Makundi sita (6) ya hatari za kuwekeza kwenye ardhi/majengo

Makundi sita (6) ya hatari za kuwekeza kwenye ardhi/majengo

Aliko Musa

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
209
Reaction score
315
Wengi huamini kuwa kutawanya uwekezaji uhusisha kuwekeza mitaji fedha kwenye aina tofauti tofauti za bidhaa au huduma. Lakini hii sio kweli. Ni rahisi kutawanya uwekezaji kwenye hisa kwa sababu bei za hisa ni nafuu ukilinganisha na bei za ardhi na majengo.

Kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo, ni vigumu sana kutawanya mtaji fedha kwa kumiliki ardhi au majengo mitaa tofauti tofauti kutokana na sababu ya ardhi au nyumba kuuzwa kwa bei ghari.

Lengo La Kutawanya Uwekezaji Kwenye Ardhi Na Majengo.

Lengo kuu la kutawanya mitaji fedha ya mwekezaji ni kupunguza hatari za uwekezaji uliofanywa.

Zaidi ya hatari ya masoko, utawanyaji wa mitaji fedha hauwezi kukunufaisha kwenye ardhi na majengo.

Makundi 6 Ya Hatari Ya Kumiliki Ardhi Na Majengo.

Moja.

Hatari ya soko.

Hii ni maarufu zaidi kwenye uwekezaji wa hisa ambao hatari ya masoko ni kawaida. Kwenye ardhi na majengo, unatakiwa kuweka umakini mkubwa kwenye uchaguzi sahihi wa ardhi na majengo.

Usitumie taarifa za kitaifa kufanya maamuzi ya kutathmini hali ya soko mahalia. Hakikisha unatumia taarifa za soko mahalia ili kujifunza historia yake na muenendo wa sasa wa hali ya soko.

Fuatilia idadi ya nyumba zilizopo sokoni, tofauti kati ya bei ya kutangaza na bei ya kuuzia, na idadi ya siku ambazo nyumba hutangazwa mpaka kufanikiwa kuuzwa.

Mbili.

Hatari ya uhitaji wa chumba.

Uhitaji wa chumba unapimwa kwa kutathmini hali ya kukosa wapangaji au kiwango cha kuwa na wapangaji kwa mwaka mzima.

Huwezi kutawanya mitaji fedha kwenye miji tofauti kwa sababu ni kazi ngumu kusimamia nyumba zilizojengwa kwenye miji au mikoa tofauti tofauti.

Hivyo, hapa utakuwa unapima hatari ya kukosa wapangaji kwenye chumba kimoja kimoja. Mfano; utakuwa unapima nyumba yenye vyumba viwili vya kulala inapata wapangaji kwa viwango gani ukilinganisha na nyumba ya vyumba vitano vya kulala.

Unatakiwa kupata tathmini ya muda mrefu ili kujenga picha kamili ambayo inaweza kukusaidia kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua nyumba ya kupangisha ambayo itakuwa na hatari ndogo ya kukosa wapangaji bora.

Tatu.

Hatari ya migogoro ya wapangaji.

Jinsi unavyokuwa mbali kutoka nyumba yako ya kupangisha ilipo mpaka unapoishi ndipo kunakuwa na hatari kubwa ya kuwepo kwa migogoro wa wapangaji.

Pia, nyumba zako kujenga kwenye mitaa tofauti tofauti ndipo unaongeza hatari ya migogoro ya wapangaji wa nyumba zako.

Njia pekee ya kupunguza hatari za migogoro ya wapangaji ni kuchunguza taarifa za sasa na zilizopita za wapangaji wanaotoka kuhamia kwako. Chunguza historia ya matukio ya uhalifu waliowahi kufanya kabla ya kutaka kuhamia kwenye nyumba yako.

Nne.

Hatari ya kipato endelevu.

Hii ndiyo hatari kubwa zaidi kuliko hatari nyingine za kuwekeza kwenye ardhi na majengo. Mwekezaji anakuwa hatarini kuingiza kipato hasi cha kila mwezi au kila wiki.

Hii itaharibu mambo yafuatayo;-

✓ Mfumo wa kawaida wa bajeti binafsi ya mwekezaji.

✓ Hali ya kukopesheka ya mwekezaji.

✓ Kiasi cha kipato endelevu cha mwezi au wiki.

Changamoto ya kutawanya mtaji fedha ni kuwa unahitaji kumiliki majengo mengi ya kupangisha. Hii inakuwa vigumu kutimiza lengo lako kuu la kupanguza hatari ya kipato endelevu.

Hatua za kukabiliana na hatari za kipato endelevu ni kama ifuatavyo;-

✓ Kuwa na kiasi kikubwa cha mtaji fedha wa kuombea mkopo wa majengo. Hii itarahisisha sana kukamilisha marejesho ya mkopo ya kila mwezi hata kipindi cha hali mbaya ya upangishaji.

✓ Kuwekeza kwenye nyumba zenye kasoro kisha kuzifanya za kupangisha. Hii itaongeza nafasi kubwa ya kutengeneza kipato chanya cha nyumba za kupangisha.

✓ Kununua kwa kutumia mkopo wakati ambapo kodi za majengo ni kubwa kuliko marejesho ya mkopo ya kila mwezi.

Tano.

Hatari ya kuuza kwa pesa taslimu.

Ardhi na majengo ni uwekezaji ambao ni vigumu sana kupata fedha (an illiquid investment). Hivyo ili kupata fedha unatakiwa kuuza, au kuombea mkopo nyumba au ardhi yako.

