GE2025 Malaigwanan Kilimanjaro: Tunalaani wote wanaohamasisha maandamano

GE2025 Malaigwanan Kilimanjaro: Tunalaani wote wanaohamasisha maandamano

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966


Malaigwanan Kilimanjaro waahidi kuwachagua walinda amani na mshikamano wa Taifa_ Viongozi wa Jamii ya Kimasai nchini Tanzania maarufu kama (Malaigwanan) wametoa tamko lao rasmi kwa nchi nzima, la kuunga Mkono kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025, wakilaani uwepo wa hamasa ya kufanyika kwa maandamano siku hiyo wakiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua Viongozi wanaowataka.

Viongozi hao wametoa tamko hilo katika eneo la Donyomorwak Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro kwenye Mkutano wao wa kawaida wa Orkiama ambapo akisoma tamko hilo kwaniaba ya Viongozi hao, Bw. Jeremia Laizer, Katibu wa Malaigwanani Tanzania, ameeleza pia kwamba Jamii hiyo itamuunga Mkono Kiongozi mwenye kutanguliza mbele maslahi ya wananchi pamoja na kulinda amani na utulivu wa Tanzania.

"Tunawahimiza wananchi wote kudumisha amani, mshikamano na utulivu, kuanzia ngazi ya shina, kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa, kanda hadi Taifa zima, tukiepuka maneno ya uchochezi, migawanyiko, na fitina. Tuchague maendeleo, umoja, na mustakabali mwema wa vizazi vya sasa na vijavyo. Tuwe nguzo ya amani, nuru ya matumaini, na urithi wa thamani kwa Taifa letu. Tanzania kwanza, amani kwanza." Amesema Bwana Laizer.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa Mkutano huo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Namelok Sokoine amewapongeza malaigwanani hao kwa msimamo wao huo pamoja na kuonesha kuridhika na utendaji wa serikali ya awamu ya sita, akiwataka kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Jumatano ya Oktoba 29, 2025. Aidha baadhi ya Viongozi wengine wa jamii hiyo pia wameahidi kuwa mabalozi wa kueneza amani katika maeneo yao katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu, wakisisitiza athari za maandamano yasiyofuata taratibu kuwa ni pamoja na uharibifu na uvunjifu wa amani ambapo waathirika wakubwa mara zote wamekuwa wanawake, watoto pamoja na wazee.
 
Si tumekubaliana Watanzania ni waoga?
Mbona wanaanza kutoa mlio kila pande..
 
Ccm inapitapita kwenye makundi mbalimbali kufanya siasa zake, mara viongozi wa dini, mara viongozi wa kichifu na sasa ni malaigwanani. Hofu ya nini wakati nchi ipo sala? Kinachotafutwa ni haki, waandamanaji wana madai ya msingi waachwe waandamane kwa amani
 
Badala ya kupiga kampeni. Wao wamejikita kuzungumzia maandamano 😅
 
Kwa hali halisi hakuna maandamano, ni mikwara tu na serikali imewewesuka kwa mikwara tu inaanza kutafuta pa kushika isipeperuke kwa upepo uvumao! Kama wapo wataokaandamana haya itakuwa ni maajabu ya dunia kutokea Tanzania! Nani atajitokeza kuandamana kwenye maandamano yenye mikriti ya nguvu za dola kiasi hiki? Serikali itaingia kingi na itavuruga uchaguzi wake kwa mikono yake yenyewe, na totally huo uchaguzi ndio utakuwa umevurugika na mshindi hata wa kuzugia hatapatikana. huu mtiti ni wa kisaikolojia
 
Viongozi wa dini hasa wa madhehebu wako dilemma, wanashindwa kutoa matamko kwa huu mtiti. Huu mtiti ukiingia kichwakichwa unaharibu waumini na unaweza ukashushwa madhabahuni asubuhi tu!
 
Hivi Kilimanjaro na haya malayagwan wapi na wapi? Wangesema Arushaa au Manyara kidogo ingesound good.

Kwa Kilimanjaro Masai wachache sana hasa wilaya ya Hai na Siha
 
Viongozi wa dini hasa wa madhehebu wako dilemma, wanashindwa kutoa matamko kwa huu mtiti. Huu mtiti ukiingia kichwakichwa unaharibu waumini na unaweza ukashushwa madhabahuni asubuhi tu!
Jumapili baada ya ibada walituambie vijana wote tubaki kuna semina fupi wakawa wanaleta mambo haya haya wakaachwa hapo
 
MMeshindwa kuvumilia kuwadharau watanzania kwamba waoga, kwan wapi mmeshtuka sio waoga tena?
Maandamano yalikuwa yanakemewa na RPC Mroto wa Dodoma kidogo na RPC Dsm. Ila awamu hii yamekemewa na wote plus IGP wakaongezq na msemaji wa JW na bado wananachi wakamzodoa vilivyo katika comments section.

Wewe huogopi?
 
Mvumo tu wa upepo wa maandamano unavuma mpaka wanapepesuka! Je maandamano halisi si ndiyo yatatawang'oa kabisa?
 
Back
Top Bottom