KERO Malalamiko kuhusu kuunganishwa na CWT bila ridhaa ya Walimu wapya Uvinza

KERO Malalamiko kuhusu kuunganishwa na CWT bila ridhaa ya Walimu wapya Uvinza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi walimu wapya walioajiriwa katika Wilaya ya Uvinza tunakabiliwa na changamoto ya kuingizwa moja kwa moja katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT) bila ridhaa yetu.

Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba makato ya ada ya uanachama yameanza kufanyika kwenye mishahara yetu bila sisi kutoa idhini ya kujiunga na chama hicho.

Tunaomba mamlaka husika zitoe ufafanuzi kuhusu utaratibu uliotumika kutuingiza kwenye chama hicho na kuanza makato hayo bila ridhaa yetu.

Pia, tunaomba suala hili lifuatiliwe ili haki na maamuzi ya kila mtumishi yaheshimiwe kwa mujibu wa taratibu zinazotumika.
 
CwT inasaidia nini walimu mpaka wanaungànishwa bila idhini Yao ?.

Je inawasaidia kupata nyumba, gari ,mashamba ,ruzuku
 
Back
Top Bottom