Naomba Wizara ya Elimu pamoja na Bodi ya Huduma za Makataba Zanzibar kushughulikia changamoto hii haraka iwezekavyo, tunapata wakati mgumu sisi Wanachama pamoja na Watumishi wa hapo ambao asilimia kubwa ni Wanawake.
Hii changamoto imekuwepo kwa muda mrefu na hata leo hii Januari 21, 2025 hali ni hiyohiyo kiasi kwamba wale tuliohitaji kupata huduma tumelazima kuondoka hapo ili kwenda maeneo ya jirani kupata huduma.
Wanawake wanashindwa kufanya huduma zao binafsi kwa kuwa hakuna maji, wapo wengine wanaolazimika kwenda na maji kwenye madumu ili wakihitaji huduma waipate.
Unakuta mtu upo hapo kwa kutwa nzima kutokana na aina ya kazi iliyokupeleka pale, ukitaka kwenda kujisaidia unalazimika kwenda kwenye vyoo vya maeneo ya jirani.
Wengine ambao wanateseka ni Watoto, wanakuja hapa kusoma ila hakuna maji, wanawezaje kuvumilia kukaa na haja kubwa au ndogo?
Malalamiko yamekuwa mengi, tunaishi kwa kulalamika lakini hakuna hatua ambazo zinachukuliwa, hata Watumishi pia wanalalamika kwa kuwa nao ni sehmu ya wanaoteseka, tunaomba hili lifanyiwe kazi haraka.
UONGOZI WA MAKTABA
JamiiForums imewasiliana na Mkurugenzi wa Bodi Ya Huduma Za Maktaba Dkt. Ulfat Abdul-Aziz Ibrahim kuhusu suala hilo amesema:
“Ni kweli kulikuwa na changamoto ya maji hapo Maktaba lakini tayari tumenunua mtambo mpya na imetatuliwa na huduma ya Maji inapatikana.”