Maktaba yangu ya nyumbani

Maktaba yangu ya nyumbani

Quantum Physics na wenzake
Mambo ya cosmos
History & pre history
Self help books
How to books
Film & television books
Nutrition books etc
Safi sana, mimi natafuta cha kuanza kusoma sasa, nimemaliza kusoma "Frederick Douglass: Prophet of Freedom" cha David Blight.

Kilipata tuzo ya Pulitzer mwaka jana.

Kirefu kidogo (kurasa 764 za kitabu chenyewe) lakini historia nzuri sana.

9781416590316_p0_v6_s550x406.jpg
 
Kuna kubishana, halafu kuna kuchezea kipigo.

Mshana Jr kwangu anachezea kipigo tu.
Yule hana uwezo wa kufikia akili yako.. Uwezo wako wa kureason na kuargue ni world class ability. Mshana Jr ni mbabaishaji alietaka kupata cheap popularity kupitia kwako I'm glad ulimpa za uso kwa facts in issue through logic and rhetoric.

Huwa unaniinspire sana Kiranga
 
Kuna kubishana, halafu kuna kuchezea kipigo.

Mshana Jr kwangu anachezea kipigo tu.
Kiranga wewe ni mwepesi mno kwangu... Kumbuka sifa ni kusifiwa sio kujisifia... Unapotanguliza sifa mbele tayari hilo ni tatizo
 
The Monk, kuna vitu viwili kama sio vitatu vitakubadilisha, watu unaokutana nao na vitabu unavyosoma.

Nyongeza... Watu unaokutana nao na maandishi wanayoandika!
 
😂😂😂. Siwezi kugawa au kuuza vitabu. Nimeshindwa kabisa. Na utunzaji wa vitabu ni full time job. Ndo maana vitabu vyangu huwa navipeleka nyumbani kwa wazazi kwasababu wana library system ya kutunza vitabu.

Sina uchoyo wa vitu isipokua kwenye vitabu. Ukihitaji ntakwambia njoo usome nyumbani ukimaliza kiache. Na sababu ni kwamba, mwingine atapata mhemuko anakuomba kitabu hata kama hata kisoma na hakirudishi.

Pili unaweza kubahatika mtu akakirudisha lakini utunzaji tunatofautiana, kitabu kinarudi lakini unakikataa kwamba sio chenyewe kwa jinsi kilivyobadilika rangi na muonekano, hapo sijaongelea wale wanachora au kuweka highlighter kwa maandishi.
 
Kiranga wewe ni mwepesi mno kwangu... Kumbuka sifa ni kusifiwa sio kujisifia... Unapotanguliza sifa mbele tayari hilo ni tatizo
Hakuna sifa zaidi ya kukaririwa.

Unaponikariri kwamba sifa ni kusifiwa si kujisifia, unanisifia.
 
Sijawahi kusoma kitabu nikakimalizaa....
Kibongobongo huku uhitaji kusoma sana vitabu mana changamoto za maisha si kubwa sana....

Kaelimu haka tu hapa mtaani naonekana alwatan.

Hata nikisoma naona havitakuwa na maana kwa watu wanaonizungukaa.

Maisha yanasonga, ugali na kachumbari napata.

Nisome nini kipya mazee?

Maisha haya nayafurahia vizuri sana tu.

Kusoma Ulaya, bongo ubaya ubaya.
 
Mshana hajui lugha na hawezi kujenga hoja kimantiki.

Quite possibly hajui lugha kwa sababu hawezi kufuatilia hoja kimantiki.
Kujenga hoja ni sayansi ya kimahesabu inayotaka ujuvi wa kuwa umesoma vitabu vingi na uwe na knowledge pana.

Mshana Jr yeye huwa anabishana ili aonekane na yeye kabishana na mtu mkubwa JF kama Kiranga ila kiranga anatumia skills za kufanya argument kwa method tofauti tofauti na anakimudu kiingereza cha ndani saana tofauti na bwana mortuary attendant.
 
Kiranga,

Yes ni kizuri sana. Nimeshakisoma. Tafuta Death of a Nation by Dinesh D'Souza na The Bluest Eye by Toni Morrison.
 
Sina uchoyo wa vitu isipokua kwenye vitabu. Ukihitaji ntakwambia njoo usome nyumbani ukimaliza kiache. Na sababu ni kwamba, mwingine atapata mhemuko anakuomba kitabu hata kama hata kisoma na hakirudishi.
Pili unaweza kubahatika mtu akakirudisha lakini utunzaji tunatofautiana, kitabu kinarudi lakini unakikataa kwamba sio chenyewe kwa jinsi kilivyobadilika rangi na muonekano, hapo sijaongelea wale wanachora au kuweka highlighter kwa maandishi.
Kabisa. Watu wengi wanachukulia poa vitabu hawatunzi. Yaani kwao siyo kitu cha maana.
 
Mkuu Nyani Ngabu hongera sana kwa maktaba nzuri nyumbani.

Kwa mtiririko wa hivyo vitabu utakua into IT and/or Business field.

Binafsi sio mtunzaji mzuri sana wa vitabu huwa nagawa mara tu nikimaliza au kuviacha popote pale.

Nimekua muumini wa vitabu soft copies but for some reason bado nanunua magazines hardcopies, siwezi kabisa kusoma magazine online, hii leo nimenunua Men's Health na National Geographic.

Vitabu vya Kiswahili nilivyowahi kusoma bado ninavyo ila sasa nimekuwa-inspired kuanza kutunza vitabu vyote.
 
Quantum Physics na wenzake
Mambo ya cosmos
History & pre history
Self help books
How to books
Film & television books
Nutrition books etc

Nice. Last year nilisoma Astrophysics for People in a Hurry by Neil Tyson it was a good read.
 
Mimi kwenye simu ndo ninavyo vingi nadownload nasoma.

Ila sisomi novel na vitabu vyote vinavyofundisha formal education nadhan tutakuwa na taste tofauti.
 
Back
Top Bottom