Malalamiko juu ya show za Diamond abroad

Huyu nditi kila siku yeye ni kumponda diamond tuu!! Au anatafuta kick huyu?? Huyu bwa mdogo niaje ajee
 
ilishaona live show ya ali kiba, barnabas, ditto au amin? acha masihara wako watu wenye sauti zao bwana
 
ndio maana huwa sijutii thamani ya pesa yangu nikitoa kuingia ngwasuma, ni sebene nonstop mavocal ya ukweli na mauno ya uhakika.

nadhani diamond anahitaji kukaa karibu na banana zoro atanufaika na vingi sana.

aaah huyo msanii wa kona bar hadi bss tu hana jipya juu ya ku cross boda kama kweli maunda angekua mbali
 
mimi sioni ubaya akikoselewa ni vizuri akayabeba mapungufu yake ayafanyie kazi na siyo kubishana nayo hiyo itamshusha chini mara 1 ambaye kazi zake hazikosolewi ni mwenyezi mungu pekee.

We ni mpambanaji wa kweli, na unayajua maisha yanavyotaka big up.
 
Ajifunze kiduchu kwenye shows za P square,kuna baadhi ya nyimbo ( mf. Roll it) inarudiwa ktk Version 2 tofauti ambapo mojawapo wanacheza zaidi,Mungu mkubwa na atafika mbali.
 
Diamond ni msanii mzuri...anajielewa,anathamini kazi yake,ana juhudi,ana heshima sana,ni muungwana...Kitu anachomiss domo ni hiki kwa kweli,sauti nzuri stejini.....Ukiona show zake mara nyingi uwa anaimba mstari mmoja alafu utaona Mic anawasogezea washabiki wapokee mstari unaokuja...Sijawahi shuhudia domo akiimba wimbo mmoja mpaka mwisho bila kushusha mic chini,akiimba kidogo utamuona tuimbeee woteeee.....Kwa sasa analikimbilia kwa kasi soko la kimataifa,ila aangalie isije kuwa hajajiandaa na mahitaji ya soko alafu likam-disappoint ...Tunapenda anavyocheza tena sana ila haturidhiki na anavyoimba,atafute ata mtaalamu wa sauti amsaidie kucontrol sauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…