Makosa ya Ufaransa kuruhusu Prussia kuipiga Austria probably ndio kubwa katika Historia ya Wafaransa na Waingereza

Makosa ya Ufaransa kuruhusu Prussia kuipiga Austria probably ndio kubwa katika Historia ya Wafaransa na Waingereza

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
2,869
Reaction score
3,187
Tangu kukamilika kwa Thirty Years War (1618 - 1648) na kusainiwa kwa Westphalia Treaty mwaka 1648, Nchi za Uingereza na Ufaransa zilitawala Siasa na Uchumi wa Ulaya. Uingereza kupitia Industrial Revolution iliyoanza 1780s ili-dominate uchumi wa Dunia huku Ufaransa akidominate siasa za Ulaya. Kulikuwepo States nyingine kubwa za Austria, Spain na Russia na Prussia zilizokuwa zikipigana na mataifa madogo madogo ya Ulaya na kujitanua.

Hata hivyo, check and balance iliyobuniwa na Mataifa ya Ulaya baada ya 1648, ilisababisha kutokuwepo kwa mbabe mmoja pekee Ulaya, mpaka alipojitokeza Mtawala wa Ufaransa aitwaye Napoleon Bonaparte in 1890s - 1810s, aliyevamia Mataifa karibia yote ya Ulaya na kushindwa tu Uingereza iliyokuwa na Superior Navy kuliko ya Ufaransa. Hata hivyo, ukoloni huo wa Ufaransa kwa mataifa ya Ulaya, ulisababisha Nationalism kubwa sana barani Ulaya hasa kwa mataifa huru ya kijerumani yakiongozwa na Austria na Prussia.

Baada ya Napoleon kuanguka 1812, Prussia na Austria, ambazo ni za kijerumani zilipata nguvu ya kutaka kujaza Vacuum iliyoachwa na Utawala wa Ufaransa katika Central Europe. Kipindi hicho, kulikuwepo appetite ya mapinduzi ya wananchi katika Ulaya nzima lakini tawala za kifalme hazikutaka Serikali za kidemokrasia.

Baada ya pressure za kidemokrasia kuzidi, Mfalme wa Prussia, Wilhelm I, alimteua mwaka 1861 Otto von Bismarck kuwa Chancellor na huyu jamaa alipanga mbinu za kupigana na Austria ili aweze kucontrol mataifa madogo ya Kijerumani. Hivyo, ilitokea bahati nzuri mwaka 1864 Denmark ilivamia Jimbo la Schleswig-Holstein linalokaliwa na Wajerumani wengi kuliko Wadanish. Bismarck aliikaribisha Austria kuipiga Denmark na kuweza kugawana Jimbo hilo mwaka 1864.

Hata hivyo, Prussia ambayo ilikuwa imeshaanza ku-undergo Industrial Revolution (tangu 1840s) ilitaka kuipiga Austria ili itawale Majimbo yote ya Wajerumani ambapo hadi kipindi hicho, Wajerumani ndio Taifa (Nation) pekee barani Ulaya pamoja na Waitalia ambalo hawakuwa unified chini ya Taifa na Dola (Sovereign State) moja.

Hata hivyo, Bismarck alijua kuwa, kukua kwake kumeshaanza kuogopesha wengine na kwamba Mataifa mengine ya Ulaya hasa Uingereza na Ufaransa yasingeruhusu Prussia kuipiga Austria (ambayo hadi kipindi hicho ilichukuliwa ni Taifa kubwa kuliko Prussia). Hivyo Bismarck aliingia mikataba ya kirafiki na Ufaransa na Italia ya kutoingiliana in case kuna mgogoro na nchi nyingine, so mwaka 1866, Prussia ilipigana na Austria na kuipiga kwa aibu ndani ya muda mfupi na kufanikiwa kuanzisha German Confederation.

Kipigo cha Austria kiliwashangaza Wazungu coz hawakutarajia Prussia kuishinda. Ilileta hofu na lawama huko Ufaransa na Uingereza jinsi walivyoruhusu kuanzishwa kwa Dola jingine kubwa katika Central Europe. Prussia iliunganisha majimbo yote ya kijerumani isipokuwa Majimbo ya Kusini ya Bavaria (Bayern) na Baden Wurttemberg yaliyoko karibu na Austria. Hivyo, Bismarck aliona kuwa, ni Vita na Ufaransa pekee ambayo ingesababisha Majimbo hayo kujiunga na Ujerumani mpya.

