Kwa karibu miaka kadhaa sasa kuna mlolongo wa matukio ambayo yangetokea nchi nyingine yoyote yangetoa nafasi ya pekee kwa vyama vya upinzani. Mlolongo huo kwa Tanzania hata hivyo haujatoa nafasi hiyo kwa upinzani kiasi kwamba kama taifa badala ya kuangalia upinzani kutoa uongozi katika saa na wakati huu bado wananchi wanaangalia CCM pamoja na madudu yake kutoa uongozi kwa taifa.
Hili lawezekana ni kutokana na makosa ya upinzani na vyama vikubwa vya upinzani nchini. Makosa ambayo kimsingi kabisa yamechangia kudhoofisha demokrasia na hivyo kuufanya upinzani wa Tanzania ulivyo sasa kuwa kikwako cha mabadiliko tunayoyataka na kwamba umejenga ukuta wa kuzuia mabadiliko ya kweli kuja kwani wananchi wachache wameweka matumaini katika upinzani huo ingawa ukweli ni ulivyo sasa upinzani wa Tanzania hauwezi kuthaminiwa kuongoza taifa letu.
Kama chama chenye muundo, historia, watu na raslimali nyingi kama CCM kimeshindwa kuongoza mabadiliko ya kweli kwa Mtanzania itakuwaje kwa chama kama CUF au Chadema? Kama CCM imeshindwa kufanya hivyo ndani ya miaka 45 hivi itachukua muda gani kwa upinzani dhaifu kama wa kwetu kufanya hivyo?
Ni makosa gani ambayo upinzani usipoyarekebisha haraka (ndani ya hii miezi 12) hawatastahili kuaminiwa na uongozi wa taifa hata wakiomba kwa machozi?
Au upinzani wetu unasubiri kuombewa na kupepewa ili Mungu hatimaye awaangushie masanduku ya kura kama alivyofanya kwenye masimulizi ya safari ya wana Israeli alipowaangushia mana na kuwapeperushia kware!?
Je yawezekana upinzani wetu umekuwa hauna maana na wananchi wajitahidi kuokoa merikebu inayozama wakijua ina watu wanaoweza kuifikisha mbele kuliko kurukia mtumbwi ambao hauna uwezo wa kukabili mawimbi ya bahari!?
Duh, umetupiga sana. Hata hivyo unfairly. Unapoangalia makosa ya kambi ya upinzani ni vema uangalie 'factors' za ndani na za nje. Katika SWOT analysis hizi ni fursa na vitisho. Hapo utaweza kutoa hukumu sahihi kabisa.
Vilevile ni muhimu sana kuangalia historia ya vyama hivi katika muktadha wa historia ya Tanzania na utamaduni wa kisiasa wa Watanzania. Vyama katika nyakati tofauti - kuanzia kina Marando na Bagenda, Mtei na Makani, Fundikira na Kasanga Tumbo na Mapalala na Seif walipoamua kujitoa mhanga na kuanzisha vyama - kumekuwa na hatu kadhaa zimepigwa katika kujenga dmeokrasia ya kweli katika nchi yetu.
Watu wanaiweka Tanzania katika mizania ya nchi nyingine jambo ambalo ni kosa kubwa maana Tanzania inapaswa kupimwa kutokana na historia yake. Zoezi la ujenzi wa Taifa na kuwa na Taifa moja chini ya uongozi mahiri wa Mwalimu lilifanywa katika misingi ya udikteta mkubwa sana na chini ya amri moja ya 'zidumu fikra za mwenyekiti'. Tanzania ikajenga jamii ya watu wanaoheshimu mamlaka bila kuhoji na hata vyama vingi vilipoanzishwa vilionekana ni vya wasaliti. Ni mtu mmoja tu mpaka sasa ambaye alikonga nyoyo za Watanzania na kuaminiwa - Augustino Lyatonga Mrema - lakini naye akavurugwa sana na dola, kuitwa pandikizi na kuondoa kabisa credibility yake katika jamii. Jamii imefanywa kuamini kuwa Mrema ni 'kichaa' na hana sifa ya uongozi. Hii ni kazi iliyopangwa na kutekelezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba leo ni watanzania wachache sana ambao wanakumbuka sacrifice ya Mrema katika ujenzi wa demokrasia nchini.
