Makundi yanayoongoza kwa ubaguzi na chuki dhidi ya watu weusi

Ubaguzi hautoisha kamwe, haswa kwa sisi waTZ tunabaguana wazi wazi kabisa wenyewe kwa wenyewe, kuanzia ngazi ya familia(washua dhidi ya wasaka tonge,
ukoo(zenye mamlaka),
rangi(waTanzania weupe wenye asili ya Asia{wahindi&waarabu} dhidi ya sie watz weusi, kipato(mf.wachaga), elimu(mf.wahaya,nyakyusa,ngoni),
n.k n.k
 
Nyinyi mbona kutwa humu mnaanzisha nyuzi za kuwabagua waarabu, wahindi na wachina wanao ishi ndani ya nchi hii?
 

Waafrica ndiyo wabaguzi kuliko hao wote!! Kinachokosekana kwa Mwafrica ni ambague nani kwa kigezo kipi?? Tunakosa vingine vyooote tumerudi kwenye ukabila, ukanda na udini!!

Angalia threads zinazoanzishwa kukashifu makabila na dini za wengine!! Wiki iliyopita kulikuwa na futari imeandaliwa na taasisi kwa watumishi wake, kuna mtumishi alidiriki kusema chakula kilichoandaliwa na Waislam sili!!

Bahati mbaya sana, waliokuwa wameorganise tukio lote la futari ni Wakristo, alishikwa na aibu sana!! Nikamuuliza na Waislam nao wakatae kula hiyo futari? Aliishia kusema tu sijamaanisha hivyo!!

Uone jinsi Waafrica tulivyo na ubaguzi mkubwa!! Na ubaguzi wetu huenda mbali zaidi mpaka kuwekeana chuki, visasi na hata kukwamishana katika maisha
 
Zile nchi ambazo bendera zao zimechorwa misalaba misalaba 🇫🇮🇬🇬🇫🇴🇸🇯🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 nchi za Scandinavia .nasikia ubaguzi uko kiwago cha chin mno
Wana exposure, wazungu wasio na exposure mfano kutembea ndio wabaguzi
 
Siku hizi wamarekani weusi na wao wanaonyesha chuki za waziwazi dhidi ya waafrika wa kutoka kusini mwa jangwa la Sahara. Yaani katika classification, sisi ndio tumewekwa kundi la chini kabisa la binadamu.
Lakini mimi nakwenda popote nonapotaka, ubaguzi hauwezi kunizuia hata siku moja. Nawahurumia watoto wangu tu kwasababu hiki kizazi cha sasa ni sensitive sana. Sio wagumu kama sisi baba zao
 
Sasa mpka hapo, umemaanisha ni dunia nzima inatubagua watu weusi
 
Mtu mweusi ndio nini? Kwanini usiseme mtu mwenye asili ya bara la afrika. Hilo jina limekaa kama tusi halifai
 
Na watu weusi wenyewe hawawezi kuungana dhidi ya watu weupe wamejawa na uchawa, usaliti na uzandiki
 
Sasa na wasomali na wenyewe wanatudharau! 😁

Wasomali miyeyusho sana aisee..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…