KERO Malalamiko kuhusu ulanguzi wa tiketi za mabasi ya mkoani unaofanywa na mawakala

KERO Malalamiko kuhusu ulanguzi wa tiketi za mabasi ya mkoani unaofanywa na mawakala

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mara nyingi wamiliki wa kampuni hawajui Hili, mambo ya kukata tiketi Online yameua upigaji ule wa kizamani hasa Kwa safari za kutoka mkoa mmoja kwenye mwingine...

Biashara za mabasi Tanzania kwenye Management huwa zina tabu Sana hasa hasa kampuni ikiwa kubwa coz Bosi kazungukwa na wapigaji kibao wanaotafuta namna ya Ku survive....Kwa kampuni uliyosema Kwanza haina Bosi mmoja, ina mabosi zaidi ya nane but mgt ina kiongozi wanaoelewek maana ni ndugu wameamua kuungana chini ya jina moja but Kila ndugu ana magari Yake....

Zipo kampuni very smart ambazo mlanguzi halambi hata Mia yaani kwenda ofisini kwao kukata tiketi ni kujisumbua Tu
 
Leo asubuhi nilikosa kazi nikawa naangalia tickets online (Busbora.co.tz) za kutoka sehemu mbalimbali,nikacheck Kahama kwenda Dodoma kwa safari ya kesho 28/9/2026.

Katarama na Kaizirege hakuna siti yaani 0!!😀

Hii itakuwa michezo!! Wengine wote zipo siti mpaka 55,how? Nikajifariji yatakuwa mambo ya Polo haya!!
kampuni kubwa kweye ruti ngome tiketi huisha haraka kidogo.

Hii ni kazi ya wa wamiliki wa magari. Kwangu mimi nadhani huu mchezo unachezwa kati ya wakata tiketi na hao ''mawakala''. Wana-create hali ya uongo ya basi kujaa ili wauze tiketi kwa kuweka ''cha juu''. Na baadae wanagawana kati ya dalali na wale wafanyakazi wa basi. Au pengine inawezekana hata wamiliki wa mabasi wako kwenye huu mchezo? Tatizo kubwa ni kuwa wanasiasa-viongozi wengi wameingia kwenye biashara hivyo kunakuwa na mgongano wa maslahi. Mimi siku zote huwa nasema akiingia mfanya biashara mwenye mtaji mkubwa na anayejua kuendesha biashara ya kusafirisha abiria kwa ''kujali wateja'' ataua hizo kampuni nyingine zote.
mambo yaleyale ya kariakoo nishafika dukani mwenyewe lakini hapohapo dukani unazungukwa na madalali/mawinga na mwenye duka akiwa hapohapo
 
kampuni kubwa kweye ruti ngome tiketi huisha haraka kidogo.


mambo yaleyale ya kariakoo nishafika dukani mwenyewe lakini hapohapo dukani unazungukwa na madalali/mawinga na mwenye duka akiwa hapohapo
Huu umeshakuwa kama utamaduni wa mtanzania. Mpaka kwenye mitumba, unaweza kukuta nguo kwenye banda lakini wauzaji ni wengi na wala huwezi kujua mmiliki ni nani. Hizi ''ajira'' za kukaa idle, mtu hafanyi kazi bali anaishi kwa ujanja ujanja zimetapakaa nchi nzima hasa mijini.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Ikifika mwisho wa mwaka hali ndio itakuwa mbaya zaidi.
 
Si mkate online. Yaani maisha walivyosimplify kweli unaenda kukata tiketi ofisini?
Kabla ya kumshauri ulitakiwa usome na ulielewe tatizo lake, naona unamshauri jambo ambalo alianza kulifanya na akashindwa kupata tikiti kwani ilionesha basi limejaa.
 
Mimi nilipanda Bus la Osaka lenye Choo ndani nililipa 45k kwenye Ticket na Receipt inasoma 55k na mtu akalipa 55k Akili Mtu wangu
 
Tarehe 13/09/2026, nilikuwa na safari kutoka Mbagala, Dar es Salaam, kuelekea mkoani Lindi. Kabla ya kwenda stendi, nilikagua upatikanaji wa tiketi mtandaoni na nikagundua kuwa karibu mabasi yote yalikuwa yamejaa kwa muda ambao nilipanga kusafiri. Niliamua kwenda Stendi ya Mbagala Rangi Tatu nikitumaini kupata nafasi kwenye basi au gari jingine.

