Makosa yaliyowagharimu Simba leo Agosti 13, 2022

Makosa yaliyowagharimu Simba leo Agosti 13, 2022

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari za wakati huu wadau,

Ndugu zangu wa simba poleni sana na hongereni sana yanga mabingwa wa kihistoria kwa ushindi wa leo.

Karikoo derby imemalizika kwa ushindi wa goli 2 kwa 1 kwenye mchezo huo ilaUkiangalia mechi jinsi ilivyokuwa team ziligawana umiliki wa mpira na uchezaji katika vipindi tofauti kwa maana ya yanga kipindi cha pili na simba kipimo cha kwanza na kila team ilitumia kipindi chake vizuri na matokea kumalizika kwa yanga kushinda kwenye mechi hyo.

Licha ya simba kucheza vizuri kipindi cha kwanza ila walipoteza nafasi nyingi ambazo zingeweza kuwa magoli lakini kiyombo na kibu denis walikosa utuliku kama waliokuwa nao sakho na chama wanapoingia kwenye box au karibu na lango la mpinzani.

Izrael Patrick mwenda hakutakiwa kurudi kipindi cha pili alifanya makosa mawili kipindi cha kwanza baada ya kupiga back pass zilizoishia njiani na kuishia kwa wachezaji wa team pinzani lakini hata kwenye kushambulia na kukaba kwa wakati hakuwa na kasi na kusababisha inonga kufanya kazi yake alipokosekana kapombe alihitajika kipindi cha pili.

Simba wanahangaika na usajili ila eneo la goal kipa hawalipi kipao mbele licha ya kuwa na changamoto pale simba ukimtoa manula hakuna kipa mwenye consistency kucheza iwe kwenye league au kimataifa kakolanya ana shida ya mipira ya juu na ile ya kurudishiwa mingi anapiga nje badala ya kuanzisha mashambulizi mbadala wa manula unahitajika wasipokuwa serious simba kwenye eneo hlo yajayo yana furahisha kakolanya hafai kwenye league wala kimataifa kiwango kimeshuka huenda kukaa benchi mda mrefu kumemuathiri.

Enonga ni beki mzuri ila ana masikhara sana iwe mechi za kimataifa au za league kuu viongozi huenda wanaliona hlo tatizo ila wanalipuuzia na leo athari yake imeonekana kuna siku atakuja kuigharimu team kwenye mechi muhimu zaidi ya leo tshabalala alitakiwa aongee naye wakati mchezo ukiwa unaendelea kama captain ila badala yake mkude ndo huwa ana ongea mara kwa mara enonga asipoacha utoto yajayo yanafurahisha.

Striker za simba ni tatizo jingine aina ya uchezaji wa kibu na kiyombo unafanana ni wachezaji ambao hawana utulivu wakiwa na mpira sehemu wanayo takiwa watoe pasi wanapiga sehemu ya kupiga wanapiga chenga zisizo na maana hawana utulivu kwenye eneo la mwisho yule mzungu hafai hata ndondo cup maana hata fitness yake haipo sawa ndo maana leo ilikuwa wanakosa nafasi za wazi za kufunga na kutoa pasi.

Simba imebadilika ikiwa haina mpira inacheza vizuri kwa ku retains possession haraka na kuziba nafasi zilizo wazi mpaka pale alipotoka sadio kanoute, chama na mkude ndo hali ikaanza kubadilika maana Aziz Ki na Feisal walikuwa free na kutengeneza nafasi za magoli labda kocha wa simba kuna kitu alitaka kujaribu lakini hakikufanikiwa na simba kupoteza mchezo.

Kocha wa simba anaonekana anapenda soka la kasi team ikiwa na mpira ila katika vitu vitakavyomuondoa haraka simba ni sakata lake la kumkataa phiri na kumchezesha mzungu na kumuamini zaidi mwenda kuliko kapombe na chama anavyowaamini akiendelea hvyo hamalizi msimu hata derby ijayo anaweza asifike.

NB:Tatizo kubwa la yanga hawajui kucheza kipindi wakiwa hawana mpira kwa walivyocheza leo wakikutana na team yenye kasi kama ilivyokuwa vipers watapata tabu wanachelewa kurudi kwenye eneo la ulinzi na ku retains possession kwa haraka.