Opportunity hiyo ilijitokeza mwaka 1870 wakati kulipozuka mzozo wa kiplomasia kati ya Ufaransa na Prussia juu ya nani alipaswa kutawala Hispania baada ya Mfalme kufariki na kubaki wazi. Mzozo huo ulisababisha Prussia kumfukuza Balozi wa Ufaransa Mjini Berlin baada ya Balozi huyo kumlazimisha Mfalme wa Prussia aahidi kutojihusisha na masuala ya Utawala wa Hispania, suala ambalo Mfalme aliona amedharauliwa.

Kukataa kwa Prussia juu ya wito wa Ufaransa, kuliwaudhi sana Wafaransa na kuhisi Prussia imewasaliti, so Ufaransa ilitangaza vita dhidi ya Prussia. Kumbuka hadi kipindi hicho, Ufaransa lilikuwa Taifa la pile Ulaya na la tatu duniani nyuma ya Uingereza na Marekani pekee katika matatifa yenye nguvu.

But katika hali ambayo ilishangaza Dunia nzima, Jeshi la Ujerumani (hata majimbo ya Kusini yaliungana na Prussia) liliipiga vibaya Ufaransa na kuteka Mji Mkuu wa Paris mwaka 1871. Vita hiyo imeacha mpaka Leo doa Kuu kwa Ufaransa na hata Waingereza wanajilaumu pia jinsi walivyoruhusu Wajerumani kuungana na kuwa Taifa lenye nguvu za kijeshi kuliko yote barani Ulaya na lenye uchumi wa pili nyuma ya Uingereza.

IMG_5179.GIF

Much more to come.....
Nawasilisha wazee.
 
IMG_5181.JPG

Ujerumani ya leo, ni zao hasa la Vita ya Prussia vs Austria. Isingekuwa Ufaransa kuamua kutoingilia, walahi labda tungekuwa na Dola tofauti kabisa ya Ujerumani tuijuayo.

Ujio wa Ujerumani ndio uliosababisha kuvunjika kwa Mfumo wa checks and balance uliokuwepo tangu 1648 na kupelekea kuundwa kwa Alliances barani Ulaya kwani Ujerumani iliharibu kabisa balance ya zamani kwa kuchukua nafasi ya pili Ulaya kama Taifa la pili kwa nguvu za kiuchumi huku likiwa ya kwanza kiteknolojia na kijeshi.

Maumivu ya kupigwa kwa Wafaransa na Wajerumani hadi kutekwa kwa Mji Mkuu, ndiyo yaliyosababisha Uadui mkubwa kati ya mataifa hayo, so nchi hizo zililazimika kuimarisha majeshi yao na kutafuta marafiki. Usingekuwa uadui huu, kamwe WW I isingetokea kwani Serbian Crisis ulikuwa hauna umuhimu mkubwa. Na kama WW I isingetokea basi WW II nayo isingetokea.
 
Wafaransa waliathirika sana kuona Ujerumani imeundwa kupitia mgongo wao mwaka 1871. Waingereza walianza kuionea wivu Ujerumani hasa baada ya 1890 kutokana na Viwanda vyake kuwa na ufanisi mkubwa kuliko vya kwao vya tangu 1780s. Of course, Wajerumani waliongoza Dunia nzima katika teknolojia ya chemical lakini ilikuwa hasa mikakati ya a Ujerumani kuanza shipbuilding kwa ajili ya Jeshi lake (Navy) ndicho kilichowaogopesha kwani Ujerumani ilitaka kushindana na Uingereza baharini kwa kuwa bahari ilikuwa imetawaliwa almost solely na Waingereza.
Wajerumani walitaka kulinda makoloni yao mapya ya German East Africa (Tanganyika-Ruanda-Urundi), Cameroon, Togo na German South West Africa (Namibia) yaliyokuwa Afrika, pamoja na Papua New Guinea na baadhi ya Visiwa vya Pacific.
Licha ya makoloni ya Ujerumani, kutofikia hata asilimia 10% ya ubora (achana na wingi) wa makoloni ya Waingereza, ama kutozifikia Ufaransa, bado ilizitoa out vibaya katika bidhaa bora. Ndipo kipindi hicho cha mwishoni mwa 1890s hadi kizazi chetu, jina chuma cha Mjerumani limekuwa synonymous na ubora wa hali ya juu wa bidhaa zao. So Waingereza wakawachukia sana.
Hali hiyo ya chuki ya Waingereza na Wafaransa kwa bidhaa za Wajerumani kuanzia 1890 - 1980, ni sawa na chuki ya Wamarekani kwa Wachina katika kizazi cha sasa.
 
