Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Baadhi ya wakazi Wilaya ya Arumeru, Arusha wameomba Serikali kuingilia kati hali ya uhaba wa chakula ambayo sio ya kawaida inayoendelea katika mkoa huo.
Hali hiyo imesababisha makundi ya kina mama na watoto kutembea umbali mrefu wakitafuta chakula kwa kuombaomba maeneo tofauti, ambapo mara kadhaa wameshuhudiwa wakifanya hivyo katika nyumba za watu mbalimbali wakiomba unga na chakula.
Hali hiyo kwa sasa imedumu zaidi ya miezi miwili kutokana na ukame wa kukosekana kwa mvua.
Baadhi ya Kata zilizokumbwa na hali hiyo ya ukosefu wa chakula ni zile zilizopo katika vijiji vya Oldonyo Sambu, King'ori, Ngwansio, Malula, Kata ya Ngaramtoni, Kata za Tindigani na baadhi ya Kata za Wilaya ya Hai
Dora Mollel ni mmoja wa wanawake wanaozunguka mtaani kutafuta msaada wa chakula anasema analazimika kufanya hivyo kwa kuwa hawana hela ya kununua vyakula huku akidai kuwa bidhaa za sokoni zipo bei ya juu, kwa hiyo unafuu waliouona ni kuja mjini kupiga hodi katika mageti ya watu na kuomba unga au chochote kile.
Upande mwingine, baadhi ya wakazi wanaoshuhudia kadhia hiyo wameelezea kusikitishwa na kinachoendelea wakidai kuna wamama ambao wanafikia hatua ya kuomba hata pumba ili wakawapikie watoto wao.
Hali ya wanawake na watoto hao wanaoomba chakula pia ipo katika masoko ya Tengeru na Kisongo ambapo wahusika wanazunguka wakiwa na viroba mgongoni kwa ajili ya zoezi hilo.
Aidha, majira ya usiku wahusika hao wamekuwa na kawaida ya kuokota mabaki ya vitu sokoni kisha wengine wanaomba nauli za kurudi makwao na wanapokosekana wanalazimika kutembea umbali wa kilomita zaidi ya 6.
Siku chache zilizopita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela akiwa katika ziara Kata ya Kikatiti, mmoja wa akina mama aliyekuwa katika mkutano huo alimlalamikia kuhusiana na suala la njaa, ambapo kiongozi huyo alitoa kauli kuwa viongozi wafuatilie wahanga wa janga la njaa kutokana na ukame.
==================
UFAFANUZI WA DIWANI
Diwani wa Tarafa ya King’ori, Rosemary Mtalo amesema: “Nimeona hiyo taarifa mtandaoni, kweli kuna watu wana njaa ila siyo kama ilivyoripotiwa, lakini hatujasikia watu waliokufa kwa njaa.
“Michakato ya kuwasaidia imeshaanza, hata hapa tupo mezani tunaijadili, tumeshaongea sana, Serikali iiangalie Wilaya ya Meru na hata Mkuu wa Wilaya anayo hii taarifa.
“Tayari tumeshaandika majina ya kaya na tumependekeza wananchi wapewe chakula.”