada ya uchagu,zi mkuu aliwahi kusema kuwa mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar alihongwa pesa na akanunua nyumba; yule mwenyekiti alienda mahakamani Lipumba alihukumiwa amlipe milioni 30; sasa ukilinganisha kiwango alichohukumiwa Musiba kulipa ni wazi japo hukumu inaheshimiwa lakini kuna hisia kukomolewa. Hivi Musiba hakukata rufaa au rufaa pia alishindwa? Sikuwahi kufuatilia hiyo kesi.

Tujiulize maswali mowili: Hivi JPM angekuwepo hiyo hukumu ingetoka jinsi ilivyo? Ingetekelezeka.?
 
Nenda ukamtetee MAHAKAMANI.
 
Kaiambie mahakama sisi hayatuhusu.
 
Unajua thamani ya utu wa mtu?
Au ndiyo nyie huwa mnasema ni afadhali mngezaliwa mbwa Ulaya kuliko kuzaliwa binaadam bongo?
Thamani ya utu sio hiyo billion tisa boss wangu,ndio maana binadamu akiuwawa na tembo waathirika wanalipwa million moja,ila mwanakijiji akiuwa tembo ni million 25 na jela juu
 
Thamani ya utu sio hiyo billion tisa boss wangu,ndio maana binadamu akiuwawa na tembo waathirika wanalipwa million moja,ila mwanakijiji akiuwa tembo ni million 25 na jela juu
Kila mmoja na ajipime utu wake una thamani ya hali na kiasi gani.
Kama wako una thamani ya kilo ya sukari ni sawa, nikubishie mimi ni nani?
 
Musiba alipotakiwa kuomba msamaha mbona aligoma?
Msamaha ni bei gani?
Linalomkuta ni haki yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…