MALALAMIKO KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA HALMASHAURI NA UONGOZI WA NEWALA DC

MALALAMIKO KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA HALMASHAURI NA UONGOZI WA NEWALA DC

Nesta2

New Member
Joined
Nov 3, 2026
Posts
2
Reaction score
1
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Abdalah Nandonde,ameanzisha sera mpya na katili kwa kuchukua fedha zote za uendeshaji wa ofisi (OC)(Huletwa na serikali kuu kwa vitengo na idara) pamoja na fedha zilizotengwa kwa ajili ya posho za watumishi, akieleza kuwa fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kutengeneza gari linalotumika katika shughuli za ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri. Hatua hii imeathiri kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa shughuli za kawaida za ofisi pamoja na uwezo wa watumishi kupata stahiki zao kwa wakati ukizangatia hali ngumu ya maisha na ukata uliopo ndani ya Halmashauri.
Matumizi ya fedha hizo kwa madhumuni hayo yanapaswa kuchunguzwa kwa kina ili kubaini kama fedha za OC na posho za watumishi zimetumika kwa mujibu wa bajeti, mipango ya matumizi na taratibu za usimamizi wa fedha za Serikali za Mitaa.
Ni muhimu pia kubaini kiasi cha fedha kilichochukuliwa, matumizi yaliyofanyika na kama kulikuwa na idhini na msingi wa kiutawala wa kuelekeza fedha hizo katika matengenezo ya gari.
Aidha, Abdalah Nandonde amekuwa akitumia lugha chafu, matusi na kauli za kudhalilisha dhidi ya baadhi ya watumishi wa Halmashauri katika mazingira ya kazi. Mwenendo huu umesababisha hofu na kushusha morali ya baadhi ya watumishi katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa msingi huo, mamlaka husika zinapaswa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu matumizi ya fedha za OC na posho za watumishi, pamoja na mwenendo wa kiuongozi wa Mkurugenzi. Hatua stahiki zichukuliwe endapo uchunguzi utathibitisha ukiukwaji wa taratibu za fedha, maadili ya utumishi wa umma au haki na heshima ya watumishi.
Lengo ni kuhakikisha kuwa fedha za umma zinalindwa, watumishi wanapata stahiki zao na Halmashauri ya Wilaya ya Newala inaendeshwa kwa uwazi, uwajibikaji na kwa kuzingatia maslahi ya wananchi na watumishi.
 
Naye aache dhuruma, kwanini asitumie fedha za mapato ya ndani kutengeneza hilo gari? Baadae ukifuatilia taarifa ya matumizi utasikia kiasi fulani kimetumika kukarabati gari hilo hilo tena. Nachoka kabisa
 
Naye aache dhuruma, kwanini asitumie fedha za mapato ya ndani kutengeneza hilo gari? Baadae ukifuatilia taarifa ya matumizi utasikia kiasi fulani kimetumika kukarabati gari hilo hilo tena. Nachoka kabisa

Huyu anatamaa ya pesa kaka na Wala dhumuni siyo matengenezo ya gari. Pesa zaidi mill. 100 anafanya matangenezo yepi? Kama Halmashauri hii isingekuwa kwenye Mpango wa Kupewa OC kutokea serikali kuu hiyo gari isingetengenezwa. Huyu ni mtu mbinafsi, mmbabaishaji na mwizi
 
Back
Top Bottom