Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru, mikoa mbalimbali nchini imejitokeza kushiriki shughuli za kutunza mazingira, ikiwemo kufanya usafi na kupanda miti.
Mkoani Morogoro, Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana na Kikosi cha Mazao Mzinga na wadau wa mazingira wamepanda miti 7,000 katika eneo la hifadhi ya bwawa la Mindu. Bwawa hili linatoa huduma ya maji safi kwa zaidi ya 75% ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro.
Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Mhandisi Elibariki Mmassy, aliwataka wananchi kuacha tabia za uharibifu wa mazingira, akionya kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi ya waharibifu.
Mkoani Tabora, zaidi ya miti 67,000 ilipandwa katika maeneo mbalimbali, ikiwemo zahanati ya Maili Tano ya Ipuli. Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Mohamedi Mtulyakwaku, aliwataka viongozi wa wilaya na wananchi kuhakikisha miti inasimamiwa na kustawi.
Mhifadhi Mkuu wa TFS, Nuru Tengeza, alisema zoezi hilo ni endelevu na linahusisha kugawa miche ya miti kwa wananchi. Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. John Mboya, alisisitiza kuwa kulinda mazingira ni jukumu la kila mtu, huku Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Sauda Mtondoo, akiahidi kusimamia upandaji na utunzaji wa miti katika wilaya yake.
Aidha, katika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania, vijana wa Generation Samia (Gen S) wamejitolea kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, wakitoa shukrani kwa waasisi wa taifa na kupongeza juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuliletea taifa maendeleo.