Nimesikia malengo ya TRA kukusanya Tril 2 kutoka vyanzo vya ndani nadhani ni jambo jema ili kujenga msingi wa kujitegemea.
Ila naomba kujua kama Waziri Dr. Mpango anamkakati wa kutengeneza sera rafika za fedha ili kukuza uzalishaji wa ndani. Maana kodi ni matokea ya Watanzania au watu wanaofanya biashara na Tanzania kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma za ndani ili kutokea hapo kodi ipatikane.
Wizara ya fedha wana mkakati na sera za ndani ya muda mfupi kuona tunaongeza exports na kuvutia forex wakati huo tunapunguza imports??
Tunaunga mkono Rais Magufuli ila wasaidizi wake kwenye sera za fedha tunaweza kuja na majibu ya kisera kwenye say
CAPEX kwa hasa kwa Tanzanian investors ili manunuzi ya equipment(technology), na ku-train staff ili kuingiza mauzo ya nje final products za
Pamba
Korosho
Kahawa
Katani
Chai
Cocoa
Ngozi
au namna gani kwa muda mfupi tunaongeza uzalishaji wa mafuta ya kula na sukari ambazo tuna-import by 60% mafuta ya kula na sukari ya matumizi ya kawaida na industrial sugar??
Haya yakifanyika tunakuza mzunguko wa fedha, mzunguko ukiwa mkubwa kodi inapatikana.
Viwanda vya basics needs za Watanzania kama nguo na viatu say hata kwa sare za watoto wa shule, vikizalishwa ndani man power inayozalisha wakatakuwa subject to PAYE na kuchangia pension funds.
Nchi kama Netherlands na Israel ng'ombe anatoa maziwa kwa watani wa lita 30-45;
Feeding ya ng'ombe ni all sets of food inputs (qualitative and quantitative diet)
Sisi good practices ya ng'ombe wetu tunaowaswaga wanakula nyasi akifaidi sana ni pumba na mashudu; ni wastani wa lita 2-6 kwa siku.
Wakubwa, tuna shauku sana kuijenga Tanzania ikiwamo kulipa kodi; ila kodi kama ni kwa mfanyakazi ni mpaka afanye kazi mwisho wa mwezi anakatwa PAYE, kwa mfanyabiashara likewise auze bidhaa na huduma ili kupitia mauzo serikali inapata.
Wizara ya fedha, wekezeni sera za kifedha kwenye all it takes tuongeze uzalishaji wa ndani na kusisimua kukua export.
F.