Habari, mimi ni mkazi wa Gongo la Mboto Kituo Kipya. Kuna club/bar inaitwa UBENA SPORT CLUB iliyopo karibu na reli ambayo imekuwa ikitusumbua sana sisi wakazi wa eneo hili kutokana na kelele kubwa za muziki.
Muziki wao unapigwa kwa sauti kubwa kiasi kwamba tunashindwa kupata usingizi. Mara nyingi huanza kupiga muziki kuanzia saa moja jioni na kuzima karibu saa tisa au saa kumi kasoro alfajiri.
Tunaomba mamlaka husika ziangalie suala hili na kuweka utaratibu kwa hizi club na bar zilizopo karibu na makazi ya watu. Ikiwa wanataka kuweka muziki kwa sauti kubwa basi wahakikishe wanaweka vifaa vya kuzuia kelele (soundproof) ili wasisumbue wananchi wanaoishi maeneo ya karibu.
Mtu anapotoka kazini anahitaji muda wa kupumzika, lakini kutokana na kelele hizi tumekuwa tukikosa usingizi na kuathirika katika maisha ya kila siku.
Tunaomba serikali na viongozi wa eneo hili walifanyie kazi suala hili ili wananchi waweze kuishi kwa amani.