Kipi kiliwapa upper hand wajerumani katika biashara ya viwanda dhidi ya Uingereza?
 
Kipi kiliwapa upper hand wajerumani katika biashara ya viwanda dhidi ya Uingereza?
Walikuja na teknolojia mpya tofauti na ya Uingereza - Taifa la kwanza kuendelea kiviwanda tangu 1780s ambayo kufikia 1900 walijikuta wanaachwa nyuma kiteknolojia na Wakuja Ujerumani na Marekani. Aidha, Ujerumani ndo wali-introduce mfumo wa makampuni kuungana (merger) na kuwa makubwa na kuzalisha Conglomerate na Cartels, ambayo yalikuwa more powerful kuliko Individuals walikuwa Lancashire (Manchester, Blackburn, Blackpool, Bilton, Sheffield, Bradford na Leeds). Vilevile, utayari wa Ujerumani kuwekeza kiwango kikubwa cha fedha katika urafiti kwa kufadhili Vyuo, ilisababisha mwamko mkubwa na kuibua wanasayansi wengi kibao (akiwemo Albert Einstein). Ujerumani kati ya mwaka 1900 - 1940, Ndiyo iliyoongoza Dunia nzima kwa kutoa washindi wengi wa Nobel katika Sayansi hasa Chemistry na Physics.
Ni bahati mbaya tu kwa Wajerumani kuwa, sisi Waafrika wa sasa tumezaliwa kipindi magari ya Mjapani yakidominate masoko ya Nchi zetu masikini but in 1950 -1970, the talk of the town ilikuwa Chapa ya VW (Volkswagen - soma Folksvageni) Beetle. Haya ni magari yaliyoanzishwa na Hitler mwaka 1939 huko Wolfsburg.
Leo masoko ya Mjerumani kwa chapa zake za VW, BMW (soma BEMAVE), Daimler (soma Dimla) Benz & Mercedes Benz, Mann, Audi, yamespecialize kwenye magari ya kifahari Ndiyo maana wazungu wanauziana tu huko wao kwa wao kutokana na gharama.
 
Walikuja na teknolojia mpya tofauti na ya Uingereza - Taifa la kwanza kuendelea kiviwanda tangu 1780s ambayo kufikia 1900 walijikuta wanaachwa nyuma kiteknolojia na Wakuja Ujerumani na Marekani. Aidha, Ujerumani ndo wali-introduce mfumo wa makampuni kuungana (merger) na kuwa makubwa na kuzalisha Conglomerate na Cartels, ambayo yalikuwa more powerful kuliko Individuals walikuwa Lancashire (Manchester, Blackburn, Blackpool, Bilton, Sheffield, Bradford na Leeds). Vilevile, utayari wa Ujerumani kuwekeza kiwango kikubwa cha fedha katika urafiti kwa kufadhili Vyuo, ilisababisha mwamko mkubwa na kuibua wanasayansi wengi kibao (akiwemo Isaac Newton). Ujerumani kati ya mwaka 1900 - 1940, Ndiyo iliyoongoza Dunia nzima kwa kutoa washindi wengi wa Nobel katika Sayansi hasa Chemistry na Physics.
Ni bahati mbaya tu kwa Wajerumani kuwa, sisi Waafrika wa sasa tumezaliwa kipindi magari ya Mjapani yakidominate masoko ya Nchi zetu masikini but in 1950 -1970, the talk of the town ilikuwa Chapa ya VW (Volkswagen - soma Folksvageni) Beetle. Haya ni magari yaliyoanzishwa na Hitler mwaka 1939 huko Wolfsburg.
Leo masoko ya Mjerumani kwa chapa zake za VW, BMW (soma BEMAVE), Daimler (soma Dimla) Benz & Mercedes Benz, Mann, Audi, yamespecialize kwenye magari ya kifahari Ndiyo maana wazungu wanauziana tu huko wao kwa wao kutokana na gharama.

Kwa nini sasa mpaka Vita ya Kwanza ya Dunia inaanza UK bado alikuwa anamzidi kwa mbali kwa Utajiri huyo mjerumani?
 
