Malagarasi Hydropower Project - Loan Approved

Sijui ni mimi sina kumbukumbu; hivi mraji wa umeme wa Rufiji ukikamilika si tutakuwa na ziada ya umeme kama taifa? Kama ni ndiyo hatuna kipaumbele kingine zaidi ya kuanza mradi mpya wa umeme?
 
Safi sana Mzalendo wa kiafrica Rais wa AfDB bwana Adesina Akinwumi, tunataka kuachana na mikopo ya mabeberu. AfDB ni ya waafrika na itajenga Afrika
 
Sijui ni mimi sina kumbukumbu; hivi mraji wa umeme wa Rufiji ukikamilika si tutakuwa na ziada ya umeme kama taifa? Kama ni ndiyo hatuna kipaumbele kingine zaidi ya kuanza mradi mpya wa umeme?
Umeme ni bidhaa saleable tumezungukwa na nchi zina uhaba wa umeme.Kitakacofuata ni kujenga mkonga wa umeme kuuza nch jirani
 
Umeme ni bidhaa saleable tumezungukwa na nchi zina uhaba wa umeme.Kitakacofuata ni kujenga mkonga wa umeme kuuza nch jirani
Tutauza kwa "COST + mark up" au "below cost" kama tunavyowauzia Zanzibar?
 
Umeme ni bidhaa saleable tumezungukwa na nchi zina uhaba wa umeme.Kitakacofuata ni kujenga mkonga wa umeme kuuza nch jirani
Mnafikiria serikali zilizopita zilikuwa na wapumbavu kiasi ambacho walikuwa wanashindwa kukopakopa hovyo? I mean kukopa imekuwa sifa na kitu cha kushangilia siku hizi? Tena US $140 kwa nchi kama yetu? Huyu jamaa mpaka aondoke aitacha Tanzania kwenye madeni yasiyoelezeka. Ndiyo maana anataka kuua demokrasia ili aweze kumpachika mtu wa kumfichia madhambi yake siku atakapotoka.
 
Tutauza kwa "COST + mark up" au "below cost" kama tunavyowauzia Zanzibar?
Hawana hadhi ya kufanya majadiliano kama haya. Wanaokopa na hawa wapiga debe akili zao ni moja. Ni kama walivyokurupuka kununua ndege ambazo zinawaozea sasa hivi na zimeishaingiza hasara ya mamilioni japo inafichwa.
 
Mkuu serikali zilizopita zilifanya mengi mazuri.Kuanzia 2015 tumeanza kutafuta kujitegemea kiuchumi, ni lazima tukope ili tuwekeze na kuweka mazingira mazuri kwa uwekezaji.Wawekezaji wakija watalipa kodi na tutapunguza utegemezi na finally tutapata nguvu ya kukopa na kulipa.Sasa serikali inatakiwa kukopa sana kwa sasa ili kuongeza TAX BASE.Tunataka kuondokana na traditional taxation sources mambo ya kodi ya sigara, soda, bia nk
 
Ndivyo mnamvyomdanganya jamaa siyo? Haya.... siku zote ukweli huchelewa kufika lakini lazima utafika.
 
Jamani, kila kitu ni mkopo au msaada!!

SGR mkopo, Stigliers mkopo, flyover msaada, kupambana na covid misaada, ujenzi wa madarasa mkopo, ujenzi wa vyoo vya wanafunzi mkopo, ARVs msaada, chanjo za watoto misaada, ujenzi wa barabara kuu mikopo na misaada - ni kitu gani tunagharamia wenyewe? Kwa upande wa bajeti ya maendeleo, hela yetu inatosha kununulia ndege tu?
 
Safi sana Mzalendo wa kiafrica Rais wa AfDB bwana Adesina Akinwumi, tunataka kuachana na mikopo ya mabeberu. AfDB ni ya waafrika na itajenga Afrika
Wewe ndiyo mjinga kweli!! Hivi unajua kwenye hiyo AfDB ni nani mwenye hisa kubwa?

Kama hufahamu, hiyo bank wenye hisa kubwa ni EU na USA. Jielimisheni. Siyo kila chenye neno Africa ni cha Waafrika. Unakopa hapo AfDB, unalipa riba halafu hao AfDB inapokutana na wanahisa, wanaamua juu ya malipo ya wanahisa.

Leo hii, wazungu wakiondoa pesa yao AfDB, hiyo bank inayumba. Ndiyo maana wenye akili wakiwasikia wajinga wanawasema wazungu eti ni mabeberu, unajua kuwa ni maneno yanayotoka kwa mwendawazimu.

Angalia wanahisa 10 wakubwa wa AfDB, halafu nionesha nafasi ya donor country:

AfDB 10 biggest shareholders:

Nigeria: 9.1%; US: 6.5%; Egypt: 5.5%; Japan:5.4%;

South Africa: 4.9% Algeria: 4.1%; Germany: 4%;

Canada: 3.8%; Ivory Coast: 3.7%; France: 3.6%

Mpaka India ni wanahisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wapumbavu watasema huo mradi hauna uhusiano na maendeleo ya wana Kigoma.
 
Kila jambo mbele ya uso wa Tanzania ni muhimu sana
= Maendeleo ya miundombinu ni muhimu,
= Maendeleo ya kiuchumi ni muhimu,
= Maendeleo ya kisiasa ni muhimu,
= Maendeleo ya kiteknolojia pia ni muhimu.

Tusiwe vipofu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…