SoC01 Makosa ya Serikali kufuatia mapambano dhidi ya UVIKO-19 na chanjo yake

SoC01 Makosa ya Serikali kufuatia mapambano dhidi ya UVIKO-19 na chanjo yake

Stories of Change - 2021 Competition

The ricco king

New Member
Joined
Aug 1, 2021
Posts
2
Reaction score
0
Utangulizi
Dunia nzima imekumbwa na janga zito la ugonjwa wa UVIKO-19 lililoanza mwaka 2019 huko nchini China bara la Asia na kutokana na uzito wa janga hilo kila nchi imejitahidi kufanya kila namna ili kunusuru wananchi wake na madhara yatokanayo na ugonjwa huu hatari, zipo nchi zilizozuia wananchi wake kutoka majumbani, kukusanyika kwa namna yoyote na hata kuwalzimisha chanjo na madawa mbalimbali.

Kwa sasa hivi jambo kubwa linaloongelewa sana duniani kuhusiana na ugonjwa huu ni chanjo hizi za UVIKO-19 ambazo zipo nyingi na nchi zilizoendelea baadhi zimetengeneza chanjo zao na nchi zinazoendelea kama sisi Tanzania tunapokea chanjo kutoka mataifa mbalimbali na mpaka sasa kuna aina zaidi ya tatu zinazoruhusiwa kuchomwa hapa nchini.

Lakini kwa inavoonekana serikali yetu imekurupuka sana kwenye hili swala la chanjo na tumeingia kichwa kichwa mno, zaweza kuwa na msaada au la lakini njia waliyoitumia kuhamasisha wananchi sio sawa kabisa na si ajabu kwa hizi nadharia zinazovuma mtaani kuhusu chanjo kuendelea kuvuma na mpaka kuja kufanikiwa kuelewesha watu kuchanja kama matarajio yao itachukua muda sana.

Kosa limeanzia wapi?
Hapa nchini kwetu janga hili limeanza kusumbua mwaka 2020 mwezi wa tatu ambap Hayati rais Magufuli alihitahidi kupambana nalo kwa njia kadhaa ikiwemo kumshirikisha Mwenyezi Mungu kupitia dini mbalimbali pia kutumia njia za mitishamba na jadi kama kujifukiza na kutumia dawa zilizotengenezwa hapa nchini kama vile Kovido.

Kwa njia zake alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza hofu kwa wananchi juu ya gonjwa hilo na kupelekea kulishinda na Tanzania ikawa kati ya nchi chache ambazo shughuli za kiuchumi ziliendelea bila kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na hakukuwa na makatazo ya kutotoka majumbani, ilifika hatua mpaka hospitali kama muhimbili na mloganzila ziliweka vifaa vya kujifukiza na tulihubiriwa umuhimu wa kufanya hivyo na ilisaidia kiukweli.

Sasa tuko kwenye awamu ya sita ya mama Samia ambapo shida imeanza maana bila ya kutarajia na katika mshangao mkubwa mambo yamebadilika kwa kasi tofauti na tulivyotarajia hasa ukizingatia mama alifanya kazi bega kwa bega na Hayati, na maswali yanayogonga vichwa vya watanzania wengi ni kwanini hatuhamasishwi tena njia za jadi kama kujifukiza? Je ile dawa ya kovido imeishia wapi? Vifaa vya kujifukiza muhimbili na mloganzila vimeishia wapi? Je Mungu tuliyemuomba mwaka jana akatusaidia hana nguvu tena mwaka huu? Je zile njia zote ukijumuisha mazoezi na zingine zilizofanya tukaisahau uviko-19 hazifanyi kazi tena?

Maswali haya yamekosa majibu kwa kila anayejiuliza, mbaya zaidi hivi sasa kinachoongelewa sana ni chanjo na ubaya wenyewe sio chanjo kama chanjo ila zimechanganyika na siasa ndani yake, kila mtu amekua mjuaji kupitiliza na wanasiasa kuongelea hili swala kwa kulazimisha au kuhimiza hili swala la chanjo haikua na umuhimu kabisa, sababu ni kwamba chanjo inahusisha afya ya mtu sasa kwa nini madaktari na maafisa wa afya wasiwe mstari wa mbele kuliongelea hili swala badala ya wanasiasa? Kwanini tunasikia maswala ya chanjo kutoka kwa wanasiasa na viongozi wa dini?

Je, wana elimu gani juu ya maswala ya afya na chanjo? Je kama wao walielimishwa kwa namna moja au nyingine na wakaelewa kwanini serikali isiwekeze kuwaelimisha na wananchi undani wa swala hili kabla ya kuambiwa tukachanje? Mtanzania wa vijijini anapataje taarifa kuhusu hizi chanjo? Na sasa hivi kuna chanjo aina kama tano ambazo zinatofautiana na inategemea hali yako ya kiafya au mapendekezo yako ili kuamua ipi uchome je watanzania wanalijua hili au wanaijua moja ya johnson johnson?

Nini kifanyike?
Kwa hali ya kawaida huwezi ukaniambia nikachome sindano fulani kisa tu wewe umechoma ama fulani amechoma tena hadharani akipigwa picha hata kama unayochoma ni chanjo kweli tunayoijua bado elimu kubwa inabidi itolewe na pia zile njia zilizotusaidia mwaka jana kipindi cha hayati ziendelezwe ili wananchi watoke kwenye sintofahamu ya lipi ni lipi, ile dawa iliyotengenezwa Tanzania ya kovido iendelezwe na yenyewe maana ni rahisi kuamini dawa kutoka nchini kwetu kuliko madawa tusiyoyajua kutoka magharibi yaliyojaa nadharia zenye ukakasi.

Pia, nadhani wanasiasa wasiongelee jambo ambalo hawana taaluma nalo wawaachie madaktari na watoa huduma za afya ndio wahusika wakuu katika jambo kama hili

Mwisho kama chanjo ni hiari kama inavyosemwa basi hakuna haja ya kumbeza mtu asiyetaka kuchanjwa vivyohivyo hakuna haja pia ya kusema au kutangaza hadharani kama utachanja au hutachanja kwa kua ni jambo binafsi na halituhusu na hata ukichanja haimaanishi mimi nitachanja kisa wewe umesema umechanja mpaka nijue faida zake na kwanini nichanje, tunauguaga magonjwa mengi na kupata dawa kadhaa na wala hatutangazi, hili ni gonjwa kama magonjwa mengine hofu ndiyo inasumbua wengi, tusitafute umaarufu kupitia janga hili.

Ni hayo tu.
(Picha kwa msaada wa mtandao)

images (35).jpg
 
Upvote 0
Back
Top Bottom