Tusipojifunza na kuelewa historia hii ya vuguvugu la demokrasia Tanzania tutaishia kulaumu watu kila kukicha bila kwenda mbele. CCM itaendelea kutawala na kila baada ya miaka mitano kutakuwa kinatokea chama kina nguvu na baadae kuangushwa, wabunge wenye nguvu na baadae kuangushwa na hata wanasiasa wenye mvuto na baadae kupakwa matope na kunuka.
Demokrasia hulindwa. Viongozi hulindwa zaidi ili kubakia kama alama ya harakati. Raila Odinga aliongoza harakati za mapinduzi Kenya mwaka 1982, akaswekwa lupango kwa miaka zaidi ya tisa na kuishi uhamishoni nchini Norway kwa miaka mingi. Akajiunga na chama cha baba yake mwaka 1992 FORD, kikavunjika na kuwa na FORD-K na FORD-A. Baba yake Mzee Jaramogi alipokufa Raila akataka kunyakua uongozi wa chama, akashindwa na Michael Kijana Wamalwa na Raila akaenda kuanzisha chama chake NDP. Akaivunja NDP na kuingia KANU kuwa Katibu Mkuu na akaipasua KANU vipande 2 na kuanzisha LDP. Akaingiza LDP katika muungano wa NARC na kumpa Kibaki Urais (literally alimpa Urais maana Kibaki alikuwa armchair leader of opposition). Akatoka NARC na kuanzisha ODM-K, akagombana na Kalonzo na kuanzisha ODM na leo ni Waziri Mkuu mwenye nguvu Kenya.
Mchakato wote huu Raila alionekana msaliti, mpenda vyeo na mtu wa vita. Lakini leo huna tena KANU na Raila alipata kuniambia, demokrasia Afrika itaimarika tu iwapo vyama vilivyoleta uhuru vitapasukapasuka na kuondoa ile claim yao ya sisi tulileta uhuru - hii ni claim ya CCM na hata kumkumbatia Mwalimu kama wao.
Lakini tuna kina Raila Tanzania? Mazingira ya kisiasa yanatoa fursa ya kujenga kina Raila?
Unawezaje kupewa dola ilhali vyombo vya dola havikuamini? Maana taifa haliongozwi na siasa tu. Idara za usalama na majeshi zina nafasi kubwa sana katika kuamua mustakabali wa nchi. Wanasiasa wa Tanzania ni mara ngapi tunajenga rappour na watu wa usalama ili angalau kujua wanawaza nini. Hakuna.
Mwanakijiji utaandika mpaka utachoka na kutulaumu mpaka utakasirika. Demokrasia ya Tanzania itajengwa kwa sober approach ya kutazama historia yetu na kujua 'political culture' ya Watanzania. Unatutaka tuchukue fursa inapotokea. Wazo murua kabisa. Lakini capacity ipo wapi? Wapo wap wanaofikiri na kuziona fursa? Wapo wapi watu wanaojenga scenerios na kujiuliza what if?
Tulianza vizuri zoezi la kujenga imani kwa wananchi kupitia Bunge. Tulifanikiwa kupata sizable number ya wabunge wa CCM na kujenga coalition nzuri na kupashana habari. Tukamezwa. Tukajikuta tumewauzia ajenda tukijua kabisa hawatafika nayo mbali.
Ndani ya CCM hivi sana wanachowaza ni nani atakuwa Rais ajaye kati ya Membe na Lowasa. Hakuna ajenda ya Taifa, hakuna vision pale. Lakini wanasiasa wa upinzani tunaimba nyimbo zao hawa mabwana na hata 'opinion makers' kama wewe Mwanakijiji mnaimba nyimbo zao.
Juzi nilisema hapa JF, lets be sober and scan the political situation objectively. Kinachoniumiza kichwa ni kwamba, kuna vijana wachache katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wamechoka na bickerings za wanasiasa. Watataka ku restore order! Mzee Sarakikya aliiwahi kuniasa kuwa tusiruhusu hali hiyo itokee kwani ikitokea hawatarudi makambini! Ili isitokee kuna haja ya kufikiri vizuri -
Ignore CCM