Jacob Mulikuza
Member
- Jul 15, 2021
- 16
- 61
Kila mara tumekuwa tukishuhudia na kusikia matukio ya ukatili na unyanyasaji wa watoto yakiongezeka na kuripotiwa nchini Tanzania. Kutokana na ongezeko hili, jitihada mbalimbali zimechekuliwa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupunguza ukatili na unyanyasaji wa watoto.
Kwa kutambua umuhimu wa makuzi sahihi ya watoto nchini, ni vyema tukarejea kwenye misingi imara ya jamii kama nguzo muhimu ya ulinzi wa mtoto. Jitihada nyingi zimekuwa zikifanyika na mashirika yasiyo ya kiserikali kupambana na unyanyasaji na ukatili wa Watoto ila jamii kwa namna moja ama nyingine imesahau jukumu lake la muhimu kwenye makuzi na ulinzi wa Watoto.
Msomaji wa makala zangu ndugu Mariana Balampama Mkurugenzi wa Shirika lisilo za Kiserilali-Pact Tanzania alinisihi niweze kuandika Makala yenye maudhui ya makuzi ya watoto kwa kuzingatia ustawi sahihi wa watoto nchini Tanzania. Hivyo kwa ombi hili makala hii ya leo itajikita kuangalia jukumu la jamii kwenye makuzi ya mtoto na kuzuia unyanyasaji na ukatili wa watoto.
Kila jamii hupitia mabadiliko ambayo huwa chanya ama hasi. Mabadiliko makubwa yanayoonekana kwenye jamii za kitanzania huchochewa na mfumo wa uzalishaji mali wa ubepari (Capitalism) ambao husisitiza maendeleo yanayohusisha jitihada binafsi badala ya jamii nzima kwa ujumla. Mfumo wa kibepari si tu umeathiri namna nzima ya uzalishaji mali ili kufikia maendeleo bali mahusiano na majukumu ya kijamii yamebadilika kwa kiasi kikubwa. Jamii zote za kitanzania zimetokana na mfumo wa ujamaa (Socialism) uliosisitiza umuhimu wa uzalishaji mali na maendeleo kwa juhudi za jamii nzima hivyo kila kitu kilikuwa chini ya umiliki wa jamii nzima ikiwamo makuzi sahihi za watoto kama taifa la baadae.
Ni vyema tukafahamu kuwa endapo watoto wanapitia ukatili na ama unyanyasaji basi hiyo ni akisi ya jamii zetu. Na kwa umuhimu huu basi, namna bora ya kuzuia na kukomesha unyanyasaji na ukatili wa watoto lazima uwe ni jukumu la jamii nzima na sio mzazi mmoja mmoja. Kutokana na ombwe la makuzi shirikishi katika jamii zetu ndio maana unyanyasaji na ukatili wa watoto umekithiri, jukumu la makuzi ya watoto limeachwa kwa wazazi wa watoto husika na hiyo kupelekea ubinafsi wa makuzi na endapo mtu mwingine atashughudia mtoto akipitia ukatili wengi wetu hatujihusishi tukidhani yule sio mtoto wetu hivyo kuliacha jambo hili kwa mzazi husika.
Jitihada sahihi lazima ziwe sehemu na zao la jamii husika kwani matatizo mengi huzaliwa kutokana na jamii zetu hivyo lazima jamii nzima iwe suluhisho la matatizo haya ya ukatili na unyanyasaji wa watoto. Tukumbuke wahusika wa ukatili na unyanyasaji wa watoto wako ndani ya jamii zetu hivyo ni vyema jamii nzima ikajikita kuhakikisha udhibiti sahihi unakuwepo ili watoto wetu wabaki salama. Kutokana na ombwe kwenye jamii zetu tumeacha malezi shirikishi na kujikita kwenye malezi binafsi na hii ndio huwa chanzo kikuu cha ukatili na unyanyasaji wa watoto.
Tukumbuke kuwa, maadili ni mali ya jamii nzima kwani muundo wake na utekelezaji wake hutokana na makubaliano ya jamii hivyo makuzi sahihi ya mtoto ni makubaliano sahihi ya jamii na endapo kutakua na uvunjifu wa maadili kutoka na makubaliano ya jamii basi wahusika huadhibiwa kutokana na kanuni na taratibu za jamii zetu. Ni muhimu zaidi kwa jamii kutambua ya kuwa, jukumu kubwa la jamii ni kuzuia unyanyasaji na ukatili wa watoto kwa kuzingatia makuzi sahihi. Kwa hali ilivyo sasa, watoto wanapitia unyanyasaji na ukatili wa hali ya juu na huku sababu mbalimbali za chanzo chake zikisahau kabisa jamii kama chanzo kikubwa cha anguko la makuzi sahihi ya watoto.
Wakati tukiwa tunatafuta njia sahihi ya kuwalinda watoto wetu dhidi ya unyanyasaji ni vyema tukaanzia kujitathimini kama jamii, kuangalia mapungufu yetu, kubadilisha tabia zetu kama jamii dhidi ya watoto na kuboresha makuzi shirikishi kama jamii. Ni kwa umuhimu huu basi, mabadiliko ya kweli yakaanza kwenye jamii yetu kwa manufaa ya Watoto, kwani, watoto ni mali ya jamii hivyo ni jukumu la jamii nzima kuhakikisha makuzi sahihi ya watoto. Ni jukumu la jamii kuzuia aina zote za unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto kwa nguvu zote, kuacha vitendo vyote vya kudhalilisha watoto kwa ama kutumia vibaya picha zao, kutwatumikisha, kutowaheshimu na aina nyinginezo za unyanyasaji wa watoto.
Kwa kuzingatia jitihada mbalimbali zilizopo kutoka kwa serikali na wadau wengine za maendeleo, ni muhimu sana mkazo wa ulinzi wa watoto ukarudi kwa jamii ili kuwa na jitihada za kudumu na zenye tija. Kwa umuhimu huu, ni vizuri kwa jamii zetu zikarejea kwenye misingi imara ya kutunza watoto kwa ushirikiano na kuacha ubinafsi kwenye makuzi ya watoto. Ni kutokana na ombwe hli la jamii tunaona watoto wengi wakipata malezi kutoka kwa dada wa kazi, mitandao ya kijamii, makundi rika, malezi binafsi na mengine mengi. Hayo yote hutokea endapo jamii inasahau majukumu yake ya awali na kudhani watoto watakuwa chini ya uangalizi wa wazazi na ama walezi wao tu. Watoto ni wetu sote hivyo tuanze na makuzi shirikishi na kuachana na makuzi binafsi ya watoto wetu.

Upvote
8