Rachel P
Senior Member
- Dec 26, 2024
- 151
- 617
Kiumbe mwanadamu amefanywa katika misingi ambayo inamgawasha katika category muhimu ambapo kila category ni complimentary au sub ya kundi jingine.
Mfano, Mwanamke na mwanaume ni category za kijinsia zenye utofauti mkubwa lakini kila moja inamcompliment mwenzie kama taswira ya kioo na kitu halisi.
Bila kujali jinsia viumbe hawa wamegawashwa makundi manne ya hulka na tabia zenye kuwakilisha element muhimu za uhai. Yaani maji, hewa, moto na udongo.
Wanadamu wenye kundi la maji na hewa huwa na asili inayofanana huku wa kundi la moto na udongo wao wana asili tofauti na special kwa kila moja.
Tuanze na kundi la maji.
Hawa ni watu wenye hisia kali na hufanya maamuzi ya utashi wao kwa kuangalia hisia zao bila kujali reasoning wala logic za maamuzi yao. Wao hupenda kuzungukwa na watu wanaoelewa hisia zao na kujaribu kuvaa hisia za wengine (sympathy) ili kujiwekea ulinzi wa kutoumizwa au kuumiza hisia za yeyote.
Kwa kufanya hivyo wao ndio wanaoongoza kwa kuvunjika mioyo.
Tuje watu wa hewa.
Watu wa hewa wao huongozwa na maneno au sauti zinazoleta taarifa katika kuamua au kuendesha maisha yao kwa ujumla. Ni watu waongeaji sana na wanaopenda kujua mambo ya wengine kuliko ya kwao.
Wao huongozwa na maoni ya watu wengine kwa kusikiliza maoni yao na kujaribu kujiweka sawa na vile wengine wanasema kuhusu wao au watu wengine.
Muda mwingi hupenda kusikiliza au kuzungumzia habari za watu wengine hasa zile zenye asili ya usiri.
Hii huitumia kujitengezea wao taswira yao kwenye macho ya watu wengine kupitia maoni ya watu wengine kuhusu wao wenyewe au wale wanaowazunguka.
Na kama vile ilivyo tabia ya hewa kuchukua umbo la chochote ilicho ndani yake. Watu hawa pia wanabadilika haraka na kuchukua haiba mpya kulingana na maoni ya watu wanaowazunguka.
Twende kwa watu wa moto ...
Watu wa moto wao ni wenye kutengeneza logic zao kwa kulazimisha kuonekana au kujionesha au kutengeneza attention. Wao hufurahia na kutamani sana kuwa ndio kitovu cha hamasa na attention za watu wengine.
Watu hawa hupoteza haiba zao na hata furaha pale wanapogundua kwamba watu wengine hawawaoni au hawawapi attention wanaoitaka. Ni watu wakorofi mara nyingine ili kuhakiki kama wana attention wanayoitamani kila wakati.
Wanaongoza kwa kupenda madaraka ubabe na kupaza sauti zao kila wanapowasiliana hata kama haikuhitajika sauti ya juu katika mazungumzo husika.
Kundi hili huitwa kundi la kwanza au kundi namba moja kutokana na kupenda sana ushindani na ubishani ili kujihakikishia wanapata attention toka kwa wengine wanaowazunguka.