Nilipofika stendi, nilipokelewa na mawakala wa kampuni ya mabasi ya Tashriff. Walinieleza kuwa kuna basi lililokuwa likitokea Tanga na kwamba bado lilikuwa na nafasi. Jambo la kushangaza ni kwamba basi hilo lilikuwa miongoni mwa mabasi niliyoyaona mtandaoni likionyesha kuwa limejaa.

Wakala alinipatia tiketi ya mashine yenye jina la abiria tayari pamoja na nauli ya kwenda Lindi. Hata hivyo, aliniambia niongeze Shilingi 10,000 kwa sababu, kwa maelezo yake, "magari yanasumbua sana." Nilikataa kulipa fedha hiyo na baada ya kusisitiza, hatimaye nililipishwa kiasi kilichoandikwa kwenye tiketi.

Nilipokuwa katika ofisi yao ya mizigo, iliyopo karibu na vyoo vya kulipia ndani ya stendi, nilisikia abiria wengine wakilalamika kuhusu kuuziwa tiketi kwa bei kubwa tofauti na bei halisi. Pia nilimwona mmoja wa mawakala akiwa na tiketi nyingi za mashine ndani ya begi lake.

Hali hii inanifanya kujiuliza: Je, kuna utaratibu ambao mawakala hununua au kuchukua tiketi nyingi mapema na kisha kuziuza kwa abiria kwa bei wanazopanga wenyewe?

Ikiwa ni kweli, hii ni changamoto inayopaswa kuchunguzwa kwa sababu inaweza kuwa inawaumiza abiria wanaotegemea huduma hizi, hasa wakati wa msongamano wa wasafiri.

Naiomba kampuni ya Tashriff, pamoja na mamlaka husika, kulifuatilia suala hili na kuchunguza mwenendo wa mawakala wake katika Stendi ya Mbagala Rangi Tatu. Abiria wanapaswa kulipia nauli halali iliyoainishwa, bila kulazimishwa kutoa fedha za ziada zisizoeleweka.

Nina nakala ya tiketi yangu kama ushahidi wa tukio hili na niko tayari kuiwasilisha kwa mamlaka husika kwa ajili ya uchunguzi.
Nauli halisi ya kwenda lindi ni kiasi gani bosi natamani one day nisafiri huko
 
Watanganyika kila sehemu nikilio tu huyu mzenji atawaua zaidi.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Hii ni kazi ya wa wamiliki wa magari. Kwangu mimi nadhani huu mchezo unachezwa kati ya wakata tiketi na hao ''mawakala''. Wana-create hali ya uongo ya basi kujaa ili wauze tiketi kwa kuweka ''cha juu''. Na baadae wanagawana kati ya dalali na wale wafanyakazi wa basi. Au pengine inawezekana hata wamiliki wa mabasi wako kwenye huu mchezo? Tatizo kubwa ni kuwa wanasiasa-viongozi wengi wameingia kwenye biashara hivyo kunakuwa na mgongano wa maslahi. Mimi siku zote huwa nasema akiingia mfanya biashara mwenye mtaji mkubwa na anayejua kuendesha biashara ya kusafirisha abiria kwa ''kujali wateja'' ataua hizo kampuni nyingine zote.
Hao wamiliki wa mabus hawawez kubali
Check dangote alitaka kuuza cement nchi nzima kwa sh 10,000/tuu wapampiga biti
 
Huu umeshakuwa kama utamaduni wa mtanzania. Mpaka kwenye mitumba, unaweza kukuta nguo kwenye banda lakini wauzaji ni wengi na wala huwezi kujua mmiliki ni nani. Hizi ''ajira'' za kukaa idle, mtu hafanyi kazi bali anaishi kwa ujanja ujanja zimetapakaa nchi nzima hasa mijini.
huu ni wizi wa wazi
 
Anasema online kunaonesha mabasi yamejaa. Kama uhuni uliokuwa ukifanywa mwanzo SGR, mtu ananunua tiketi nyingi halafu anaziuza.
Treni ya kawaida ya Kigoma-Tabora-Dar wakati wote mfumo online unaonesha nafasi zimejaa.
Bado tatizo ulilosema lipo.
Kwenye basi nyingi za baadhi ya route zinatatizo hilo hilo.
Zingine watu wanashika siti hawalipii kabisa (booking).
Wanaziachia baadaye gari limeshaondoka.
 
Back
Top Bottom