Makubaliano yaliyopitishwa bungeni ni makubwa kisheria kuliko mkataba wowote wa bandari utakaotengenezwa

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Kumekuwa na upotoshaji wa kimakusudi unaofanywa na spika, baadhi ya wabunge, viongozi wa serikali na wapiga debe wengine wa sakata la Bandari kupewa DP world.

Wapiga debe hao wamekuwa wakisema kilichopitishwa bungeni ni makubaliano tu ya ushirikiano na sio mkataba, hivyo makubaliano hayo ni jambo dogo lisilo na athari zozote mbaya kwa taifa kwa kuwa mkataba wenyewe bado haujatengenezwa na utakuwa imara na bora zaidi kuliko hayo makubaliano.

Sasa ili kuondoa upotoshaji na kuweka kumbukumbu sawa hapa JF, sote tunapaswa kufahamu haya.

1. Makubaliano, mapatano, mashauriano au mapendekezo yoyote baana ya pande mbili, yanayowekwa chini kimaandishi na kufungwa kisheria, huo ni MKATABA.

2. Mkataba mmoja mkuu, taratibu na baadaye unaweza kuzaa ndani yake mikataba mingine mingi midogo midogo huku ikizingatia mkataba mkuu.

3. Kilichopitishwa bungeni kuhusu bandari na Dubai (DP world) (ambacho wapiga debe wamekiita ni makubaliano) kiuhalisia ndio mkataba mkuu na ndio mkataba mama (Hakuna tena mkataba mwingine wenye nguvu ya kisheria ya kupindua, kugeuza au kutofautiana na huo mkataba mama).

Kama kuna kasoro zozote kwenye hicho kilichopitishwa bungeni sote tujue hakuna mkataba mwingine wowote utakuja kuzifukia.
 
Hivi wewe unaipenda Tanganyika ?
 
Back
Top Bottom