Kipi kiliwapa upper hand wajerumani katika biashara ya viwanda dhidi ya Uingereza?
Kanuni ya uchumi na teknolojia huwa iko wazi kuwa, as time passes, jamii iliyoendelea inafikia level of maturity ambapo haiwezi kukua zaidi ya hapo hadi mwingine anapokuja kutake-over.
Hii ndiyo iliyozipata Civilisations:
  • Mesopotamia - 3,500 BC
  • Babylonia - 2,000 BC
  • Hittite - 1,500 BC
  • Hellenic (Greek) - 1,000 BC
  • Roman - 200 BC
  • Iberian (Spanish & Portuguese) - 1400 - 1600
  • British & French 1600 - 1920
  • German 1840 - 1970.
  • Americans 1840 - 2000.
  • Russian 1940 - 1980.
  • Japan 1900 - 2010
  • Chinese 1990 - ?
  • Indian 2000 - ?
  • African ? - ?
 
Kwa nini sasa mpaka Vita ya Kwanza ya Dunia inaanza UK bado alikuwa anamzidi kwa mbali kwa Utajiri huyo mjerumani?
Utajiri wa Muingereza ulitokana na faida kubwa ya makoloni waliyokuwa nayo. Makoloni hayo yalitoa ajira kwa urahisi kwa masikini wote, hivyo huko a Uingereza walibakia tu wenye shughuli zenye vipato vya uhakika. Fikiria kila koloni litoe ajira kwa Waingereza hata 200 pekee. Hao ni viongozi wenye vitega uchumi wakistaafu wanarudi a Uingereza kula maisha. Ndiyo maana Uingereza ilikuwa Nchi ya kwanza kuwa na mature economy ambako watu hawategemei Manucturing Industry bali Services industry. Mabenki, makampuni ya bima na usafirishaji yakawa na nguvu kwenye uchumi wao hadi kufanya London kuwa jiji kubwa duniani by 1950 likiwa na watu zaidi ya milioni 7. Kipindi hicho, ilikuwa ni ajabu sana kwani jiji la pili kwa ukubwa Ulaya wakati huo la Berlin likiwa na milioni 3 pekee.
Kiukweli ni Uingereza hasa iliyofanikiwa kutawala Nchi zote bora - USA, India, Canada, Australia, Nigeria, South Africa, Kenya na Rhodesia. Ndiyo maana hata licha ya ukoloni kuisha, bado Waingereza waliendelea kuzidi Nchi zote za Ulaya katika GDP on per Capita licha ya kupigwa mbali tangu 1950s na Ujerumani katika uzalishaji wa karibia kila category ya bidhaa za viwandani.
Lugha ya kiingereza, imewapa sana ulaji Waingereza na ndicho kitu watajivunia maisha yao yote kwa jinsi Dunia yote inajikuta inalazimishwa bila kupenda kufahamu kiingereza kutokana na mapinduzi ya ICT (Information & Communication Technology). Angalia tu Ligi Kuu ya Barclays, timu ya mwisho kwenye msimamo inapata fedha nyingi za mgawo wa Ligi kuliko karibia timu zote duniani (labda inazidiwa na timu za soka zisizofikia 10) hiyo ni faida ya haki za matangazo ya Ligi.
 
Wajerumani wangeshinda vita ya Kwanza ya Dunia wangeshika namba moja katika utajiri? Kwa nini licha ya kupokonywa makoloni yote Ujerumani sasa anawazidi kifedha nchi zote zilizofaidika na ukoloni?
 
Wajerumani wangeshinda vita ya Kwanza ya Dunia wangeshika namba moja katika utajiri? Kwa nini licha ya kupokonywa makoloni yote Ujerumani sasa anawazidi kifedha nchi zote zilizofaidika na ukoloni?
Swali zuri sana. Kuna watu huwa wanajidanganya na indeed tumeaminishwa kwenye Historia kuwa, Umasikini wetu umetokana na Ukoloni wa Wazungu. Nitakuwa wa mwisho kuikubali hoja ya namna hiyo, achana na kuisikiliza. Ili uelewe Afrika lazima pia uelewe na Ulaya, America na Asia.
Hakuna Nchi yoyote duniani iliyowahi kupata maendeleo kutokana na kuwa na makoloni bali nchi iliyoendelea ndiyo iliyoweza kupata makoloni - full stop.
Pamoja na Uingereza kuwa na makoloni mengi, bado ilianza ku-undergo Agrarian Revolution 1500-1600s) kabla ya Waingereza kuanza kutoka nje ya Nchi yao kutafuta makoloni (spheres of influences). Indeed, ni baada ya Industrial Revolution (Phase I) ya 1770s - 1790s, ndipo Concept ya Muingereza kuwa na himaya (Possessions - mind you haya siyo makoloni) ya kuuza bidhaa zao ilipoongezeka. Na Muingereza hakutaka Makoloni, so akaitawala US, Canada, Australia, New Zealand, India na Pakistan indirectly akipendelea mfumo wa Free Trade (Leissez-Faire) mpaka Wakuja Wajerumani chini ya Bismarck miaka ya 1870s walipoharibu balance of power barani Ulaya, waliwashitua Waingereza kwa kuwa walitaka makoloni kama Waingereza for strategic reasons but mostly for prestigious reasons.
Kuna baadhi wanailaumu Ujerumani kwa umasikini wetu, fuatilia vyema Historia utagundua hawa kuja Afrika kwa pressure ya raw materials kama tulivyoaminishwa. Na indeed hadi Wajerumani wanaondoka mwaka 1917 kwenye Vita, hawakuwahi kupata faida kamwe katika uendeshaji wa Reli ya Kati (Central Line) iliyojengwa kutokana Dar - Kigoma kuanzia mwaka 1905-1914.
 