Unahitaji kuwa na akaunti ya kutunzia fedha (Savings account), akaunti za akiba na uwekezaji ambao utaweza kupata fedha kwa urahisi zaidi pale unapopata uhitaji wa haraka. Tumia kiasi kikubwa cha mtaji fedha wa kuombea mkopo wa majengo ya kununulia majengo ya kupangisha tu.

Sita.

Hatari ya riba ya mkopo.

Hii ni hatari ya kulipia kiasi kikubwa cha riba ya mkopo tofauti na faida unazopata kutokana mkopo uliopewa. Mikopo ya riba inayobadilika (variable rate loans) inaweza kuvutia kipindi cha mwanzo cha marejesho kwa sababu riba yake huwa ndogo sana ukilinganisha na riba ya mikopo ya riba isiyobadilika (fixed-rate mortgage).

Unatakiwa kununua nyumba zenye kasoro na kisha kuzifanya za kupangisha kwa miaka mitano kabla ya kuuza. Hii unaweza kuifanya hata kama umechukua mkopo wa riba inayobadilika.

Mkopo wa riba inayobadilika unafaa kwa ajili ya kuwekeza kwenye majengo ambayo utayauza ndani ya miaka miwili (2) tu. Kwenye aina hii ya hatari, kununua majengo mengi ya kupangisha sio suluhisho.

Haya ni makundi ya hatari ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo. Kutoka kwenye makundi haya unaweza kutengeneza kiasi kikubwa cha fedha au unaweza kupoteza kiasi kikubwa cha fedha ndani ya muda mfupi tu.

Muhimu; Naomba unishirikishe maoni, mapendekezo na ushauri ulionao kuhusu somo hili. Mchango wako ni wa muhimu sana kwenye kuboresha huduma zangu za uandishi wa ardhi na majengo.

Nipigie kupitia; +255 752 413 711.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Calls/WhatsApp; 0752 413 711
 
Kwenye ardhi au jengo wewe ndiyo mmiliki lakini kwenye hisa unasubiri kuambiwa tu tumepata pokea gawio au hakuna faida, hakuna gawio
 
Hapa Nakubaliana na wee👍😫👇
"Wengi huamini kuwa kutawanya uwekezaji uhusisha kuwekeza mitaji fedha kwenye aina tofauti tofauti za bidhaa au huduma. Lakini hii sio kweli"
 
Kwenye ardhi au jengo wewe ndiyo mmiliki lakini kwenye hisa unasubiri kuambiwa tu tumepata pokea gawio au hakuna faida, hakuna gawio
Biashara Ya hisa naona imekaa kitapeli Sana, sijajua Sababu niliwekeza mtaji kdg sana au vipi, nna hisa za Vodacom ila faida ata siioni
 
Binafs Nna baishara ya nyumba za kupangisha, from my experience

1. Sijengi tena single rooms,
-Wapangaji wengi wa single room Ni single afu wapitaji, hivyo suala la kudhulumiwa Kodi kawaida Sana. Nafuu kdg chumba na sebule
-Single rooms inasababisha msongamano wa wapangaj, hivyo kusababisha migogoro.
Nb: Kuna sehem nna behewa la single rooms 8,migogoro ni kila kukicha.

2. Boresha Nyumba kupunguza wapangaji wababaishaji wa Kodi.
-Nilikosea zaman kutojenga standard house nkihofia kukosa wapangaji maana jamii yetu wengi kipato Cha chini. Nisichokijua, Wapangaji wengi wa kipato Cha chini wasumbuf Sana kulipa Kodi na hawajui kutunza nyumba. Bora nichelewe kupangisha ila nipangishe mpangaji wa maana.

3. Wapangaji wenye familia Ni muhimu wakae kivyao,
-Kuwamix wapangaj mabachela na wenye familia Eneo moja inaleta Sana migogoro. Sifikirii tena kurudia hili kosa

4. KILA mpangaji ajitegemee vyoo,maji na umeme.
-migogoro mingi ya nyumba za kupanga iko kwenye hivyo vitu 3. Kuna nyumba nmeiweka hivyo, mwaka wa 2 Sasa sjaitwa kusuluisha kesi ya Aina yoyoye ile na wanaishi kwa amani Sana.

Wengine muongezee🙏
 
Asante sana sana.
 
Biashara Ya hisa naona imekaa kitapeli Sana, sijajua Sababu niliwekeza mtaji kdg sana au vipi, nna hisa za Vodacom ila faida ata siioni

Unatakiwa kufanya uchaguzi sahihi kwa kuambatana na wataalam kwenye eneo hili.

Unaweza kufuatilia masomo ya EMILIAN BUSARA kupitia mtandao wa you tube.

Pia ametoa vitabu tofauti tofauti kuhusu HISA, VIPANDE NA HATIFUNGANI.

Karibu tuendelee kushirikishana kuhusu UWEKEZAJI KWENYE ARDHI NA MAJENGO (REAL ESTATE INVESTMENT).

Rafiki yako,

Aliko Musa.
 
Hapa Nakubaliana na wee👍😫👇
"Wengi huamini kuwa kutawanya uwekezaji uhusisha kuwekeza mitaji fedha kwenye aina tofauti tofauti za bidhaa au huduma. Lakini hii sio kweli"

Asante sana na tuko pamoja.
 
Back
Top Bottom