JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Makubaliano yote ni mikataba kama yatakuwa yamefanywa kwa hiari na watu wanaostahili kufanya makubaliano, kwa malipo ya kitu halali na ambayo hayajatajwa waziwazi na sheria hii kuwa ni batili:
Mikataba yote inatakiwa iwe kwenye maandishi au ifanywe mbele ya mashahidi, au sheria yoyote ihusuyo usajili wa nyaraka.
Sheria hiyo inabainisha kuwa kila mtu mwenye umri wa mtu mzima na mwenye akili timamu, ambaye hajazuiwa na sheria yoyote, ana uwezo wa kuingia mkataba.
Makubaliano yanayofanywa na mtu ambaye hajatangazwa na sheria hii kuwa na uwezo wa kufanya mkataba, makubaliano hayo kisheria ni batili.
Katika kufanya mkataba, mtu anasemekana kuwa na akili timamu wakati wa kufanya mkataba ikiwa ana uwezo wa kuelewa na kutafakari maslahi yake katika mkataba husika.
Sheria inaongeza kuwa mtu ambaye mara nyingi anakuwa na matatizo ya akili, lakini muda mfupi anakuwa timamu, anaweza kufanya mkataba wakati anapokuwa na akili timamu.
Na mtu ambaye mara nyingi anakuwa na akili timamu, lakini muda mfupi anakuwa na matatizo ya akili, hawezi kufanya mkataba muda anaokuwa na matatizo ya akili.
Upvote
2