Makosa yaliyowagharimu Simba leo Agosti 13, 2022

Umeona goli la sakho lile licha ya simba kufungwa ila wametoa burudani safi kabisa derby hazitabiriki kama furaha ya Yanga nikuifunga simba halafu kimataifa mnatobolewa basi hongereni tukutane CAF kwa wakubwa huko.
Mbumbu x2
 
Hana kosa lakini hana ubora sana. Ubora wa kipa unaonekana mabeki wanapofanya makosa. Kuitwa kipa bora maana yake ni kufanya saves.
Hakuna kipa asiepigiwa mashuti lakini sio ukipigiwa iwe imo kisa eti mabeki wamefanya makosa. Magoli yote yamepita karibu yake na huyu angekuwa ndie kipa kule south dhidi ya Orlando hata penati tusingefika.

Ukweli ni kwamba Manula yuko mbali sana yaani kaimarika wakati Beno ni Manula wa zamani.
 
Simba wakiulizwa ni kwa nini huwa wanafungwa na Yanga kila siku👇😁😁😁
Your browser is not able to display this video.
 
Simba viongozi wao wanajifanya wajuaji, usajili wanafanya wanavyojisikia wanasingizia mapendekezo ya kocha.
Unamtoa Thadeo umemsajili nani kuziba nafasi yake swala la ushambuliaji limeongelewa muda mrefu lakini wachezaji wanaoleta hawakidhi Bado wameendelea kujaza mawinga na viungo washambuliaji.
Kufanya mazoezi ya wazi hii imesemwa lakini wanajifanya hawasikii.
 
Simba imefungwa kwa makosa ya bench la ufundi sio uwezo wa mchezaji mmoja mmoja.Bench la yanga liliamua matokeo uku la simba likiamua kupoteza mchezo.Makosa madogo madogo uwanjani yapo na nikawaida ndo maana timu zinafungwa ila je baada ya kufungwa unakuja na mbinu gani za kurekebisha mambo ili nawewe ufunge hapo ndipo bench la ufundi la simba lilipokwama.Kakolanya ni mzuri ila ana tatizo lakukosea makadirio wakati wa kuruka.Ni golikipa ambaye hafatilii moves za mpira kwahiyo akipigiwa shuti ndo anakua kama anashtuka na kuruka ndo maana jana kafungwa magoli ya aina moja.
 
Footwork yake haipo sawa kuanzisha mashambulizi na mipira ya juu haruki.

Kwenye footwork nakuunga mkono na hili sio tatizo la Beni tu hata Manula footwork yake sio nzuri sana, yule kipa wa Yanga kaiva katika hili.
 
Ata mimi naona usajili wa kocha ni huyo mzungu tu ila wengine ni usajili na ujuaji wa viongozi wao wenyewe.
 
Ata mimi naona usajili wa kocha ni huyo mzungu tu ila wengine ni usajili na ujuaji wa viongozi wao wenyewe.

Mzungu na yule beki Outtara. Jana kocha kakosea mwenyewe tu kwa zile sub zake, pale ni bora angempumzisha mwenda akaingia kapombe basi.
 
Simba kipindi cha kwanza mmecheza mchezo mzuri lakini binafsi nadhani ni sababu ya wrong selection ya kikosi kwa kocha wa Yanga.

Aziz alianzia pembeni ambapo sio mzuri sana akitokea pembeni hivyo alichezeshwq off position pia Farid Musa anapenda sana kuchezea mpira na kufanya beki line ya Simba i recove position kwa haraka.

Alipoingia moloko ana kasi na Aziz ki akarudi kati kule pembeni hapo ndipo Yanga wakarudi mchezoni.

Mzungu siwezi kumlaumu ameingia tayari Simba mmeshapoteana mipira haifiki kwa wingi mbele.
 
Simba wana bahati kufungwa magoli mawili tu, ilitakiwa yawe manne. Wanaudhaifu mkubwa sana, wajitathmini kama kweli wanataka kufika mbali.
 
Shida kubwa ya Simba ni kiungo mkabaji ambaye yuko fiti na active uwanjani kwa dk 90 sio unamtegemea mkude anae duwaa hana spidi hajui kukaba na akikaba anakabia matako,magoli yote yalifungwa huku mkude akimuangalia Mtoa pasi bila kumdistab.
Bila kumsajili Kiungo wa ukabaji katili au inonga apandishwe sita pale nyuma wacheze Onyango na Outtara tutaendelea kupigwa.Yote kwa yote Kuna kitu kimebadilika kwenye tm tumpe mwalimu muda
 
Umeona goli la sakho lile licha ya simba kufungwa ila wametoa burudani safi kabisa derby hazitabiriki kama furaha ya Yanga nikuifunga simba halafu kimataifa mnatobolewa basi hongereni tukutane CAF kwa wakubwa huko.
Goli la Sakho ni offside ya wazi kabisa
 
Goli la Sakho ni offside ya wazi kabisa
Mh mh basi mbili bila na bora mmeshinda yanga maana lingebaki lile moja lawama zote zingeenda kwa tff.
 
Hata kumuanzisha Kibu na Kyombo ni makosa hawa wote wanafanana ni watumia nguvu na papara,ni sawa na Kanoute na mkude sio wazuri kunusa hatari na mkude ndio hajui kabisa art ya kukaba
Mzungu na yule beki Outtara. Jana kocha kakosea mwenyewe tu kwa zile sub zake, pale ni bora angempumzisha mwenda akaingia kapombe basi.
 
Mpira wa Bongo bado sana kiungo mkabaji sio lazima awe katili kuna watu wanakaba soft na ni bora wana cut pass lines tu mfano Busquets na Rodri ushawaona wana ukatili?

Mpira umechange sana hufikurii kwanini viungo wakatili wana fail kotei alikuwaje anakaba sana ila team ikiwa na mpira hana faida vivyo hivyo kwa Lwanga anakaba ila team ikiwa na mpira ni useless.

Kocha wa simba alikosa plans na usajiri wa okwa sjui Okra naona ni kamari tu wazee

Kama wapo serious wamchukue manzoki haina ata haja ya kuwa na kiungo mvunja kuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…