A
Anonymous
Guest
Naomba kuwasilisha malalamiko kuhusu mwenendo wa dereva wa lori la serikali katika Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe, ambaye anadaiwa kusababisha ajali kwa bodaboda kutokana na uzembe wa kufuata kanuni za usalama barabarani.
Dereva huyo anapofika kwenye barabara zenye vumbi kuelekea eneo la Iwiji, amekuwa akiendesha bila kufuata upande wake wa barabara, hali inayowaweka waendesha bodaboda na watumiaji wengine wa barabara katika hatari ya kupata ajali.
Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili na kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha usalama wa watumiaji wa barabara na kuzuia ajali zinazoweza kusababishwa na uzembe wa uendeshaji.
Dereva yeyote, iwe wa gari binafsi au la serikali, anapaswa kuzingatia sheria za barabarani na kulinda maisha ya wananchi.