Wajerumani wangeshinda vita ya Kwanza ya Dunia wangeshika namba moja katika utajiri? Kwa nini licha ya kupokonywa makoloni yote Ujerumani sasa anawazidi kifedha nchi zote zilizofaidika na ukoloni?
Korea Kusini ni eneo la mashamba ya mpunga tu na haina rasilimali za asili but fortunately, wana rasilimali watu ya ubora wa hali ya juu. Hii inamaanisha rasilimali kubwa ni watu (teknolojia) but ukiwa na vilaza hata upewe kila kitu ni kazi bure. Yanayotutokea sisi Waafrika ndio ukweli huo. Kila Nchi dunia nzima anaionea wivu sana Congo DRC kwa rasilimali ilizojaliwa but ina watu vilaza kabisa wasiotambua umuhimu wa amani (surely kuna instigations from outside). Tanzania tuna rasilimali lukuki na sisi tumeshidwa kuzi-harness.
 
Mkuu naona bado hoja iko imepwaya, kama ujerumani hawakunufaika na makoloni(Mfano Tanganyika waliitawala kwa miaka thelathini tu) na wanahistoria wanadai Infrastructure ya Ulaya ilijengwa kutokana na faida ya Ukoloni(Fedha iliyonyonywa) hasa hasa waingereza hii ikimaanisha Waingereza na wakoloni wengineo walitajirishwa sana na Ukoloni, Imekuwaje Wajaerumani kuwapiku wakoloni wote? Ujerumani GDP yao iko Dola Trilioni 3.5 wakati Uingereza GDP iko kwenye dola trilioni 2.5. Kuna nini hapa? Kama ni Elimu nadhani wote tunajua kielimu Waingereza wako juu( AMbapo hapa hoja yako ya High Quality Human Resource ya Germany inakuwa baseless when it comes to United Kingdom)

Heshima kwako!
 
Jaribu kujiuliza ni nini kiliifanya Hispania na Ureno kuitwa Nchi masikini katika EU kama kuwa na makoloni ni hoja? Ilikuwaje Hispania iliyotawala America ya Kusini yote (ukitoa tu Brazil, Guyana, Suriname na French Guiana)? Ilikuwaje Marekani likawa Taifa tajiri kuliko yote hata kabla ya WW I, wakati haikuwa na makoloni?
Mbona Uholanzi na Nordic Countries (Norway, Sweden, Finland na Denmark) zimekuwa tajiri kuliko Ureno iliyoitawala Brazil, Mozambique, Angola na Guinea Bissau?
Ingekuwa makoloni ndio utajiri, basi Nchi tajiri duniani kati mwaka ya 1920 - 1940 zilifaa ziwe hivi:
  1. Uingereza
  2. Ufaransa
  3. Hispania
  4. Ureno
  5. Italia
  6. Uholanzi
Cha ajabu, kwa kipindi hicho, Nchi tajiri zilikuwa ni:
  1. Marekani
  2. Uingereza
  3. Ujerumani
  4. Ufaransa
  5. Japan
  6. Italia
IMG_5212.PNG

Hapo unaona Marekani, Ujerumani na Japan, hawakuwa na makoloni lakini wali-perform.
Hakuna anayekataa kuwa raw materials iliwasaifia Wazungu kuwapunguzia gharama za bidhaa lakini mi nakwambia hadi miaka ya 1900, Ujerumani aliagiza pamba kutokana Marekani na siyo Afrika - think.
Hakuna Nchi duniani iliyoendelea kwa kutegemea makoloni - Muulizeni Mreno amezitawala Guinea, Angola na Mozambique tangu 1464, 1483 na 1505 respectively but ndiye muda wote amekuwa masikini barani Ulaya.
 
