Nimeona taarifa hii kuhusu Wafanyabiashara wa Soko la Sinza Makaburini Jijini Dar es Salaam kulalamika kuwa juu ya ubovu wa miundombinu ya soko hilo, ikiwemo uchakavu wa vyoo pamoja na kukosekana kwa sehemu maalum ya kutupa taka.
Kuna Mfanyabiashara Robert Swai ambaye amehojiwa na kusema soko hilo halina huduma ya umeme licha ya kuwa lipo katikati ya Sinza.
Nilipofika sokoni hapo baad aya kuona taarifa hii nikashuhudia mbali na vyoo pia hakuna sehemu ya kuegesha magari na wenyewe wanasema choo kilichokuwa kikitumika eneo hilo kilikuwa cha mtu binafsi lakini wamekifunga.
Unajiuliza kweli hapo kuna uongozi? Mamlaka ziko wapi? Wanaona ni sawa hii?