Makundi ya Damu (blood groups) na Mahusiano

Makundi ya Damu (blood groups) na Mahusiano

Godmmit brother.. umepatia kabisa.
Kwa kuongezea group O si pushover, ni wavumilivu ila ukiwapanda kichwani watakuadhib with extreme prejudice. Halaf ni watu wa maamuzi magumu sometimes
Daah kama unanisema vile.
Mimi nikimkubali mtu kama mshikaji au hata mpenzi atafurahia sana.
Lakini pia ninajua kuvumilia kwa kiwango cha juu mno hadi watu huogopa.

Lakini nikichafukwa sawasawa we kimbia tu.
Mara nyingi hata polisi huwa nikichafukwa nalianzisha humo humo bila kujali.

Hii imenigharimu sana tu lkn jinsi ninavyoendelea kukua naona ninakuwa na subira kiasi[emoji28]

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Heshima zenu popote mlipo na poleni na kupanda kwa gharama za maisha........

Moja kwa moja kenye mada

Kuna uhusiano kati ya Kundi la damu na Tabia ya mtu katika mahusiano/mapenzi.
Kwa mujibu wa tafiti na machapisho mbali mbali zifuatazo ni baadhi ya sifa za watu kulingana na kundi la damu (blood group) katika mahusiano au mapenzi.

Blood group "A"
* Ni ngumu kidogo wao kufunguka na kushirikisha mambo yao
*Sio waongo (waadilifu na wakweli)
*Wana aibu na waoga hupenda kujificha
*Ukitaka kuchumbia au kuchumbiwa na mtu wa kundi A unahitaji uvumilivu
*Wakiamua kupenda utawafahamu wakati wote ingawa wataruhusu ufahamu sehemu ambayo unahusika. Hawawi wazi kila eneo

Blood group "B"
*Unaweza kufurahi nao sana kwenye mahusiano lakini uwe tayarii kuvumilia hasira zao za ghafla
*Vumilia hali yao ya kukwepa majukumu
*Wanaweza kuwa wakali na wakatili na wasiomaanisha kile wanachosema.
*Wanatabia ya umbea na wachonganishi sana
*Wanaweza wasiwe watu wazuri kuwa wapenzi kutokana na kukosa uaminifu na urahisi wa kuumiza mioyo ya wengine

Blood group "AB"
*Ni watu wanaoaminika kuwa wabinafsi zaidi
*Ni watu ambao mara nyingi hawaeleweki. Anaweza kuanzisha
Kitu kikaishia katikati halafu akaanzisha kingine
* Ni watu wazuri kwenye mambo yanayohusu fedha
*Ni wabishi na wakosoaji na mara nyingine hutoa maneno yanayo umiza
*Ukiwa katika mahusiano nao hufurahisha na unaeeza usiwe na nyakati nyingi za upweke

Blood group "O"
*
Huonesha mapenzi kwa wale wanaowapenda na hutarajia upendo wa jinsi ile ile wao wanavyoonesha upendo kwako bila hivyo utakosana nao
*Wanaaminika kuwa na tabia za kijeshi
*Wana roho nzuri sana ila hawapendi uongo
---###-------###------

Kutokana na utafiti huu Binafsi naona kuna uhalisia kulingana na tunayokutana nayo katika jamii.
Tabia ni kama ngozi kuisha hadi uchune japo nguvu ya "pesa" inajaribu kuficha tabia za baadhi ya watu hasa wanawake.
Tujifunze kuishi nao maana ndivyo walivyo na hawawezi badilika maana washwahili wanasema "Mbwa ukimjua jina hakusumbui"
Ukiona hamuendani kitabia na unampenda jitahidi ujue mbinu za kivita za kuishi naye blood group inaweza kukusaidia maana nzi kufia kwenye kidonda sio ufala ila kupenda

Nakaribisha maoni ......
Me ni B+ kusema kweli tabia zote ninazo tena umbea[emoji134][emoji134][emoji134] ninaongoza
 
Back
Top Bottom