Makusanyo Soko la Sinza Makaburini yanaenda wapi? Hakuna vyoo wala sehemu za kutupa taka

Makusanyo Soko la Sinza Makaburini yanaenda wapi? Hakuna vyoo wala sehemu za kutupa taka

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Nimeona taarifa hii kuhusu Wafanyabiashara wa Soko la Sinza Makaburini Jijini Dar es Salaam kulalamika kuwa juu ya ubovu wa miundombinu ya soko hilo, ikiwemo uchakavu wa vyoo pamoja na kukosekana kwa sehemu maalum ya kutupa taka.

Kuna Mfanyabiashara Robert Swai ambaye amehojiwa na kusema soko hilo halina huduma ya umeme licha ya kuwa lipo katikati ya Sinza.

Nilipofika sokoni hapo baad aya kuona taarifa hii nikashuhudia mbali na vyoo pia hakuna sehemu ya kuegesha magari na wenyewe wanasema choo kilichokuwa kikitumika eneo hilo kilikuwa cha mtu binafsi lakini wamekifunga.

Unajiuliza kweli hapo kuna uongozi? Mamlaka ziko wapi? Wanaona ni sawa hii?


Video: EATV

Pia soma: Wafanyabiashara Soko la Sinza walalamika kufanyiwa ubabe wa kulazimishwa kusaini mikataba viongozi wa Halmashauri ya Ubungo
 
Mkuu acha kiherehere jali maisha mambo yako. Achia mamlaka husika itatue hizo changamoto.
 
Ccm wakija kuchangia nijulishe
FB_IMG_1677334339094.jpg
 
Angekuwepo yule mwamba angewambia hao wafanya biashara wote wakajisaidie nyumbani Kwa diwani R I.P Jiwe
 
Wacha wahusika waendelee kununua vieiti kwa pesa ya makusanyo ya soko hilo! Shame!
 
Back
Top Bottom