Habari JF,
Nina dukuduku kutoka Mkoa wa Manyara kuhusu Shule ya Sekondari Endasak. Wahitimu wa Kidato cha Sita wa mwaka 2026 wanatakiwa kuchangia Sh100,000 kila mmoja kwa ajili ya gari.
Kinachotia wasiwasi zaidi ni madai kwamba mwanafunzi asiyetoa mchango huo hazuiliwi tu kushiriki katika shughuli husika, bali pia hapewi cheti cha kuhitimu.
Swali langu ni hili: Je, utaratibu huu uko sahihi? Gari hilo litawanufaishaje wahitimu ambao baada ya kumaliza masomo hawatakuwa tena wanafunzi wa shule hiyo?
Ikiwa mchango huo ni wa hiari, kwa nini inadaiwa kuwa cheti cha kuhitimu kinazuiwa kwa wale ambao hawajalipa? Na ikiwa ni mchango wa lazima, ni mamlaka gani iliyoidhinisha utaratibu huo?
Naiomba Wizara ya Elimu na mamlaka husika za elimu zichunguze suala hili na kutoa ufafanuzi ili kujulikana kama madai haya yana msingi wa kisheria.
Vyeti vya kuhitimu vinapaswa kushughulikiwa kwa kuzingatia taratibu rasmi, bila wanafunzi kuwekewa masharti yasiyoeleweka.
Asanteni.