kampuni kubwa kweye ruti ngome tiketi huisha haraka kidogo.Leo asubuhi nilikosa kazi nikawa naangalia tickets online (Busbora.co.tz) za kutoka sehemu mbalimbali,nikacheck Kahama kwenda Dodoma kwa safari ya kesho 28/9/2026.
Katarama na Kaizirege hakuna siti yaani 0!!😀
Hii itakuwa michezo!! Wengine wote zipo siti mpaka 55,how? Nikajifariji yatakuwa mambo ya Polo haya!!
mambo yaleyale ya kariakoo nishafika dukani mwenyewe lakini hapohapo dukani unazungukwa na madalali/mawinga na mwenye duka akiwa hapohapoHii ni kazi ya wa wamiliki wa magari. Kwangu mimi nadhani huu mchezo unachezwa kati ya wakata tiketi na hao ''mawakala''. Wana-create hali ya uongo ya basi kujaa ili wauze tiketi kwa kuweka ''cha juu''. Na baadae wanagawana kati ya dalali na wale wafanyakazi wa basi. Au pengine inawezekana hata wamiliki wa mabasi wako kwenye huu mchezo? Tatizo kubwa ni kuwa wanasiasa-viongozi wengi wameingia kwenye biashara hivyo kunakuwa na mgongano wa maslahi. Mimi siku zote huwa nasema akiingia mfanya biashara mwenye mtaji mkubwa na anayejua kuendesha biashara ya kusafirisha abiria kwa ''kujali wateja'' ataua hizo kampuni nyingine zote.
Huu umeshakuwa kama utamaduni wa mtanzania. Mpaka kwenye mitumba, unaweza kukuta nguo kwenye banda lakini wauzaji ni wengi na wala huwezi kujua mmiliki ni nani. Hizi ''ajira'' za kukaa idle, mtu hafanyi kazi bali anaishi kwa ujanja ujanja zimetapakaa nchi nzima hasa mijini.kampuni kubwa kweye ruti ngome tiketi huisha haraka kidogo.
mambo yaleyale ya kariakoo nishafika dukani mwenyewe lakini hapohapo dukani unazungukwa na madalali/mawinga na mwenye duka akiwa hapohapo
Sasa mtu akilangua si anatumia ela mzeeHawa siyo madalali labda hujui maana ya dalali. Hawa ni walanguzi.
Kabla ya kumshauri ulitakiwa usome na ulielewe tatizo lake, naona unamshauri jambo ambalo alianza kulifanya na akashindwa kupata tikiti kwani ilionesha basi limejaa.Si mkate online. Yaani maisha walivyosimplify kweli unaenda kukata tiketi ofisini?
Na wewe hujaelewa!Acha ushamba madalali kila sehemu wapo na sio kosa kisheria wew umeshindwa kununua tiket online unaenda ofisin alafu aunalalamika daah kweli wew matonya
Kaka una kichwa kigumu, hapo usichoelewa ni nini?Si mkate online. Yaani maisha walivyosimplify kweli unaenda kukata tiketi ofisini?
We umeelewaNa wewe hujaelewa!
Nauli halisi ya kwenda lindi ni kiasi gani bosi natamani one day nisafiri hukoTarehe 13/09/2026, nilikuwa na safari kutoka Mbagala, Dar es Salaam, kuelekea mkoani Lindi. Kabla ya kwenda stendi, nilikagua upatikanaji wa tiketi mtandaoni na nikagundua kuwa karibu mabasi yote yalikuwa yamejaa kwa muda ambao nilipanga kusafiri. Niliamua kwenda Stendi ya Mbagala Rangi Tatu nikitumaini kupata nafasi kwenye basi au gari jingine.
Nilipofika stendi, nilipokelewa na mawakala wa kampuni ya mabasi ya Tashriff. Walinieleza kuwa kuna basi lililokuwa likitokea Tanga na kwamba bado lilikuwa na nafasi. Jambo la kushangaza ni kwamba basi hilo lilikuwa miongoni mwa mabasi niliyoyaona mtandaoni likionyesha kuwa limejaa.
Wakala alinipatia tiketi ya mashine yenye jina la abiria tayari pamoja na nauli ya kwenda Lindi. Hata hivyo, aliniambia niongeze Shilingi 10,000 kwa sababu, kwa maelezo yake, "magari yanasumbua sana." Nilikataa kulipa fedha hiyo na baada ya kusisitiza, hatimaye nililipishwa kiasi kilichoandikwa kwenye tiketi.
Nilipokuwa katika ofisi yao ya mizigo, iliyopo karibu na vyoo vya kulipia ndani ya stendi, nilisikia abiria wengine wakilalamika kuhusu kuuziwa tiketi kwa bei kubwa tofauti na bei halisi. Pia nilimwona mmoja wa mawakala akiwa na tiketi nyingi za mashine ndani ya begi lake.
Hali hii inanifanya kujiuliza: Je, kuna utaratibu ambao mawakala hununua au kuchukua tiketi nyingi mapema na kisha kuziuza kwa abiria kwa bei wanazopanga wenyewe?
Ikiwa ni kweli, hii ni changamoto inayopaswa kuchunguzwa kwa sababu inaweza kuwa inawaumiza abiria wanaotegemea huduma hizi, hasa wakati wa msongamano wa wasafiri.
Naiomba kampuni ya Tashriff, pamoja na mamlaka husika, kulifuatilia suala hili na kuchunguza mwenendo wa mawakala wake katika Stendi ya Mbagala Rangi Tatu. Abiria wanapaswa kulipia nauli halali iliyoainishwa, bila kulazimishwa kutoa fedha za ziada zisizoeleweka.
Nina nakala ya tiketi yangu kama ushahidi wa tukio hili na niko tayari kuiwasilisha kwa mamlaka husika kwa ajili ya uchunguzi.
Hao wamiliki wa mabus hawawez kubaliHii ni kazi ya wa wamiliki wa magari. Kwangu mimi nadhani huu mchezo unachezwa kati ya wakata tiketi na hao ''mawakala''. Wana-create hali ya uongo ya basi kujaa ili wauze tiketi kwa kuweka ''cha juu''. Na baadae wanagawana kati ya dalali na wale wafanyakazi wa basi. Au pengine inawezekana hata wamiliki wa mabasi wako kwenye huu mchezo? Tatizo kubwa ni kuwa wanasiasa-viongozi wengi wameingia kwenye biashara hivyo kunakuwa na mgongano wa maslahi. Mimi siku zote huwa nasema akiingia mfanya biashara mwenye mtaji mkubwa na anayejua kuendesha biashara ya kusafirisha abiria kwa ''kujali wateja'' ataua hizo kampuni nyingine zote.
huu ni wizi wa waziHuu umeshakuwa kama utamaduni wa mtanzania. Mpaka kwenye mitumba, unaweza kukuta nguo kwenye banda lakini wauzaji ni wengi na wala huwezi kujua mmiliki ni nani. Hizi ''ajira'' za kukaa idle, mtu hafanyi kazi bali anaishi kwa ujanja ujanja zimetapakaa nchi nzima hasa mijini.
Treni ya kawaida ya Kigoma-Tabora-Dar wakati wote mfumo online unaonesha nafasi zimejaa.Anasema online kunaonesha mabasi yamejaa. Kama uhuni uliokuwa ukifanywa mwanzo SGR, mtu ananunua tiketi nyingi halafu anaziuza.