Nemesis
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 5,517
- 4,477
Lakini tuna kina Raila Tanzania? Mazingira ya kisiasa yanatoa fursa ya kujenga kina Raila?
Unawezaje kupewa dola ilhali vyombo vya dola havikuamini? Maana taifa haliongozwi na siasa tu. Idara za usalama na majeshi zina nafasi kubwa sana katika kuamua mustakabali wa nchi. Wanasiasa wa Tanzania ni mara ngapi tunajenga rappour na watu wa usalama ili angalau kujua wanawaza nini. Hakuna.
Hatuna akina Raila na tunaweza tusipate. Lakini tunashindwa kumpata Svangirai? mtu ambaye maisha yake, hamu yake, historia yake ni kupigania haki za wanyonge kikweli kweli bila woga? come on guys! Robert Mugabe alikuwa anaungwa mkono na waZimbabwe kuliko Kikwete, jamaa ni mbabe kuliko yeyote yule Tanzania. ZANU-PF ilikuwa inaungwa mkono kuliko CCM inavyoungwa mkono.
Lakini tumeshuhudia wananchi wa Zimbabwe wakichagua wabunge wa upinzani na Svangirai akipata zaidi ya 47% licha ya Mugabe kuiba na kutishia maafisa wa kura. Mkuu wa majeshi wa Zimbabwe alishasema hawezi kumpigia saluti kiongozi wa upinzani hata akishinda Urais. Lakini wananchi bado walimchagua Svangirai. Wananchi walipiteswa na wengine wakauawa lakini bado tu.
Upinzani wa Tz umejifunza nini toka MDC?
Mkuu Zitto, muda huu ndo ulikuwa wa kujenga chama na kuhamasisha wananchi kwa ajili ya uchaguzi. Lakini kimyaaaa hakuna operation sangara wala zinduka. Viongozi wetu mnasubiri muda wa kampeni. Hakuna ushindi hapo. Ninawasiwasi sana na ninyi viongozi wetu, kama kweli mnania thabiti ya kushika dola.