View attachment 814740

Then which is a reason behind? Issue ya high Quality Human Resource ni Insignificant Hapa
 
Mkuu naona bado hoja iko imepwaya, kama ujerumani hawakunufaika na makoloni(Mfano Tanganyika waliitawala kwa miaka thelathini tu) na wanahistoria wanadai Infrastructure ya Ulaya ilijengwa kutokana na faida ya Ukoloni(Fedha iliyonyonywa) hasa hasa waingereza hii ikimaanisha Waingereza na wakoloni wengineo walitajirishwa sana na Ukoloni, Imekuwaje Wajaerumani kuwapiku wakoloni wote? Ujerumani GDP yao iko Dola Trilioni 3.5 wakati Uingereza GDP iko kwenye dola trilioni 2.5. Kuna nini hapa? Kama ni Elimu nadhani wote tunajua kielimu Waingereza wako juu( AMbapo hapa hoja yako ya High Quality Human Resource ya Germany inakuwa baseless when it comes to United Kingdom)

Heshima kwako!
Yes, kwenye elimu ya makaratasi Waingereza wamekuwa juu but unapoongelea engineering it has become synonymous with the Germans. Tangu miaka 1870s hadi leo hii, Ujerumani imeiacha Dunia kwa mbali. Ndiyo maana wamekuwa champions wa biashara kwa muda mrefu kutokana na ubora wa bidhaa zake. Uingereza pamoja na kuwa na makoloni bado alipata tabu sana. Na Ndiyo chanzo cha Waingereza kuichukia sana Ujerumani. Hata hivyo, ilikuwa katika WW I na II, ndipo Muingereza alipomchukia sana Ujerumani. I tell you, had it not for the American interference in WW I in 1916, walahi Muingereza alikuwa yuko mikononi mwa Ujerumani. Vilevile, isingekuwa Mjapani kuipiga Pearl Harbour, possibly Wamarekani wasingeingilia WW II ambako Hitler alikuwa keshateka Ulaya nzima isipokuwa Uingereza na Urusi. So, wenye akili wote wanajua kuwa Waingereza walishinda vita kwa msaada wa Marekani.
Mpaka Leo hii, Uingereza akimfunga Mjerumani kwenye michezo anakua emotional sana kuliko Mjerumani kuifunga England. Mfano: Uingereza iliifunga Ujerumani WC 1966 na walifurahi sana but since then, wamepata vipi go vya mfululizo kwenye WC - QF huko Mexico 1970; SF huko Italia 1990 na 2ND Round huko South Africa 2010. Mpaka Leo hii Waingereza wanawaona Wajerumani kama mshindani (rival) wake Mkuu kwenye soka lakini Wajerumani hawajali Rivalry hiyo bali Wajerumani (Deutsch) wanajali Rivalry dhidi ya Uholanzi (Dutch), right?
 
Mkuu naona bado hoja iko imepwaya, kama ujerumani hawakunufaika na makoloni(Mfano Tanganyika waliitawala kwa miaka thelathini tu) na wanahistoria wanadai Infrastructure ya Ulaya ilijengwa kutokana na faida ya Ukoloni(Fedha iliyonyonywa) hasa hasa waingereza hii ikimaanisha Waingereza na wakoloni wengineo walitajirishwa sana na Ukoloni, Imekuwaje Wajaerumani kuwapiku wakoloni wote? Ujerumani GDP yao iko Dola Trilioni 3.5 wakati Uingereza GDP iko kwenye dola trilioni 2.5. Kuna nini hapa? Kama ni Elimu nadhani wote tunajua kielimu Waingereza wako juu( AMbapo hapa hoja yako ya High Quality Human Resource ya Germany inakuwa baseless when it comes to United Kingdom)

Heshima kwako!
Licha ya Ujerumani kubwa ha mbali on GDP, but still Ujerumani na Uingereza hawatofautiani sana kwenye GDP on per Capita. GDP ya Ujerumani imekuwa kubwa zaidi kutokana na kuwa na watu wengi pia (milioni 82 vs milioni 65).
 
Nilirefer situation ya Mjerumani kuwa hana makoloni lakini kumpita Muingereza( During Hitler's Era)
 
Back
Top Bottom