KERO Malalamiko kuhusu mabadiliko ya vigezo vya udahili kwa Wanafunzi wanaotaka kujiendeleza kielimu

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero yangu ni kuhusu mabadiliko ya vigezo vya udahili vinavyowekwa na NACTE na TCU bila kuzingatia changamoto zinazowakabili wanafunzi tuliosoma chini ya vigezo vya zamani.

Mimi ni mmoja wa watu waliosoma kozi ya afya na sasa ninataka kujiendeleza kielimu. Hata hivyo, nimekutana na kikwazo cha kutakiwa kuwa na somo la Fizikia (Physics), ilhali wakati ninasoma kozi yangu ya awali, hitaji hilo halikuwepo.

Hali hii inatuweka katika wakati mgumu sisi tuliosoma kwa kufuata vigezo vilivyokuwepo wakati huo. Kwa nini tubadilishiwe masharti baada ya kumaliza masomo yetu, kiasi cha kutuzuia kuendelea na elimu?

Naomba NACTE na TCU zifafanue: Je, mabadiliko ya vigezo vya udahili yanazingatia wanafunzi waliomaliza masomo yao chini ya mfumo wa zamani? Tunaomba kuwe na utaratibu wa mpito unaowapa nafasi wanafunzi hawa kujiendeleza bila kuathiriwa na masharti mapya ambayo hayakuwepo walipoanza masomo yao.
 
Ungekuwa specific kwamba mwaka gani kozi flani ilikuwa haihitaji Physics, Lakini mwaka flani na kozi flani kigezo cha Physics kikawekwa kwa kozi flani.
 
Kero yangu ni kuhusu mabadiliko ya vigezo vya udahili vinavyowekwa na NACTE na TCU bila kuzingatia changamoto zinazowakabili wanafunzi tuliosoma chini ya vigezo vya zamani.

Mimi ni mmoja wa watu waliosoma kozi ya afya na sasa ninataka kujiendeleza kielimu. Hata hivyo, nimekutana na kikwazo cha kutakiwa kuwa na somo la Fizikia (Physics), ilhali wakati ninasoma kozi yangu ya awali, hitaji hilo halikuwepo.

Hali hii inatuweka katika wakati mgumu sisi tuliosoma kwa kufuata vigezo vilivyokuwepo wakati huo. Kwa nini tubadilishiwe masharti baada ya kumaliza masomo yetu, kiasi cha kutuzuia kuendelea na elimu?

Naomba NACTE na TCU zifafanue: Je, mabadiliko ya vigezo vya udahili yanazingatia wanafunzi waliomaliza masomo yao chini ya mfumo wa zamani? Tunaomba kuwe na utaratibu wa mpito unaowapa nafasi wanafunzi hawa kujiendeleza bila kuathiriwa na masharti mapya ambayo hayakuwepo walipoanza masomo yao.
malalamiko yako haujayaweka wazi. Ungesema moja kwa moja ni kozi gani hapo awali haikuhitaji Physics lakini kwa sasa kozi hiyo hiyo ina uhitaji wa Physics
 
Back
Top Bottom