Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Kumekuwa na hii tabia ambayo wahudumu wa afya wanaifanya sana kwa wagonjwa wanaotumia bima za afya. Unakuta mtu anaumwa ugonjwa fulani anaandikiwa dawa ambayo kwa makusudi kabisa wanajua dawa husika haipo kwenye orodha ya dawa kwenye fungu la bima alilopo mgonjwa husika na ni ngumu dawa hiyo kupatikana katika maeneo hayo.
Hivyo mgonjwa analazimika kulipia dawa hizo kutoka mfukoni kwake wakati kulikuwa na machaguo bora mengine ya dawa kuliko ambayo amemuandikia mgonjwa na inapatikana kwenye fungu la dawa zinazopatikana kwenye bima yake, lakini kwakuwa dawa hiyo ni ya gharama kubwa na itawapatia faida basi mgonjwa anaandikiwa dawa ambayo haipo kwenye kifurushi cha bima yake.
Hii inawapa nafasi wahudumu wa afya kijiongezea faida kinyume na utaratibu kwa kuwadhulumu na kuwapa hasara wananchi wanaolipia bima hizi. Waziri Ummy Mwalimu tafadhali liangalie hili ili wananchi wapate huduma wanazostahili kwa wakati na ubora.