KERO Malalamiko kuhusu Hitilafu za Mfumo wa CAS katika Maombi ya Kujiunga na Vyuo vya Afya

KERO Malalamiko kuhusu Hitilafu za Mfumo wa CAS katika Maombi ya Kujiunga na Vyuo vya Afya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ndugu Katibu Mtendaji,

Napenda kuwasilisha kero na malalamiko yangu pamoja na ya waombaji wengi wanaotumia mfumo wa Central Admission System (CAS) kwa ajili ya kuomba kujiunga na vyuo vya afya kwa mwaka wa masomo 2026/2027.

Kwa takribani wiki moja sasa, mfumo wa CAS umekuwa ukikumbwa na changamoto kubwa zinazowakwaza waombaji na kuhatarisha uwezo wao wa kukamilisha maombi kwa wakati. Changamoto hizo ni pamoja na:

1. Kushindwa kutuma namba za uthibitisho (Validation Codes) za usajili wa CAS. Mara nyingi mfumo hautumi kabisa namba hizo, na pale zinapotumwa hufika baada ya muda mrefu kiasi kwamba zinakuwa tayari zimeisha muda wake wa matumizi (expired), hivyo kushindwa kutumika.

Kushindwa kupokea na kuthibitisha malipo yaliyokwisha kufanyika.

2. Waombaji wengi wamelipia ada za maombi lakini mfumo hauonyeshi malipo hayo au kuchelewa kuyathibitisha, jambo linalowazuia kuendelea na hatua za uchaguzi wa kozi na vyuo.

3. Mfumo kushindwa kufunguka au kufanya kazi kwa ufanisi kwa siku sita mfululizo. Hali hii imekuwa ikisababisha usumbufu mkubwa kwa waombaji wanaojaribu kuingia kwenye akaunti zao na kukamilisha maombi.

Tunafahamu kuwa tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni 10 Julai 2026. Endapo changamoto hizi zitaendelea, kuna uwezekano mkubwa wa vijana wengi kukosa fursa ya kuomba na hatimaye kukosa nafasi za kujiunga na vyuo vya afya, si kwa sababu ya kutokidhi vigezo bali kutokana na matatizo ya mfumo.

Kutokana na hali hiyo, tunaomba majibu na ufafanuzi kutoka NACTVET kuhusu:

1. Je, ni nini chanzo cha hitilafu hizi za mara kwa mara?

2. Je, ni hatua gani za haraka zimechukuliwa kurekebisha mfumo?

3.Je, kuna mpango wa kuongeza muda wa maombi iwapo changamoto hizi zitaendelea?

4.Je, NACTVET ina mkakati gani wa muda mrefu wa kuboresha mfumo wa CAS ili uwe wa kuaminika, wa haraka na rafiki kwa waombaji?

Tunaamini taasisi yenu itapokea maoni haya kwa uzito unaostahili na kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha haki na fursa za waombaji wote zinalindwa.

Wako kwa dhati,

Mdau wa Elimu na Udahili wa Vyuo vya Afya Tanzania

KERO YA NACTEVET.jpg
 
Back
Top Bottom