Huu sio uchambuzi ni mtazamo na maoni yangu na wewe unaruhusiwa kuweka ya kwako.
 
Ndo Mpira. Vijana Japo Wamepoteza Lkn Strong Message Wametoa KWAMBA HUU MOTO NI MPAKA SEMI FAINO CAF. Ndo mana CAF waliwaalika ARUSHA. Yes Mwaka huu Hawataishia Quarter.....SEMI tu.

Hii ni misamiati Kwa Uto..
 
Mimi nimeangalia mchezo lakini sijaona kosa lolote la Beno. Hakuna kosa la kipa hata moja. Sheria ya ulinzi ni mabeki wakabe mtu asipige, akipiga na kama hajakulenga kwa size ya goli basi asilimia ya kufungwa inakuwa kubwa. Kaka unazungumzia kiwango cha Beno kivipi?
 
Footwork yake haipo sawa kuanzisha mashambulizi na mipira ya juu haruki.
 
Mimi nimeangalia mchezo lakini sijaona kosa lolote la Beno. Hakuna kosa la kipa hata moja. Sheria ya ulinzi ni mabeki wakabe mtu asipige, akipiga na kama hajakulenga kwa size ya goli basi asilimia ya kufungwa inakuwa kubwa. Kaka unazungumzia kiwango cha Beno kivipi?
Kakolanya kwa Leo kacheza vizur japo mengine kachambua vizur fitness ya Simba inabid iboreshwe

Watan zetu utopolo hongeren kwa ushind
 
Maoni yako ni mazuri, ila siungi mkono point yako kwa Beno.
Ni kweli akipewa mpira under pressure anapiga nje ( sio mara zote), hiki ni kitu ambacho hutokea kwa wengi wakiwa kwenye pressure.

Japo kukosa application kumemfanya asiwe yule Beno ninaemjua mimi, ila ana utulivu sana kuliko Manula.
 
Ndo Mpira.... Vijana Japo Wamepoteza Lkn Strong Message Wametoa KWAMBA HUU MOTO NI MPAKA SEMI FAINO CAF..... Ndo mana CAF waliwaalika ARUSHA. ...Yes Mwaka huu Hawataishia Quarter.....SEMI tu.
Hii ni misamiati Kwa Uto..
Hiki ndicho kinacho waponza mdomo
 
Habari za wakati huu wadau,
Ndugu zangu wa simba poleni sana na hongereni sana yanga mabingwa wa kihistoria kwa ushindi wa leo...
Wazungu wote pale hawahitaji kupewa mechi nyingine kwani kocha kazingua sana kumuacha Kapombe na Phiri.
Pia hakuwa na sababu kumtoa Chama.

Hata hivyo nadhani viongozi wajiuzulu maana sidhani kama ni watu wa mpira na sidhani kama wanasikia ushauri wa wachezaji wa zamani wa Simba.

Simba hatutakiwi kuwachekea hawa viongozi
 
Umeona goli la sakho lile licha ya simba kufungwa ila wametoa burudani safi kabisa derby hazitabiriki kama furaha ya yanga nikuifunga simba halafu kimataifa mnatobolewa basi hongereni tukutane CAF kwa wakubwa huko.
Sasa kwa hicho kikosi chenu Makolo mnatoboaje CAf..? Hv umesahau yaliyowakuta mwaka Jana kwa Mkapa,,,, Sasa mwa huu mko prelimenary level MTAJUA hamjui dadeq
 
Maoni yako ni mazuri, ila siungi mkono point yako kwa Beno.
Ni kweli akipewa mpira under pressure anapiga nje ( sio mara zote), hiki ni kitu ambacho hutokea kwa wengi wakiwa kwenye pressure.

Japo kukosa application kumemfanya asiwe yule Beno ninaemjua mimi, ila ana utulivu sana kuliko Manula.
Labda ni Manura, Lakini Manura ni mstaarabu hawezi kuwaza hivi!
 
Sasa kwa hicho kikosi chenu Makolo mnatoboaje CAf..? Hv umesahau yaliyowakuta mwaka Jana kwa Mkapa,,,, Sasa mwa huu mko prelimenary level MTAJUA hamjui dadeq
Kwa hyo simba kufungwa na yanga ndo ishakuwa mbovu hvyo
 
Back
Top Bottom